Si mimi ninayesema, bali ni maneno yake mwenyewe Peter msigwa kwenye twitter yake. Nimeitafuta Twit yake na kuwawekea hapa.Mkuu usiturushe roho. Hebu fafanua tafadhali.
- Peter Msigwa
12 August via Twitter
Kuna mzungu kakamatwa na Pembe za ndovu Kamtaja WEKA MBALI NA TEMBO Kwamba kazipata kutoka kwake. SOON WATAUMBUKA.
Kwa hiyo Tundu Lissu na Msigwa wakionekama mahakamani tayati wameshashitakiwa??? Mbona sijaona gazeti lolote?
Sasa angefanyeje ilhali keshautangazia umma kwamba asipoombwa msamaha ataenda mahakamani? Hizi tabia za kukimbilia mahakamani zinawahusu CCM wote. Hujiulizi walipata wapi ujasiri wa kuwapeleka mahakamani akina Lwakatare, Kileo na makamanda wengine kwa mashitaka ya ugaidi huku wakijua ni mashitaka ya kutunga? Hiyo ni hulka tu ya CCM kuamini kwamba mahakama ni ya kwao hivyo itawatetea.
Sasa kama Kinana ana ubia na TOLL, na mkurugenzi wa TOLL kakamatwa na pembe za ndovu, kama Kinana anamiliki meli ambazo ndiyo zinaaminiwa kusafirishwa pembe za Ndovu, ni kwa vipi yeye asihusishwe? Kwanini hazijawa meli za watu wengine au bandari ya nchi kavu ya mtu mwingine? Naamini ataifuta tu hii kesi kabla hata haijafika pabaya, maana ushahidi wa mazingira tu unatosha kumtia hatiani.
Ngoja msigwa wamzomue amezoea kuropoka sana.
Tumpe hongera Kinana kwa kumfikisha mahakamani huyo mropokaji, kiukweli kwa kuropoka kwake kuhusu Kinana, hata chama changu kilichafuka sana.
Umesema kweli kuwa "......sidhani............" Hii inamaanisha haujui kama ambavyo na huyo Kinana uliyekurupuka kumtetea asivyojua wenzake wana taarifa zipi. Sijui wewe kama mleta thread unataka kutuambia kitu gani ambacho wewe haujui ila unadhani tu.
Kama unataka kutumia hoja hiyo kumtia hatiani bwana Kinana basi nisewe umepotoka, mahakamani kesi haziamuriwi kwa kutumia ushahidi mwepesi hivyo.
Itakumbukwa kuwa Kinana ni shareholder wa hiyo kampuni ya Sharaf shipping, na ukiwa shareholder haimaanishi una husika na day to day operations za kampuni. Kampuni inakuwa na management na shareholder wapo kwa ajili ya ku-finance na ku-enjoy dividends, sasa iweje Kinana ahusishwe na ujangili au usafirishaji wa pembe za ndovu?, hapo wa kuhusishwa moja kwa moja ni watendaji wa kampuni ya Sharaf shipping na watu wa TRA.
Kuhusu mfano wako; pale Bilicanas kuna vijana uwa wanakamatwa na polisi kwa kubwia unga, je nikisema Mbowe ahusishwe na unga kwa kuwa yeye ni mmiliki wa bilicanas utanielewa?, ni sawa sawa na ndege inavyo wasafirisha "punda" au wabeba unga, huwezi kumuhusisha owner wa ndege kuwa yeye ana husika, ila utawahusisha wale wakaguzi wa airport, nadhani umeelewa mkuu.
Kufungua kesi ni jambo lingine. Na kushinda kesi ni jambo lingine. Kwa ufinyu wa akili yako tayari umesha kuja na hukumu ya kushindwa Mh. Mch. Msigwa! Kwani hukumsikia Mh. Balozi Kagasheki akisema ujangili ni biashara ya baadhi ya wanasiasa walioshika nyadhifa ngazi za juu?
Hata Kinana akishinda mahakamani, T 2015 CDM lazima tuta mng'ang'ania awa fufue ndovu wetu wote walio kufa kwenye mikono yake.
Kama unataka kutumia hoja hiyo kumtia hatiani bwana Kinana basi nisewe umepotoka, mahakamani kesi haziamuriwi kwa kutumia ushahidi mwepesi hivyo.
Itakumbukwa kuwa Kinana ni shareholder wa hiyo kampuni ya Sharaf shipping, na ukiwa shareholder haimaanishi una husika na day to day operations za kampuni. Kampuni inakuwa na management na shareholder wapo kwa ajili ya ku-finance na ku-enjoy dividends, sasa iweje Kinana ahusishwe na ujangili au usafirishaji wa pembe za ndovu?, hapo wa kuhusishwa moja kwa moja ni watendaji wa kampuni ya Sharaf shipping na watu wa TRA.
Kuhusu mfano wako; pale Bilicanas kuna vijana uwa wanakamatwa na polisi kwa kubwia unga, je nikisema Mbowe ahusishwe na unga kwa kuwa yeye ni mmiliki wa bilicanas utanielewa?, ni sawa sawa na ndege inavyo wasafirisha "punda" au wabeba unga, huwezi kumuhusisha owner wa ndege kuwa yeye ana husika, ila utawahusisha wale wakaguzi wa airport, nadhani umeelewa mkuu.
Kwisha habari yake hiyo fidia atakayolipia chadema. watamkopesha kweli ?kutoka kwny ruzuku Kama
Mkuu,
Kwa wanasheria wataelewa hapa, kuna hii ishu inaitwa defarmation, nadhani ndio litakuwa shitaka namba moja kwa mchungaji Msigwa, na utakumbuka kutokana na kashfa hiyo kuwa Kinana ni jangili, ili sababisha Kinana avunje makubaliana na partners wake na ili m-cost si chini ya milioni 300 pesa za Tanzania. Sasa unaweza kupata picha ya hiyo fidia atakayolipa Msigwa kwa Kinana.