Kinachowaangusha CHADEMA ni kuhangaika na sentensi kwenye hotuba za Rais

Wakudadavuwa

JF-Expert Member
Feb 17, 2016
15,653
2,000
Kwa bahati nzuri Raisi Magufuli huongea mambo yalivyo na si vinginevyo.Hili ndilo mwiba au sindano anayowadunga wapinzani.Badala ya kutoa hoja wamejikita kwenye sentensi ambazo wananchi hawajali au hawazingatii.

Kama hawatajirekebisha ikifika 2020 hawatakuwa na cha kusema.Mathalan watu wameshupaa kusema hakuna mikopo bila kuwa na uhalisia...kwa waliobahatika kusoma elimu ya juu wanajua bila "boom" kwa wanafunzi wanaostahili migomo haiepukiki.

Mwanafunzi haambiwi kugoma na mitandao bali hugoma anapokosa mikopo na ukiona hamna mgomo ujue pesa zipo sasa utajiumiza kupiga kelele ili kujenga taswira yako utaishia kupasukwa nyongo kwa chuki dhidi ya serikali.

Miaka ya nyuma JK alikuwa mwepesi kutoa ahadi ya kujenga nyumba kwa waathirika wa majanga mfano Kilosa na Kahama haya yote hayakutekelezeka sababu ya ukosefu wa fedha na uhalisia wa majanga na watu walisikika wakimshutumu JK kuwa anaahidi kwa kutaka umaarufu lakini haiwezekani na waliosema hadharani ni wapinzani leo JPM kusema ukweli imeonekana si sawa,watu wale wale wanapinga waliyoyaamini.

Ni dhahiri kuwa kauli JPM ni msumari mzito kwenye kaburi la siasa za upinzani.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom