Kinachofuata: Daudi Albert Bashite lazima ang'oke, muda wa usafi umefika!

Kinachofuata: Daudi Albert Bashite lazima ang'oke, muda wa usafi umefika!

Lazima ang'oke sasa. Uwepo wake si salama kwa Raia. Lazima tujiulize anapata wapi kiburi hadi cha kuvamia vyombo vya habari?
 
Hongereni kwa kazi kubwa mliyofanya huko arusha, vikwazo vilikuwa vingi tangu kuanza kwa mchakato huu.....hatimaye kwa Rehema za Mungu mumefanikisha........Nina hakika na hili la kumtoa Bashite litafanikiwa, nawatakia kila LA kheri.
 
Kwanza namshukuru Mungu kwa kuimaliza kazi ngumu,kubwa na muhimu ya kumchagua Tundu Lissu kuwa Rais wetu wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika-TLS.

Nawapongeza Mawakili wote walioshiriki kuchagua wanaowaamini. Nawapongeza watanzania walio wengi kwa kutuunga mkono Mawakili tangu mwanzo hadi leo. Mmetupa nguvu ya kuwapuuza watishaji na kuwaonesha kuwa MAWAKILI SI WATU WA MCHEZOMCHEZO!

Baada ya mambo ya Arusha,tunaelekeza nguvu zetu Dar es Salaam kumng'oa Daudi Albert Bashite anayejiita Paul Makonda. Mapambano yatakuwa ya kimyakimya na ya wazi itakapobidi. Kama hataonesha cheti chake cha kidato cha nne,Bashite ataondoka tena kwa aibu

Iwe sirini au hadharani;iwe mteule wake anapenda au analinda, Bashite atatoka. Kwa mkakati huo jinsi ulivyosukwa,Rais atasikia,kujua na kuamua kumuondoa. Muda wa kufanya usafi umefika!

Mwafaaaa!

Mzee Tupatupa wa Lumumba(kwasasa Arusha)
Akiondoka pekee haitoshi, inabidi sheria ifuate mkondo wake!
Apigwe miaka kadhaa ya kunyea ndoo...
 
Kile cheti feki ni hiki hapa hadharani.

IMG-20170318-WA0024.jpg
 
Back
Top Bottom