Kinana na timu yake waendelea na ziara katika vijiji mbali mbali na kuhutubia umati wa watu, Sikonge
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana kabla ya kufanya mkutano mkubwa alizungumza na vijana wa Kijiji cha Vijana cha Path Finder Green Village alipotembelea na kukagua miradi mbalimbali iliyopo katika kijiji hicho chenye jumla ya vijana 88. Kijiji hicho kiko umbali wa Km 40 kutoka Sikonge Mjini. Katibu Mkuu yuko katika ziara ya kuimarisha uhai wa chama, kukagua miradi inayotekelezwa kwa kufuata IIani ya uchaguzi ya CCM, kukagua maandalizi ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa pamoja na kusikiliza kero za wananchi na kuzitatua.
Kijiji hicho kinaendesha miradi ya ujenzi wa nyumba za kuishi vijana, ufugaji kuku, ufugaji nyuki, kilimo, kujifunza ufundi wa aina mbalimbali..
Kijiji hicho kimenzishwa na Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Fatma Mwassa kwa lengo la kuwapunguzia umasikini vijana waliokosa fulsa ya elimu wilayani humo.
Akiwa kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa CCM,wilayani Sikonge mkoani Tabora, Kinana alizungumzia matatizo makubwa yanayowakumba wakulima wa zao la Tumbaku huku akionesha kabrasha la taarifa ya ukaguzi na uchunguzi wa chama cha Ushirika cha WETCO LTD,ambalo linaeleza namna wakulima wa Tumbaku walivyoibiwa mamilioni ya fedha.
Aidha,Wananchi wa Sikonge wameulalamikia ubadhilifu huo mkubwa wa fedha uliofanywa na viongozi wa vyama vya ushirika,na kwamba wamekuwa wakicheleweshewa malipo ya fedha zao na pia kutolipwa kwa wakati,jambo ambalo limekuwa likiwakera wakulima hao.
Kinana aliongeza kusema kuwa vyama vya ushirika vimeanzishwa kwa wingi na wajanja wachache kwa ajili ya kujinufaisha wao na kuwanyona na kuwadhuruma wakulima wa Tumbaku, hivyo Kinana alisema kuwa amekisikia kilio cha wakulima hao,na ameahidi kuyafikisha malalamiko hayo kwa Rais Jakaya Kikwete na hatimaye kupatiwa ufumbuzi wa haraka.
Katibu Mkuu, Kinana akihutubia umati wa watu katika uwanja wa CCM, Sikonge.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Fatma Mwassa akihutubia umati wa watu.
Mbunge wa jimbo la Sikonge, Said Mkumba akiwaeleza wananchi kuhusu mafanikio na malengo yaliyoko mbeleni katika kutimiza ahadi kama zilivyoainishwa katika Ilani ya Uchaguzi ya CCM.
Kwa vile ndani ya CCM kuna upendo na furaha, huu ulikuwa ni muda wa kufurahia na kuburudika baada ya mkutano uliohudhuriwa na umati mkubwa wa wananchi.
Baadhi ya vijana wapatao 70 katika kijiji cha PathFinder Green City,wilayani Sikonge,mkoani Tabora. Wakimweleza Kinana kuhusiana na mafanikio na changamoto katika miradi yao mbali mbali ya kujitegemea.
Katibu Mkuu wa CCM, Kinana akisaidia kufunga tumbaku huku akisaidiwa na mmoja wa vijana wa Kituo cha Vjana cha Path Finder Green Village, wilayani Sikonge, Tabora.
ZeMarcopolo likes this.