Kinana na Nape waonja joto ya jiwe Bunda

Lai Otieno

JF-Expert Member
Aug 13, 2013
311
90
Baada ya kuingia mkoani Mara kwa mbwembwe,leo jioni katika viwanja vya wazi mjini Bunda katibu Mkuu wa CCM na katibu wa itikadi na uenezi wamekumbana na zomea zomea baada ya Nape kusema kuwa Wassira aliwakaribisha wapinzani Ikulu kunywa chai sasa wana njaa na wanataka tena Chai.

Imebidi Kinana atumie busara kwa Kusema hata Wasira hajatimiza wajibu wake wa kuwaletea wana Bunda maendeleo ikiwemo maji, hapa mjini Bunda polisi wanahaha kuwasaka vijana kwa kuwaweka ndani kwa taharuki iliyojitokeza.

Nawasilisha
 
wassira.png
Mh. Steven Wassira Mbunge wa Bunda
 
Namhurumia sana Kinana , anatembea kwa aibu sana baada ya msigwa kuweka wazi ujangili wake , hadi amepauka uso !
 
Akili za Nape hazina tofauti na Masogange.

Nilicheka sana jana kusikia eti nape alikuwa mlokole Nsumba akitokea Ngudu na alikuwa mshamba sana. Wa kwanza kuamka kwenda kwenye mapambio. Hii ndio siri ya unafiki. Atueleze je bado anaimani na Mwana wa Mtu licha ya unafiki wake?
 
Siasa za Mkoa wa Mara ni ngumu. Anayetaka kuzimudu anapaswa kutambua mood ya wananchi. Wakati fulani Lowassa katika Kijiji cha Kinyambwiga (Bunda) alipata wakati mgumu kwa kuwaambia wafugaji wauze mifugo ili wapate tija. Kaulizwa swali, mbona wewe hatujakutaka upunguze fedha zako benki?

Waziri Mkuu mwaka juzi alionja joto kali mjini Musoma baada ya DC wa hapo kukwepa kumtambulisha Mbunge wao Nyerere. Pinda alipopanda jukwaani akashituka kuona mambo yameharibika. Ikabidi amkaribishe Nyerere jukwaani, ndipo wakakubali kumsikiliza. Lakini kwenye hotuba akasema 'wananchi mnatibiwa, dawa zipo'. Hapo akachafua hali ya hewa. Akaambiwa wazi wazi...mwongo, mwongo. Mmoja akasema, "Ninyi wakubwa ndiyo matibiwa Ulaya na India".

Wakati fulani Lowassa alifika Tarime katika mkutano wa hadhara. Chacha Wangwe alipanda jukwaani na kumwambia, "Waziri Mkuu sikiliza, wewe ni mwanaume na mimi ni mwanaume-wote tumetahiriwa, kwa hiyo hapa ujue unazungumza na wanaume, utupatie majibu ya kweli kuhusu mgodi wa North Mara". Hiyo ndiyo Mara.

Msisahau kuwa mwaka 1995 Mwalimu Nyerere alipofika Tarime kumnadi Mkapa, alipopolewa mawe. Huo ndiyo mkoa wa Mara!!
 
mkuu nakumbuka siku hiyo Pinda ilibidi atumie sana Busara ndo mambo yakapoa,wale hawanaga utania

watu wanaojitambua huwa sio mpaka wakae madarasani na kwenye vimbweta,nashukuru nimewafaham watu wa mara kuwa wanajitambua sana
 
Nape na Kinana maifikiri mtapata mteremko kama mlioupata kwa Wasukuma,Mara ni wabishi by nature hawadanganyiki kiurahisi kama mlivyowadanganya sehemu zingine

Nape hawatasita kukuzomea ukileta siasa za maji taka huko,wana akili kukuzidi hao
 
Back
Top Bottom