Kinana alipowafunga midomo wapambe wa Lowassa! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kinana alipowafunga midomo wapambe wa Lowassa!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by KIM KARDASH, Feb 26, 2012.

 1. K

  KIM KARDASH JF-Expert Member

  #1
  Feb 26, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 5,083
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Katika kikao cha NEC ya CCM kilichofanyika hivi karibuni kulizuka mjadala mkali juu ya mabadiliko ya katiba ya ccm, huku mkongwe wa siasa na mshauri wa rais, Kingunge Ngombale- Mwiru katika hali ya kushangaza akikataa kukubaliana na maamuzi juu ya mabadiliko yoyote katika katiba.

  Akiongea kwa jazba,Ngombale alikaririwa akipinga kwanza,kuundwa kwa Baraza la ushauri ambalo litakua na viongozi wakuu wastaafu kwa maana ya marais na mawaziri wakuu wastaafu akidai hatua hiyo itafanya chama kikose watu wa kukilea japo haikueleweka alikua anamaanisha nini!

  Mapendekezo ya marekebisho ya katiba ambayo hatimaye yalipitishwa na wajumbe wa NEC, yanasema viongozi wakuu wastaafu "hawatakuwa wajumbe wa vikao vya chama ngazi ya taifa;" badala yake wanaundiwa Baraza la Ushauri ambalo litatoa ushauri kwa CCM na serikali zake.

  Kwa mujibu wa maamuzi hayo, wastaafu wataitwa kuhudhuria vikao vya kitaifa pale tu uongozi wa chama utakapoona kuwa "busara zao zinahitajika, hususan katika masuala magumu na nyeti."

  Pia bwana kingunge alipinga mpango wa kuzuia wabunge kujilimbikizia vyeo vinavyoambatana na posho pia kwa kuwa wajumbe wa NEC.Tayari wabunge pia ni madiwani katika halmashauri wanazotoka na wanahudhuria vikao kama kama madiwani wengine.

  Kuhusu mpango wa kuzuia wabunge kuwa wajumbe wa NEC, Ngombale alisema, "Huwezi kufanya haya kama unakitakia mema chama hiki. Labda kama mtakuwa mnathibitisha madai kuwa kuna agenda iliyojificha."

  Akiongea kwa jazba kali bwana Ngombale alisema, "Naomba mniweke kwenye kumbukumbu kwamba nimelipinga jambo hili." akaendelea kufoka kwa kudai bila kuthibitisha kwamba utaratibu wa kupata wajumbe wa NEC kutoka wilayani eti utakuwa na athari kubwa kwa chama hicho kwenye siku za usoni; kwani utakifanya chama kuwa na makundi makubwa ya ugomvi na visasi!!!

  Katika hali inayoonyesha kama walikua wamejipanga kabla ya bwana Ngombale kuchangia, Peter Serukamba , mjumbe wa NEC na mbunge wa Kigoma Mjini,nae alisimama na kupinga utaratibu mpya wa kutaka kuwaundia chombo maalum viongozi wakuu wastaafu na kuwatumia katika kukishauri chama.

  Lakini hoja dhaifu za Peter akifuatiwa na Kingunge,zilizimwa na Mh.Abdulrahman Kinana aliyepigilia msumari wa mwisho kwa kueleza kuwa "hata wastaafu wenyewe wamekubaliana na jambo hili." iweje nyie ndio mpinge kwa nguvu leo??

  Huku akimuangalia rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi, Kinana alisema, "Au siyo Mzee Mwinyi." Mwinyi aliitikia kwa kutikisa kichwa kuashiria kukubaliana.

  Naye Katibu wa NEC,Nape Nnauye akizungumzia nafasi ya wajumbe wa NEC wanaogombea kutoka wilayani huku wakitakiwa kuwa "viongozi wa kazi za muda wote," alisema zipo nafasi kama ile ya mwenyekiti wa wilaya, diwani, mbunge – kwa mujibu wa kanuni za uchaguzi wa CCM – ambazo si za ajira lakini za muda wote.

  "Hawa wanafanya kazi za chama za kila siku ndani ya chama, si waajiriwa wala hawalipwi mshahara. Hivyo hawa wajumbe wa NEC wa wilaya pia watakuwa katika kundi hili," alifafanua.

  Wakati huohuo, marekebisho hayo yameongeza idadi ya wajumbe wa NEC kutoka kati ya 100 na 200 hadi karibu 370 na kufanya uwakilishi wa wananchi(wanachama wa ccm)kuwa mkubwa zaidi kwenye vikao vya maamuzi vya chama hali ambayo imezidi kukisogeza zaidi chama karibu na wanachama asilia wa chama hicho ambao ni wakulima na wafanyakazi.

  Kikao hicho sasa kitakuwa na wajumbe10 kutoka Tanzania bara, 10 kutoka Visiwani na wengine 10 wa kuteuliwa na mwenyekiti wa CCM taifa.

  Pia wamo wanaoingia kwa nafasi zao kama wenyeviti wa CCM mkoa, spika na waziri mkuu wanaotokana na CCM, wenyeviti na makatibu wa jumuiya za chama na makamu wa rais wa Muungano na Zanzibar wanaotokana na CCM.

  Wajumbe wengine watakaotoka kwenye vyombo vya uwakilishi ni wabunge 10 (bara 8, Zanzibar 2);
  wajumbe watano wa Baraza la Wawakilishi na wajumbe wanaochaguliwa kutoka wilayani ambao ni 221.
  Vilevile watakuwamo wajumbe kutoka kwenye jumuiya za chama, 15 kutoka UWT (bara 9, Zanzibar 6); UVCCM 10 (bara 6, Zanzibar 4) na watano kutoka Wazazi (bara 3, Zanzibar 2).
   
 2. J

  JokaKuu Platinum Member

  #2
  Feb 26, 2012
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,734
  Likes Received: 4,958
  Trophy Points: 280
  ..Kinana ni fisadi papa wa enzi za awamu ya pili.

  ..anahusika na kuwaleta nchini Waarabu wa Loliondo.
   
 3. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #3
  Feb 26, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Hapa JK anaandaa mazingira ya kumwingiza mwislam ikulu 2015!
   
 4. M

  Mabewa Senior Member

  #4
  Feb 26, 2012
  Joined: Oct 30, 2011
  Messages: 128
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  wewe mnyisansu ni lidude linalowaza udini kila sekunde ya akili yako...na sidhani kama unaakili sawasawa hata nyumbani pia unaonekana una akili za kula kulala.
   
 5. kanininyo

  kanininyo Member

  #5
  Feb 26, 2012
  Joined: Dec 19, 2011
  Messages: 16
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hawa magamba hawana cha maana.
   
 6. NGUVUMOJA

  NGUVUMOJA JF-Expert Member

  #6
  Feb 26, 2012
  Joined: Jul 1, 2011
  Messages: 1,353
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Ubongo wako umejaa udini tu. Mambo mengine sifuri eeenh?
   
 7. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #7
  Feb 26, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  It is a matter of time! Mtayakumbuka maneno yangu.
   
 8. Kalunguine

  Kalunguine JF-Expert Member

  #8
  Feb 26, 2012
  Joined: Jul 27, 2010
  Messages: 2,544
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Mkuu mbona mdini hivyo?post zako zimejaa udini tu.kama vipi kawe shehe au kasisi.
   
 9. Kalunguine

  Kalunguine JF-Expert Member

  #9
  Feb 26, 2012
  Joined: Jul 27, 2010
  Messages: 2,544
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Kwa staili hii EL mbuyu unaokitesa chama unakuwa ushang'olewa
   
 10. Nyalotsi

  Nyalotsi JF-Expert Member

  #10
  Feb 26, 2012
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 5,104
  Likes Received: 551
  Trophy Points: 280
  lisemwalo lipo,kama halipo linakuja. Acha tuongee tu,hawa jamaa wanajua kuchapana bakora tu, wametuharibia nchi kwa udhaifu wao. Kwa nn kila wakiwepo wao nchi inakuwa na madeni kibao na hatuon hizo fedha wanafanyia nn na zinapelekwa wapi na magenge yao ya ujambazi.
   
 11. Nyalotsi

  Nyalotsi JF-Expert Member

  #11
  Feb 26, 2012
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 5,104
  Likes Received: 551
  Trophy Points: 280
  sipendi watu wanaoquote ujumbe wote aafu coment zao maneno yao kumi tu!
   
 12. mopaozi

  mopaozi JF-Expert Member

  #12
  Feb 26, 2012
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 3,290
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  ..."Sikukutana na kikwete barabarani..."-edward ngoyai lowasa
   
 13. bucho

  bucho JF-Expert Member

  #13
  Feb 26, 2012
  Joined: Jul 13, 2010
  Messages: 4,542
  Likes Received: 425
  Trophy Points: 180
  hiyo ni kweli kabisa . Hana maana huyu msomali.
   
 14. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #14
  Feb 26, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,316
  Likes Received: 1,785
  Trophy Points: 280
  His interest are at stake with this uncontrolled speed!lazima apiganie maslahi yajayo.
   
 15. only83

  only83 JF-Expert Member

  #15
  Feb 26, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 5,252
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  Serukamba nae ni fisadi mdogo anayechipukia...
   
 16. Kunta Kinte

  Kunta Kinte JF-Expert Member

  #16
  Feb 26, 2012
  Joined: May 18, 2009
  Messages: 3,660
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Hauna lolote la maana la kukumbukwa wewe!!!

  Labda tukukumbuke kama bingwa wa *****!!
   
 17. Job K

  Job K JF-Expert Member

  #17
  Feb 26, 2012
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 6,847
  Likes Received: 2,774
  Trophy Points: 280
  Mkuu umeona eeeeh! Eti mtu anachukua post nzima sijui maana yake nini? Uvivu tu!
   
 18. Shinto

  Shinto JF-Expert Member

  #18
  Feb 26, 2012
  Joined: Dec 6, 2010
  Messages: 1,781
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Are you serious dude? St. Nyerere aliangamiza uchumi wa nchi hii kwa mikono yake beyond repair! Mpaka Mwinyi na Salimu walipokuja na sera za kufufua uchumi! Au wewe ulikuwa unachapa divai tu?
   
 19. Ronal Reagan

  Ronal Reagan JF-Expert Member

  #19
  Feb 26, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,738
  Likes Received: 1,451
  Trophy Points: 280
  Ziko angle nyingi za kulitazama jambo hili.....mimi nataka kuliangalia kutoka Gorbachev angle.
   
 20. Songoro

  Songoro JF-Expert Member

  #20
  Feb 26, 2012
  Joined: May 27, 2009
  Messages: 4,136
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 0
  kajifunze kwenye katiba kama huwa tunaangali dini kwenye kuchagua Rais!!
   
Loading...