Pengine ni kweli.jogoo wa kijijini hawiki mjni.
Kugombea daladala kama huna ka-noah.Kuna mitaro imejaa takataka na maji machafu yanayonuka. Mazalio ya mbu!!
Mambo yanayonikera nikiwa jijini D'Salaam ni mengi, lakini yaliyozidi ni haya:
1.Kivutio maarufu kwa wageni na wenyeji- Foleni
2.Mgawo wa umeme usiokuwa na taarfa.
*Mengine sisemi................
Uchafu
Mji hauna mpangilio.
Foleni.
Umeme.
Maji.
Giza.
Mtandao slow/gharama.
Hili mkuu neno.Niongeze hakuna sidewalks/sehemu za kupita kwa miguu kwa ujumla, mjini sidewalk zimegeuka parking na kila mtu anajenga anavyotaka yeye ukitembea mara unapanda ngazi mara unashuka, mara unakwepa mashino/mabango/minyororo/maua yaani kama yale mazoezi ya jeshini!
Taja kinachoboa dar............dar inaboa sana
Hakika ni kero bin kero.Taja kinachoboa dar............
1. Madereva wa daladala...........
2. Matrafiki wala rushwa.............hasa pale keko karibu sollatek
3. Mapolisi wala rushwa uwanja wa taifa............
4. Mbreaki down yananiboa yavyochubua rangi za magari ya watu.............. Aaaaaaaaaaaaaaafffffffffuuuuuuuuuuuu kwa nini kituo cha kupaki breakdown ni polisi...????
Ni kweli mkuu.Ukiwa huijui dar lazima uiponde! Lakini mambo yote dar,foleni ndio kivutio cha utalii,
Nalo neno mkuu.Dar es salaam usiku bwana...foleni zimeisha mataaa yanawaka tuuu rangi tofauti....ukipaki tu wanakuja wakihabeshi, kihindi, kichina, kiarabu, kizungu, wakichaga, kipare, kihaya, wa tanga, wasanta domingo ...wote wa viwango....migahawa mizuri ya chakula...sehemu za vinywaji zilizotulia, networking ya hali ya juu, ma "deal" kibao (kama mjanja lakini), circulation ya hela ni kubwa, kazi zinazolipa zipo huku, biashara kubwa zipo huku, ukitaka kusoma kuna variety za institutions, unapata habari za nchi wa kwanza ( information is power) wenzetu zikisha expire ndio wanazidaka. Na mambo mengi ya kueleweka.....
Sisi tunajadili yanayokera dar hatudebate uzuri na ubaya wa dar.tunataka yanayokera tu!Nalo neno mkuu.
Asante kwa kunyoosha mstari.Sisi tunajadili yanayokera dar hatudebate uzuri na ubaya wa dar.tunataka yanayokera tu!
Ukiwa huijui dar lazima uiponde! Lakini mambo yote dar,foleni ndio kivutio cha utalii,