Mango juice
JF-Expert Member
- Feb 25, 2019
- 345
- 465
Kwa kweli Dada zetu sijui Mnakwama wapi? kwamba hamna elimu ya uzazi, au mnakubali kudanganywa na kubebeshwa mimba ambazo mwisho wa siku mmakuja kutelekezwa na kusabisha watoto kukosa haki zao za msingi.
Sio ajabu leo kumkuta mtaani mdada ana watoto 3 alafu kila mtoto ana baba yake sasa mtu kama huyu kweli alijipanga kubeba mimba zote hizo au kazibeba kwa bahati mbaya? Je kwa Mwanamke kama huyu Kuna haja ya kuwalaumu Wanaume kuwa wanawakimbia na kuwatelekeza watoto wao.
Hapa mtaani Kuna kesi ya Vijana watatu walio zaliwa na Mama mmoja kila mtu ana baba yake sasa Mama yao huyo akaenda kuolewa na mwanaumee mwingine aliyekuwa anaishi nyumbani kwake na watoto zake 2 baada ya mkewe wa kwanza kufariki sasa Mama huyu kwa sababu alizalishwa watoto 3 akaenda kuishi nao kwa Mme wake wa Ndoa.
Kilichotokea sasa huyu Mama alifanikiwa kuzaa watoto 2 na Mme wake huyu watoto wake hao 2 wakajengewa nyumba yao
Kimbembe kimekuja kutokea baada ya huyu mwanamke pamoja na mumewe kufariki hawa watoto 3 wa huyu Mama ambao aliwazaa kabla ya kuolewa na kila mtoto ana baba yake wanadai Urithi wa Nyumba kwa Baba yao wa Kufikia Wakati mzee huyo alijenga nyumba 2 Moja kwa ajili ya watoto wake wa kwanza kwa mkewe wa kwanza aliyefariki na Nyumba ya pili kwa ajili ya watoto zake wawili aliyezaa na mkewe huyu wa pili
Sasa katika mtafaruku huu nani alaumiwe, na Je hao watoto 3 wa huyu Mama aliowapata kabla ya kuolewa wanahaki ya kumrithi Baba yao wa kufikia?