KINACHOWACHELEWESHA Muunganiko wa Vyama vikuu vya Upinzani vinavyounda ukawa, kutaja Mgombea wa Urais imebainika,Anaandika KAROLI VINSENT endelea nayo. Akizungumza na Mtandao huu, Afisa Habari wa Chadema Tumain Makene amesema sababu hiyo taarifa Majimbo mapya yaliotangazwa jana na Tume ya Taifa ya Uchaguzi nchini NEC. Watanzania wasiwe na wasi kinachowachelesha ni Viongozi wa Ukawa ni mgawanyo wa Majimbo mapya ya uchaguzi yalioatangazwa jana na tume ya uchaguzi ndio hayo yanayojadiliwa na kuchelewesha kumalizika kwa kikao Makene ameongeza kuwa , "kwa sasa Viongozi wa Ukawa wameingia kwenye mapumziko ikiwemo kupata Futali,ila baada ya Hapo Kikao hicho kitaendelea". Vilelevile Afisa Habari huyo amewataka wana chama wa Vyama vinavyounda Ukawa Ikiwemo Chadema,CUF,Nccr Mgaeuzi pamoja na NLD wazipuuze taarifa zinaonea mitandaooni kwamba umoja huo umemeguka na kusema kwa sasa kikao hicho kinaendlea vizuri. Mwandishi wa Mtandao huu aliokuwepo kwenye Hoteli moja hapa Jijini Dar es Salaam ambapo Vikao hivyo vya Ukawa vinafanyika alishuhudia Viongozi mbali mbali wa vyama vya Vitatu ambavyo ni NLD,Chadema pamoja na Nccr-Mageuzi, CUF wakipata Chai ya jioni huku wakioneka wapo pamoja. ENDELEA KUFUATILIA UTAPATA TAARIFA KAMILI MAANA TIMU NZIMA YA WAANDISHI WAKE WAPO KWENYE MKUTANO HUO UTAPATA TAARIFA KAMILI,
WWW.FULLHABARI.BLOG.COM