Kinachojiri Arumeru sasa hivi

Leo wapo kata gani? Hebu uliza utuambie.
 

1. Kuhusu madawati mkuu ni sera ya elimu na ni nchi nzima wanafanya hivyo sasa akipata ubunge sijui atabadilishaje maana sera zinazotekelezwa ni za CCM.


2. Hapo kwa MDEE sijaelewa vizuri, kwani kijana NASSARI anapumzika kwa MDEE au ndiyo anataka kuanza.
 
Ni kweli ufafanuzi ni muhimu hapo kuhusu kamanda Halima. Ndo kusema anaweza kuwa mumewe?
 

hio ya madawati umetumia fomula gani maanake haiingi akilini kwani shule ikianza mwaka wa kwanza mpaka wa nne tayari madawati yamejaa madarasani ....kwahio kuanzia mwaka wa tano hizo dawati zinaenda wapi? wakati majengo hayajaongezeka?

 
serikali ni mkataba baina ya watawala na watawaliwa, endapo mtawala/mtawaliwa hataridhishwa na mwenendo wa mwenzie katika kufurnish mkataba husika, upande utakaodhibitisha kukiukwa kwa terms za mkataba husika anaweza kuvunja mkataba huo.
Huu ni wakati wa Arumeru east kuvunja mkataba walioingia na walaghai CCM.
Ukichagua CCM umechagua maisha magumu daima.
 

CDM kuna tatizo gani linapofika suala la ndoa. Kwani aliulizwa kuhusu ndoa?

Niliwahi kusoma mahala Mdee akisema anataka mtu ambaye si msomi!
 
Mtoto huyu vp mtoto siyo rizki hashughulikii hata apewe nini ,,, wimbo mzuri sana huu uliimbwa na SUGU!
 
hayo mambo ya ndoa yanatoka wapi tena kwani ukioa utendaji wako unakuwa na tofauti na wasio oa?
 
Hii issue ya madawati arumeru ni sugu sasa! Since time immemorial wanafunzi wanachangishwa madawati kila mwaka! Hayajai yakafurika jamani? Waanze kuchangia na vitabu basi!
Issue ya Nassari na Halima is misplaced! Nimekumbuka Mh Sita akiwa speaker alimtambulishaga ShyRose Bhanji kuwa she is engaged wanasubiria harusi and never happened. Issues personal hazitusaidii, kama arumeru na maji yote yanayoitiririka wananchi hawana maji labda mbunge bachelor ndo anafaa manake akikosa maji na hana mke kitaeleweka tu!
 
1. Kuhusu madawati mkuu ni sera ya elimu na ni nchi nzima wanafanya hivyo sasa akipata ubunge sijui atabadilishaje maana sera zinazotekelezwa ni za CCM.

mkuu mbona unapingana na waziri wako wa tamisemi?
 
Inapendeza kwa kweli lakini kubwa zaidi ni kuhakikisha April mosi tuna-capitalize haya yanayofanyika sasa. Big up CDM
 

Je walikumbuka kutoa shule kwa wananchi juu ya nguvu waliyonao? Kwani wananchi wengi hawajui nguvu waliyonayo, na siku wakijua wanasiasa uchwara wataipata

View attachment 49604
 
ndugu yangu naomba chukua muda kunielewa,mwanafunzi anapoenda kuanza form one anatakiwa aende na dawati,kaaukijua kua hiyoshule sio mpya,kwamba labda kunamadarasa hayana madawati,wanaomaliza form four wanakua wameacha madawati sasa labda uniambie kama kuna baadhi yatakua yameharibika hapo sawa alakini suala la kila mwanafunzi kila mwaka kuja na dawati sio rahihi ng wizi huo.kuhusu mdee amehoji kama kupata mke ni shida kihivyo kama magamba wanavyofikiri basi anaweza kwenda hata kwa mdee akapata mke alafu mumpe huo ubvnge.,inahitaji kufikiri zaidi kuielewa hile kauli
 
1. Kuhusu madawati mkuu ni sera ya elimu na ni nchi nzima wanafanya hivyo sasa akipata ubunge sijui atabadilishaje maana sera zinazotekelezwa ni za CCM.

Kyela hatupeleki madawati tunapoandikisha watoto wetu shule;amri hii iliondolewa mwaka 2005 baada ya Mwakipesile wa CCM kushinda ubunge kwa tofauti ya kura chini ya 100 dhidi ya hayati Mwakasumi wa TLP!

RIP Mwakasumi alikuwa anaielezea hii kwenye kampeni zake na wana Kyela wakamuelewa na CCM kuhofia kupoteza jimbo kwenye uchaguzi wa 2010 wakafuta michango yote kwenye elimu!

Mkiwa na upinzani imara CCM huwa inafuta michango ya hovyohovyo lkn wakijua Jimbo ni lao huwa wananyanyapaa mno wapiga kura!

NB>RIP Mwakasumi akajiondoa TLP na kujiunga CCM na alifariki mwaka 2010 akiwa MWENYEKITI WA CCM WILAYA YA KYELA!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…