mkalimani4
Member
- Nov 30, 2016
- 26
- 29
Nina miaka miwili nimekuwa nikitumia King'amuzi cha Continental ambacho mmiliki wake ni mkazi wa Jiji la Mwanza.
Nilikipenda king'amuzi hicho kwa kipindi hicho kutokana na kuvutiwa na matangazo yao kuwa hakina malipo ya kila mwezi.
Baada ya muda mfupi King'amuzi hicho kikabadilika na kuwa cha kulipia Tshs. 12,000/= kwa mwezi wakati hakina hata channel moja inayoonyesha mpira mubashara.
Niliendelea kufuata matakwa yao ya kulipia kila mwezi na nikishindwa kulipia ghafla wanakata channel zote isipokuwa Star tv tu.
Majuzi nimegundua kuwa ni haki yangu kuangalia channel hata kama nisipolipia kama vile; TBC1, ITV, CHANNEL TEN, CLOUDS TV . Haki hiyo nimeigundua baada ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania "TCRA" kutupasha habari njema.
Mpaka leo hii tarehe 12/12/2017 King'amuzi hicho hakijatii Agizo la TCRA wala kutupasha habari kuwa ni lini watatekeleza Agizo hilo halali.
Kutokana na kunyimwa haki yangu ya Msingi ya kupata Habari, nipo kwenye mchakato wa kutafuta Mwanasheria ili niweze kuwafungulia kesi ya Madai ya Tshs. 50,000,000/= kwa kuninyima haki zangu za Msingi.
Vielelezo nitakavyotumia ili kuthibitisha Madai yangu:-
1. Risiti ya kuuziwa King'amuzi
2. King'amuzi chao cha Continental.
3. Gazeti lililotoa Tangazo la TCRA
4. TCRA ili wathibitishe kuwa walitoa Agizo hilo.