Synthesizer
Platinum Member
- Feb 15, 2010
- 12,265
- 21,443
Mtu akisema anataka kuondoka Tanzania na kuishi nje wengi wanadhani ni kwa sababu ya kutafuta maisha mazuri tu, yaani green pastures. Lakini ukweli ni kwamba si wote wanaochochewa na green pastures.
Mimi binafsi kwa mfano, nina maisha mazuri tu hapa nchini, na nina fedha ya kutosha kukubaliwa kuwa mkazi katika nchi za nje. Nimejitahidi sana kutokuwa upande wowote kisiasa ili nisibughudhike. Lakini lazima nikiri kwamba siku hizi karibu kila siku, kila ninaposoma magazeti au kusikiliza/kuangalia taarifa za habari, naona ni maudhi tu ya uonevu kwa wananchi, wanasiasa na waandishi wa habari, viongozi tunaowaamini kutamka na kufanya mambo ya ajabu na mara nyingine ya kitoto, Bunge letu kukosa hadhi kutokana na utendaji wa viongozi na wabunge wake, Polisi na mahakama kuonekana wazi wakifanya kazi zao kwa shinikizo za kisiasa na hivyo kuwanyima watu haki zao, kuminya uhuru wa vyombo vya habari, usumbufu barabarani nikisafiri na gari yangu, nk. Ni mambo yananifanya nione nchi yangu inakuwa kama banda la vurugu, total chaos.
Vitu kama foleni barabarani, umeme na maji visivyo na uhakika nk, wala havinipi shida, nachukulia ni changamoto za kuishi Afrika. Pesa ninayo ya kutosha, lakini sasa naona nakuwa kama mtumwa wa aina fulani katika nchi yangu mwenyewe, wa kuishi kulingana na matakwa binafsi ya wababe fulani wanaojiita viongozi ambao wanajifanya wana akili kutuzidi Watanzania wengine na wanajua kila kitu na wengine wote hatuna haki wala akili, pamoja na pesa au umasikini wetu.
Hivi ninakosea kuwa na mawazo kama haya?