Kinachomtesa Shibuda ni urais

Candid Scope

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
11,883
6,884
IMG_1259.JPG

Shibuda alitangaza kugombea urais katika kipindi cha kwanza cha miaka mtano ya utawala wa Kikwete. Alipoona hana nafasi ya kutia mguu aliendelea na mipasho pale bungeni kwa chama chake CCM kama anavyofanya sasa kwa Chadema. Katika kikao cha mwisho cha bunge kabla ya uchaguzi mwaka jana Shibuda alipokuwa amegeuza kauli na kuanza kumpongeza Kikwete, Speaker Samweli Sitta na viongozi waandamizi wa serikali kwa ajili ya kujisafisha atakaporudi kugombea ubunge awe amesafishika dhidi ya mabezo yake kwa viongozi na chama chake cha CCM hapo awali, Speaker Samweli Sitta alimwuliza Shibuda kama angali bado na nia ya kugombea urais pale pale ndani ya kikao cha bunge. Shibuda kama kawaida yake alitoa jibu la kishairi kama si kingonjera kwa kusema; "unapoutua mzigo toka kichwani hufikia mabegani kwanza" mwisho wa kumnukuru.

Kwa matarajio yake kujiunga Chadema na kujiona kama msemaji sana na mzoefu bungeni alitazamia angepata wadhifa mkubwa ndani ya Chama na hivyo kujenga ndoto zake za Urais. Kutokana na kutoweka kwa ndoto hizo ndio maana tunachoshuhudia sasa ni kwenda kinyume cha sera za chama chake, kuwabeza na kuwatukana wakubwa wake wa Chadema ngazi ya kitaifa. Kama mtakumbuka katika baadhi ya vikao vya bunge amewahi kuwarudi wabunge wa upinzani kwamba hawana uzoefu na wawaheshimu wazee.
 
Ujira wa mwiha...

Wengi wa wabunge wanachong'ang'ania ongezeko la posho ni kwa ajili ya pesa za kutoa rushwa wakati wa kampeni zitakapofika. Kampeni siku hizi zinaendeshwa kwa mfumo wa takrima na rushwa.
 
IMG_1259.JPG

Shibuda alitangaza kugombea urais katika kipindi cha kwanza cha miaka mtano ya utawala wa Kikwete. Alipoona hana nafasi ya kutia mguu aliendelea na mipasho pale bungeni kwa chama chake CCM kama anavyofanya sasa kwa Chadema. Katika kikao cha mwisho cha bunge kabla ya uchaguzi mwaka jana Shibuda alipokuwa amegeuza kauli na kuanza kumpongeza Kikwete, Speaker Samweli Sitta na viongozi waandamizi wa serikali kwa ajili ya kujisafisha atakaporudi kugombea ubunge awe amesafishika dhidi ya mabezo yake kwa viongozi na chama chake cha CCM hapo awali, Speaker Samweli Sitta alimwuliza Shibuda kama angali bado na nia ya kugombea urais pale pale ndani ya kikao cha bunge. Shibuda kama kawaida yake alitoa jibu la kishairi kama si kingonjera kwa kusema; "unapoutua mzigo toka kichwani hufikia mabegani kwanza" mwisho wa kumnukuru.

Kwa matarajio yake kujiunga Chadema na kujiona kama msemaji sana na mzoefu bungeni alitazamia angepata wadhifa mkubwa ndani ya Chama na hivyo kujenga ndoto zake za Urais. Kutokana na kutoweka kwa ndoto hizo ndio maana tunachoshuhudia sasa ni kwenda kinyume cha sera za chama chake, kuwabeza na kuwatukana wakubwa wake wa Chadema ngazi ya kitaifa. Kama mtakumbuka katika baadhi ya vikao vya bunge amewahi kuwarudi wabunge wa upinzani kwamba hawana uzoefu na wawaheshimu wazee.

Huyu nae ni janga ndani ya cdm
 
Kwa hali hii vihoja na vimbwanga ndani ya Tz hii havitoisha kamwe
 
Mzee wa mjengoni akisaini yale makaratasi ya cameron na obama ,walahi mimi naanza na mzee wa ujira wa mwiha.............
 
ni mara mia kupoteza jimbo majimbo hata matano kuliko kua na takataka kama shibuda,kirusi kinacho isumbua chadema.inatakiwa asijua mipango na mikakati ndani ya chama abaki kama condom iliyo tumika
 
Kwa miropoko ya hivi karibuni, CDM wamfukuze ili apoteze na ubunge. La sivyo wasimteue kugombea ubunge ifikapo 2015.
 
Mwenye cv ya shibuda tafadhari aweke hapa jamvini halafu nitawaeleza kitu fulani.
 
Huyu nae ni janga ndani ya cdm

Nashangaa mpaka sasa Chadema hawajamkata shingo, nadhani wanamlia timing sidhani kama atakujagombea kwa tiketi yao tena; itabidi ale mataishi yake arudi CCM!!
 
Habith huyo apewe uraisi na nani? Hizo ni ndoto za mchana kama shoga kudai kapata ujauzito.

Chama
Gongo la Mboto DSM.
 
Natoa rai kwa viongozi wa chama changu cha CHADEMA heri wamtimue Shibuda, akatange tange aende DP, CHAUSTA, TADEA au hata NRA vyama vipo vingi then tupambane nae, najua makamanda mnajiamini na huyu hasitusumbue nimetokea kumchukia Shibuda sababu ya kauli zake za hovyo hambazo zinakera kwa wanachama wengi sio peke yangu Shibuda aondoke aliingia kupitia njia moja aondoke kwa njia saba, bora madiwani wa Arusha kuliko shibuda
 
Back
Top Bottom