Kingine kinachomwangusha JK ni lugha!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kingine kinachomwangusha JK ni lugha!!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Az 89, May 24, 2012.

 1. Az 89

  Az 89 JF-Expert Member

  #1
  May 24, 2012
  Joined: Nov 20, 2011
  Messages: 1,613
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  Mh. Rais kikwete katika kampeni zake za mwaka 2005 alikuja na slogan au falsafa ya "MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA" Ikibebwa Ari mpya, nguvu mpya na kasi mpya!!!, kwa lugha hii alioitumia alikamata hadi viongozi wa dini, na watu wa nyanja zote!!! Kwa masikini ambao kwao Neno"MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA" Lilibeba sanduku la matumaini mapya, kujichomoa kwenye jalala la umasikini na kujiweka angalau katika uwezo wa kumpa maji mtu mwingine anaejiskia na kiu! KILICHOTOKEA ni tofauti na walivyotegemea...lindi la umaskini, rushwa, ufisadi viliongezeka! UCHAGUZI WA 2010 alikuja na "ARI ZAIDI, KASI ZAIDI NA NGUVU ZAIDI", Lugha hii pia iliwahadaa watu japo wengi walizinduka ilibaki kwa watu wa vijijini ambao walitoa nafasi kwa mara nyingine japo sina uhakika sana Kama alishinda tena au lah! kwa sababu Mambo yaliyojadiliwa kwenye WHITE PAPER HAYAJATIMIZWA....! Kwa sasa kila kitu kimebadilika! Watu wamechoka wameshajua kuwa "MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA" ILIKUWA ZUBAISHA *****.. ILIKUWA LUGHA YA UONGO! Kuweni makini 2015.
   
 2. Az 89

  Az 89 JF-Expert Member

  #2
  May 24, 2012
  Joined: Nov 20, 2011
  Messages: 1,613
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  Imekosewa kuwa posted but i think unaweza kunisoma! Kikwete katika chaguzi zote mbili ametumia lugha au falsafa ya "MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA" kitu ambacho imekuwa kinyume kabisa na hiyo lugha! Umaskini umeongezeka! Ufisadi usiseme! Watu wa nyanja zote hata viongozi wa dini wameshashtuka kuwa ile ilikuwa ni Danganya toto! Kuweni makini 2015 kuna watu wapo chimbo wanatengeneza falsafa nyingine ya kuwashika.
   
 3. O

  Otorong'ong'o JF-Expert Member

  #3
  May 24, 2012
  Joined: Aug 17, 2011
  Messages: 31,212
  Likes Received: 10,557
  Trophy Points: 280
  Na ndo hiyo inammaliza na kuimaliza ccm. One mistake one goal.
   
 4. leroy

  leroy JF-Expert Member

  #4
  May 24, 2012
  Joined: Dec 8, 2010
  Messages: 843
  Likes Received: 128
  Trophy Points: 60

  Unamaanisha Watanzania hupenda kuweka Matumaini yao kwa wanasiasa badala ya kuchapa kazi..?
  Akija mwingine kutoka upande wa pili mtamtumaini?
   
 5. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #5
  May 24, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,813
  Likes Received: 83,195
  Trophy Points: 280
  ....Ulikuwa ni usanii tu wa kuhakikisha anaingia Ikulu lakini hana hata chembe moja ya leadership quality hata ya kuwa mjumbe wa nyumba kumi kumi achilia mbali kuwa Rais wa nchi.
   
 6. Az 89

  Az 89 JF-Expert Member

  #6
  May 24, 2012
  Joined: Nov 20, 2011
  Messages: 1,613
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  nafikiri waTanzania wengi huangalia mtu! Hawamwangalii Raisi kama Taasisi, kwani we hukumbuki walisema rais waliyemchagua ni handsome?!
   
 7. MANGUNGO

  MANGUNGO JF-Expert Member

  #7
  May 24, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 1,538
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 133
  Ari zaidi,kasi zaidi na nguvu zaidi.
   
 8. N

  Njoka Ereguu JF-Expert Member

  #8
  May 24, 2012
  Joined: Apr 7, 2012
  Messages: 822
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 35
  Hiyo ndiyo siasa. Bila hivyo unadhani wangevukaje. Subiri 2015 hivi sasa slogan nyingi na tamu zinatungwa.
   
 9. Az 89

  Az 89 JF-Expert Member

  #9
  May 24, 2012
  Joined: Nov 20, 2011
  Messages: 1,613
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  Aliweka slogan kubwa ambayo ameshindwa kuitendea haki!
   
 10. Maundumula

  Maundumula JF-Expert Member

  #10
  May 24, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 7,055
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Kichwa tofauti habari tofauti!
   
 11. samstevie

  samstevie JF-Expert Member

  #11
  May 24, 2012
  Joined: Nov 11, 2011
  Messages: 202
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Haya mambo yote yanakuja kutokana na tabia ya kuangalia upepo unavuma wapi badala ya kuwa na strategies za kukuza uchumi na huduma za jamii kupitia phases mbalimbali tangu nchi ipate uhuru. Kwa kuangalia mfano wa slogan hizo mbili ni dhahiri CCM ilishindwa kuwa na vipaumbele ambavyo vingewashawishi wananchi wawapigie kura.Kwa kuanzia na MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA 2005 Mgombea Urais wa CCM alitazamia kufanya mabadiliko makubwa ya kiuchumi huduma za jamii,kuboresha miundombinu na upatikanaji wa ajira mpya but mambo hayakwenda sawa. Hii ya ari zaidi, Kasi zaidi na nguvu zaidi ni kujaribu kugeuza nyekundu kuwa njano lakini ladha ni ileile nothing changed na impact yake tumeona ni inflation kuwa kubwa, ukosefu wa ajira na kuongezeka kwa umaskini vilivyochagizwa na vitendo vya kifisadi.Hakuna jipya na sera na ahadi zisizotekeleka. Ahadi za kampeni nyingi zilikuwa za uongo kama ambayo naikumbuka mimi ni ujenzi wa flyovers kwa jiji la Dar es salaam tena kwa miaka 5 ya utawala sijui kwa miundombinu gani inayosapoti hii ishu. Watanzania tuwe makini na si kushabikia tu maumivu ya miaka 10 ya utawala mbovu ni hatari kwa maendeleo yetu.
   
 12. Az 89

  Az 89 JF-Expert Member

  #12
  May 24, 2012
  Joined: Nov 20, 2011
  Messages: 1,613
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  Hata jina lako linasadifu yaliyomo kichwani, kasome Theory of communication!
   
 13. Az 89

  Az 89 JF-Expert Member

  #13
  May 24, 2012
  Joined: Nov 20, 2011
  Messages: 1,613
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  well!, well said mkuu!
   
 14. f

  fikirikwanza JF-Expert Member

  #14
  May 24, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 5,935
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Kikwete ni mwiba mdogo uloua tembo. ni maajabu lakini ndo imetokea Tanzania kuwa na rais rahisi kuliko hata mjumbe wa nyumba 10.
   
 15. Osaka

  Osaka JF-Expert Member

  #15
  May 24, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 1,766
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Well said!
   
 16. N

  Njoka Ereguu JF-Expert Member

  #16
  May 24, 2012
  Joined: Apr 7, 2012
  Messages: 822
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 35

  Well, pamoja na uzuri wa hoja yako, ila naona kama kichwa cha habari hakiendani na maelezo yako. Maana vitu kama hizo Ari mpya, kasi mpya ----- siyo lugha hizo ni kauli mbiu, kwa hiyo ingekuwa vyema ungesema hizo kauli mbiu zimempoza has baadaya ya kushindwa kuwaletea watanzania maisha bora aliyoahidi katika ilani ya uchaguzi 2005 na kumpatia tiketi ya kuwaongoza watz.
   
 17. Az 89

  Az 89 JF-Expert Member

  #17
  May 24, 2012
  Joined: Nov 20, 2011
  Messages: 1,613
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  sawa mkuu japo lugha inatumika kutengeneza slogan
   
 18. M

  Mbwambo JF-Expert Member

  #18
  May 24, 2012
  Joined: Nov 25, 2008
  Messages: 626
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 33
  Ni kweli kichawa cha habari ni tofauti na maneno lakini tumeelewa alikuwa anataka kusema nini?

  Jamani kweli JK alinifanya nipange foleni kubwa kwenda kumpigia kura baada ya miaka mingi iliyopita nilikuwa nimesusa kwenda kupiga kura.
  Yaani ile lugha yake aliyoji- advertise hata mimi nilitekwa nakuamni kwamba JK anafaa lakini baada ya miaka kadhaa kupita nikatambua kwamba hakufaa. Kweli mimi nimegundua kwamba sisi watanzania hatujakuwa makini sana kwa kungalia nani anafaa. Nimeona tofauti kubwa katika awamu yake ya pili alipotuomba tena kura WATANZANIA wengi hasa wa mjini hawakumpenda na hawakumpigia kura. LAKINI WA VIJIJINI NINADHANI walihitaji elimu ya kutosha na hii ni kazi ambayo Dr. Slaa na mwenyekiti wa chadema waifanye kwa moyo wao wote hii miaka 4 iliyobakia na actually sio minne ni mitatu sasa. Jitahidini kuwatembelea wananchi wa vijijini waelimishwe waelewe na wawe tayari kuleta mabadiliko makubwa kwa kuchagua chadema iongoze serikali yetu.
  Hata hivyo nina imani chadema walishinda uchaguzi lakini katiba yetu ilichangia sana kumpa ushindi JK, maana haijawahi nchi kuonyesha kwamba kuna ufisadi mkubwa kiasi cha JK kubadili baraza la mawaziri mara kwa mara?


  Kweli JK alishindwa kabisa kuonyesha kile alichosema kwetu kabla hatujampa kura na baada ya kumpa kura hali yetu kimaisha ni ngumu ajabu.
  Mungu ibariki chadema na Tanzania yote
   
 19. Az 89

  Az 89 JF-Expert Member

  #19
  May 24, 2012
  Joined: Nov 20, 2011
  Messages: 1,613
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  sawa mkuu!
   
 20. MAMMAMIA

  MAMMAMIA JF-Expert Member

  #20
  May 24, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 3,822
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 0
  KAULI MBIU MPYA ZA JK na CCM:
  Umasikini zaidi, Njaa zaidi, Ujinga zaidi, Maradhi zaidi, Giza zaidi, Mikoa mingi zaidi, Wilaya Nyingi zaidi, Mawaziri wengi zaidi, Wezi na Wizi zaidi - Yote haya yanapelekea "Maisha Bora kwa Wateule na Watawala na Maisha Duni kwa Watanzania wengi."
   
Loading...