Kinana afanya Ziara ya kushtukiza Tabora...!

Kinana afanya Ziara ya kushtukiza Tabora...!

Hapa ndo uone jinsi gani mfumo wa kupashana taarifa ndani ya CCM ulivyo na walakini. Hivi wale viongozi wa CCM wa Kijiji, Kata,Wilaya na Mkoa hawayaoni na kuyawasilisha matatizo ya wanachi wao hadi viongozi kama kina kinana ama Nape wazunguke zunguke kuangalia?. Kwahiyo hizi nafasi zingine zina manufaa gani kwa CCM na kwa watanzania?. Kweli nyani akikaribia kufa miti yote kuteleza, hata tawi la CCM linafunguliwa na KINANA jangiri halafu wananchi wanatulia tu!!!. Kweli amani hii ndo imetufikisha hapa,tunashindwa hata kuhoji na kukaripia tabia chafu kama za kina KINANA.
 
inabidi Kinana Afanye kazi ya ziada ili Kukiokoa CCM irudi kwenye line yake ili awe salama zaidi na mali zake zote.. anajua CCM ikiondoka uhalali wa utajiri wake wa kutisha nao uko hatihati..
 
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana amefanya ziara ya kushtukiza katika Mkoa wa Tabora asubuhi hii ambapo amekutana na Mkuu wa Mkoa huo Bi Fatma Mwasa na pia kukutana na viongozi wa Chama wa Mkoa ambapo alifanya kikao kidogo na viongozi hao akisisitiza juu ya utekelezaji wa Ilani na maagizo ya Mkutano Mkuu wa kufanya Mikutano ya ndani na nje na kutembelea mashina. Alisisitiza kuwa litakuwa ni jambo la ajabu ikiwa yeye kama Katibu Mkuu wa Chama katika ziara zake anatembelea na kufungua mashina kisha viongozi wa Mkoa ama eneo husika hawatembelei mashina hayo wala kufuatilia maendeleo yake.Ndugu Kinana alitua Tabora Asubuhi hii akiwa njiani kutoka katika Mkoa wa Rukwa ambako alifanya Mkutano wa Hadhara na pia kufungua shina la Isesa wilayani Sumbawanga. Ndugu Kinana hivi punde ataendelea na Ziara yake, ambapo ataelekea Geita ambako atafanya Mkutano wa Hadhara na pia kufuatilia kero za wachimbaji wadogo pamoja na hali za waajiriwa katika migodi.View attachment 72124 View attachment 72125
Mkuu wa mkoa anaagizwa kwenda kufungua matawi ya ccm? Ccm isipotoka. Madarakani mtanzania ataendelea na mateso makali
 
Wana Tabora kuweni makini sana na Tembo kama wapo! Bora muweke ulinzi nyinyi wenyewe. Huyo Msomali ni hatari sana kwa uwepo wa tembo hapa nchini!
 
Kama tilivyosikia Mh ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu, pia tumesoma katika magazeti yetu kampuni ya katibu mkuu mteule kuhusishwa na kusafirisha meno ya tembo. Japo wapo walioridhika na utetezi wake kuwa hausiki, jambo ambalo nalipinga. Upo uwezekano hausiki direct, lakini indirect anahusika na kashfa hii.(Hakuwepo bandarini,lakini aliujua mzigo)
Katika mkoa anaotoka huyu Baba, miaka michache iliyopita, walitoroshwa wanyama hai. Is it coincidence? any way hausiki au kama baadhi yatu tulidai kusakamwa kwake ni kutokana na jina/mavazi yake kushabiana na dini fulani.(ain't going there)
Sasa nasikia Mzee anasafiri kila mkoa akiongozana na mpinga UFISADI aka VUVUZELA kuangalia uhai wa chami. Kwa maoni yangu, nadhani Jamaa anapita kuangalia ni mkoa gani atapata Tembo wengi kuendeleza biashara yake. Chama chake ni kivuli cha Majambazi, na wengi hutumia mwamvuli wake kujitajirisha binafsi.
Uwanja upo wazi jadili please
 
Back
Top Bottom