Kinana na Nape waendelea na ziara Musoma, Mara.Wafanya mkutano mkubwa Musoma

MwanaDiwani

JF-Expert Member
Mar 22, 2013
5,536
2,264

Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwa amepanda kwenye kivuko cha MV Musoma kinachovusha watu kutoka Wilaya ya Rorya na Musoma kikitokea Kinesi leo akielekea Musoma mjini tayari kwa kumalizia ziara yake mkoani Mara, ambapo amekagua miradi mbalimbali ya maendeleo na kuhamasisha wananchi kushiriki shughuli za maendeleo ikiwa ni pamoja na kukagua utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM, Kinana amemaliza ziara yake ya mikoa ya Shinyanga, Simiyu na Mara leo kwa kufanya mkutano mkubwa wa hadhara kwenye uwanja wa Mukendo mjini Musoma akiongozana na Katibu wa NEC Itikadi, Siasa na Uenezi wa CCM Nape N nauye.Ndugu Kinana amesema ni haki ya wananchi kuhoji maendeleo yao kwani wanasiasa wa vyama mbalimbali vikiwemo vya upinzani vilipita na kutoa ahadi tena wengine waliahidi kutoa asali na maziwa huku wengine wakiahidi wananchi kuwa wakiwachagua watajenga barabara za marumaru.


Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwa katika kivuko hicho pamoja na wananchi, kushoto aliyembeba mtoto ni Katibu Mkuu wa UWT Taifa Amina Makilagi

Katibu wa NEC Itikadi, Siasa na Uenezi wa CCM Nape Nnauye akiwa amesimama katika ukingo wa kivuko hicho pamoja na wananchi.


Msafara wa magari ukitoka kwenye kivuko cha MV Musoma mara baada ya kuwasili mjini Musoma leo ukitokea wilayani Rorya.



Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana wa tatu kutoka kulia na Katibu wa NEC Itikadi, Siasa na Uenezi wa CCM Nape Nnauye wa pili kulia wakishuka kwenye kivuko cha MV Musoma mara baada ya msafara wake kuwasili mjini Musoma leo


Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na Katibu wa NEC Itikadi, Siasa na Uenezi wa CCM Nape Nnauye wakiwapungia mkiono wananchi waliojitokeza kuwapokea mjini Musoma


Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiangalia vikundi mbalimbali vya sanaa mjini Musoma

Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiongozwa na Jailos Chilewa Mhandisi mkazi wa mradi mkubwa wa maji wa ziwa Victoria uliopo Bukanga Makongo nje kidogo ya Manispaa ya Musoma wakati alipokuwa akikagua ujenzi wa mradi huo leo.


Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimsikiliza Jailos Chilewa Mhandisi mkazi wa mradi mkubwa wa maji wa ziwa Victoria uliopo Bukanga Makongo nje kidogo ya Manispaa ya Musoma wakati akitoa maelezo ya mradi huo, kutoka kushoto niKatibu wa NEC Itikadi, Siasa na Uenezi wa CCM Nape Nnauye na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mara Bw.Christopher Sanya


Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiendelea na ukaguzi wa mradi huo.



Ukaguzi ukiendelea



Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipata maelezo kutoka kwa mganga mkuu wa mkoa wa Mara Bw. Samson Winani wakati akikagua mradi wa hospitali ya mkoa ya Rufaa Kwanga mjini Musoma, ujenzi wa mradi huo unatarajiwa kuanza kuendelea hivi karibuni.

Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikata utepe kuashiria uzinduzi wa ofisi ya CCM Kata ya Bweri mjini Musoma.

Hii ndiyo ofisi yenyewe.


Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipokea zawadi jogoo kutoka kwamwenyekiti wa shina namba 6 mama ThabithaAmina Idd mara baada ya kutembelea shina hilo na kuongea na wanachama.



Katibu Mkuu wa Umoja wa wanawake UWT Mama Amina Makilagi akiwahutubia wana Musoma leo kwenye mkutano wa hadhara katika viwanja vya Mukendo mjini Musoma leo.



Katibu wa NEC Itikadi, Siasa na Uenezi wa CCM Nape Nnauye akizungumza na wanaMusoma leo kwenye viwanja vya Mukendo.


Hawa ni miongozi mwa wananchi waliohudhuria katika mkutano huo leo.




Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wana Musoma leo.

 
[h=3]CCM ina deni ililokopeshwa la kuwatumikia wananchi. CCM haina muda wa kurumbana na wapinzani wanaotafuta maneno na matukio kuendesha siasa zao za kilaghai na misimu.

CCM iliongoza, inaongoza na itazidi kuongoza huku vyama vingine vikifuata kwa nyuma.
[/h]
Thank you wananchi
 
Kwenye kivuko mlikuwa nao mkionyesha mko nao sambamba na kwenye magari yenu muwapakie basi mkawaache pale katikati ya mji wa musoma maarufu kama mjini stendi ya zamani.
 
Back
Top Bottom