Kinana achota busara za Dk. Slaa

Kakke

JF-Expert Member
Dec 4, 2010
1,883
1,482
KINANA-MKUTANO-WA-SHIRIKISHO-LA-CCM-VYUO-VIKUU-MORO-PIX-NO-2-300x201.jpg

Kinana

Na Mwandishi wetu


KATIBU Mkuu mpya wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), amechota busara za Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, kwa kuitaka serikali iondoshe kodi kwenye vifaa vya ujenzi ili kutoa motisha kwa wananchi kujenga nyumba za bei nafuu.

Hoja ya kutaka vifaa vya ujenzi kama vile mabati, saruji na nondo vipunguzwe bei ili kuwawezesha wananchi kujenga nyumba bora iliasisiwa na Dk. Slaa na kuingizwa kwenye Ilani ya Uchaguzi ya CHADEMA na kutumika kumnadi Dk. Slaa kwenye mikutano ya kampeni za urais mwaka 2010.

Wakati Dk. Slaa akitumia kete hiyo kujinadi nchi nzima, alisema CHADEMA ikiingia madarakani itahakikisha bei ya saruji, mabati, nondo na vifaa vingine vya ujenzi vinapungua bei hadi kufikia sh 5,000, badala ya bei ya wakati ule, ambapo mfuko mmoja wa saruji ulikuwa unauzwa kwa sh 15,000.

Hadi sasa bei ya vifaa hivyo iko juu zaidi ikilinganishwa na mwaka 2010 na hali hiyo imeendelea kuwa kikwazo kwa watu wa kipato cha chini kuweza kujenga na kumiliki nyumba.

Wakati akiinadi sera hiyo iliyomo kwenye Ilani yao ya uchaguzi, Dk. Slaa alisema vifaa hivyo vya ujenzi vinaweza kuuzwa kwa bei poa na kuwawezesha wananchi kumiliki nyumba zao.

Alisema CHADEMA itakapoingia madarakani, itapunguza kodi na kutoa ruzuku ya mabilioni ya fedha kila mwezi kwa viwanda vinavyozalisha vifaa vya ujenzi wa nyumba ili ziuzwe kwa bei rahisi.

Hata hivyo hoja hiyo ilionekana kuwasumbua sana CCM kwa kumwita Dk. Slaa muongo na kisha kumwita Meneja wa Kiwanda cha Saruji cha Wazo Hill, kinachozalisha saruji ya Twinga Cement ili kutoa ufafanuzi.

Katika ufafanuzi wake, meneja huyo alisema ni vigumu kwa bei ya saruji kupungua kwa kiwango cha sh 5,000 anachotaka Dk. Slaa kutokana na ugumu wa upatikanaji wa malighafi.

Lakni akisoma maazimio ya Mkutano Mkuu wa Nane wa CCM taifa juzi mjini Dodoma, Kinana ambaye ndiye aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Maazimio, alisema CCM inatambua kwamba kila Mtanzania ana haki ya kuishi katika nyumba bora na iliyo na staha, hivyo mkutano mkuu unaiagiza serikali itoe kipaumbele katika suala la ujenzi wa nyumba, hasa nyumba za kupanga au kununua kwa bei rahisi.

"Mkutano Mkuu unaiagiza serikali katika kutekeleza Ilani ya uchaguzi kuhusu sekta hii, ichukue hatua zifuatazo; mosi, kutoa motisha kwa ujenzi wa nyumba bora na za bei nafuu kwa kuangalia uwezekano wa kuondoa kodi katika vifaa vya ujenzi wa nyumba kama vile saruji, mabati, nondo na vingine.

"Pili, kuondoa Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) katika nyumba za bei nafuu zinazojengwa na kuuzwa na mashirika ya kiserikali na ya sekta binafsi ili kuwawezesha wananchi wa kipato cha chini kumudu kuzinunua kwa njia ya mikopo," alisema Kinana.

Katika azimio hilo, Kinana na kamati yake walikwenda mbali zaidi kwa kutaka utaratibu wa kujenga au kununua nyumba urahisishwe kwa Benki Kuu kudhibiti riba na kuitaka serikali ianzishe taasisi itakayosimamia na kudhibiti kodi za pango la nyumba ambazo hivi sasa ni kubwa mno na zinatozwa kwa mwaka mzima, hivyo kuwatesa wapangaji hususan wa kipato cha chini.

Akizungumza na Tanzania Dima Jumapili kuhusu sera ya CHADEMA aliyokuwa akiinadi kuchukuliwa na CCM, Dk. Slaa alikumbusha jinsi ambavyo Rais Jakaya Kikwete na CCM walivyowaita waongo wakati CHADEMA walipokuja na sera ya matumaini kwa Watanzania mwaka 2010, wakisema nyumba za tembe na nyasi sasa basi na kueleza mikakati yao ya kushusha bei ya saruji na vifaa vya ujenzi.
"Nimefurahi juzi kusikia CCM katika maazimio ya Mkutano Mkuu wao wakisema watashusha bei ya saruji na vifaa vya ujenzi.

"Sasa CCM na CHADEMA nani waongo? Mimi nasema hakuna kitu kinachotushangaza katika uongozi wa sasa wa CCM," alisema Dk. Slaa.

Wakati sera nyingine ya CHADEMA mwaka 2010 ilitaka elimu ya msingi kutoka darasa la kwanza hadi kidato cha nne iwe bure na iwe haki ya msingi ya kila mtoto, CCM katika maazimio yake imeitaka serikali kutazama uwezekano wa kuifanya elimu ya sekondari kuwa ya wote ili fursa hiyo ipatikane kwa watoto wote na iwe ni haki ya msingi kwa kila mtoto nchini.

Baadhi ya maazimio mengine yaliyopitishwa na mkutano huo mkuu ni pamoja na suala la nidhamu na uwajibikaji ambapo wajumbe wameiagiza Halmashauri Kuu (NEC kuendelea na zoezi la kuwabaini na kuwaondoa viongozi na watendaji wa chama wanaokwenda kinyume cha maadili ya uongozi na wanaokipaka matope chama.

"Mkutano Mkuu pia unaiagiza serikali kuwachukulia hatua kali na za haraka viongozi na watendaji wa serikali ambao ni wala rushwa, wabadhirifu na wanaotumia vibaya madaraka yao," alisema Kinana wakati akisoma maazimio hayo.

Maazimio mengine ni pamoja na kuitaka serikali kupandisha kipato cha wafanyakazi kwa kuzingatia upandaji wa gharama za maisha na sekta binafsi pia isimamiwe kutekeleza azima hiyo ya CCM wakati kwa upande wa wakulima, chama hicho kimeitaka serikali iongeze kasi ya usambazaji nishati ya umeme vijijini na kusukuma ujenzi wa miundombinu vijijini ili kuwe na mazingira ya kuvutia uwekezaji.

Siri ya uteuzi wa Kinana yafichuka
Katika hatua nyingine, siri ya uteuzi wa Kinana kuwa Katibu Mkuu mpya wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), imejulikana.
Habari kutoka ndani ya chama hicho, zilisema kuwa siri ya uteuzi wa nguli huyo wa siasa za CCM, imetokana na juhudi za Rais Benjamin Mkapa kumshawishi kushika nafasi hiyo ili kukinusuru chama.

Awali ilielezwa kuwa Rais Jakaya Kikwete, ambaye ni Mwenyekiti wa CCM taifa, alijaribu bila mafanikio kumtaka Kinana awe katibu mkuu.

Hata hivyo ili kukubali majukumu hayo, Kinana aliweka masharti ambayo mwenyekiti alikubaliana nayo na kuahidi kuleta mabadiliko makubwa ndani ya CCM ambayo katika siku za hivi karibuni imepoteza mvuto.

sifa moja kubwa anayotajwa kuwa nayo Kinana ni msimamo mkali dhidi ya masuala ya ufisadi, na kubwa zaidi anatajwa kuwa bingwa wa mikakati ya kisiasa ndani ya chama hicho, jambo linalothibitishwa na kuteuliwa kwake kuongoza kampeni za wagombea urais katika mazingira ya ushindani mkali.

Itakumbukwa kuwa Kinana ndiye aliyeongoza kampeni za Benjamin Mkapa mwaka 1995, dhidi ya Augustine Mrema, aliyekuwa mwanasiasa maarufu na aliyekubalika kwa wakati huo.

Tangu wakati huo, Kinana amekuwa akiongoza kampeni za urais. Ni mtu anayetajwa kusimamia mawazo anayoamini ni sahihi, lakini akiwa tayari kuunga mkono hoja zenye lengo la kukijenga chama.

Nafasi ya Makamu Mwenyekiti imechuliwa na Philip Mangula akirithi mikoba ya Pius Msekwa, mwanasiasa mkongwe na mzoefu akiwa na rekodi ya kuwahi kuwa katibu mtendaji mkuu wa kwanza wa CCM.


 
Hujui sera ya magamba,kikitamkwa na mpinzani hata kama ni kizuri kinaonekana hakifai,lakini acha tu waige lakini wananchi wanaelewa kinachoendelea tz.
 
Political manoeuvre; i don't believe this for the ruling party but for oppositions will be possible.
 
CCM hapo ndipo wanaponishangaza sana, kitu chochote ambacho CDM ikisema hata kama kinatekeleza lakini kama kitakipa tu CDM sifa mbele ya jamii itaonekana ni uongo, uchonganishi dhidi ya wananchi na serikali yao!!!

Kama CCM ikiweza kufanya tu bei ya bati moja ikawa 10,000 na cement nayo 10,000 nadhani itachochea sana watu kujikwamua katika juhudi za ujenzi.
 
hawa ndio walikuwa wakitaka mpango mzima wa CDM kwa watanzania.Wapo wapi mkandara ,pasco, mzee mwanakijiji?
 
Sifa na heshima ziende kwa Dr.SLAA na CHADEMA kwa kuleta sera/ilani 2010 inayotekelezeka. Sasa jukumu la ccm ni kulamba matapishi yao kwa kutekeleza walichokibeza awali
 
Back
Top Bottom