Joshua justine
JF-Expert Member
- Sep 1, 2021
- 793
- 1,007
Sio kweli kwamba spika aliropoka kwa namna ile , mtu kama spika , anaecheza na sheria siku zote, anaecheza na hoja siku zote, sio mtu wa kumdhania kuongea hovyo bila kujua anafanya nn na madhara yake yatakuwa nn.
UKWELI
Tangu aondoke mwendazake Serikali na CCM kote kulipasuka, moto ulikuwa unawaka ndani kwa ndani bila ss wananchi kujua kinachoendelea humo.
Kilichowakera zaidi kina ndugai na wenzake kina Kassim ni ujio wa Mzee wa Mizoga kuwaongoza tena kwa remote control yake. Kulianza kufanyika reshuffling ya sera za nje, diplomasia, maswala ya corona, kauli dhidi ya ukusanyaki wa kodi n.k kwa ufupi mama ni kama alifanya kwa fujo mabadiriko mengi sana huku akiongozwa na mzee wa mizoga na mabeberu jambo ambalo wanaume wa mwendazake walifikia hatua ikawashinda kuelewana na hayo , walikuwa wanaongea ndani kwa ndani , kwa ufupi hili sio jipya , ni jipya kwetu wananchi tu.
Ilipofikia hatua sasa kuwa kwa kweli haiwezekani kufanya kazi tena pamoja, wakawa wamekubaliana ndani kwao huko kwamba sasa haiwezekani, na wakakubaliana hivyo.
Kutoka nje sasa kwa wananchi huwezi kuwaambia ukweli wote huo maana tayari huyo mama yenu hakuna atakayemuelewa , wote tutaside na wakina ndugai, so ikatengenezwa stage ya kuchezea hiyo drama ili lionekane kama ni tukio moja tu lililosababisha yote hayo, lakini sio kweli, hiyo ni danganya toto.
Angalia kila mtu anavyoshangaa inakuwaje spika aropoke vile, sasa kama watu wasiojua lolote hawawezi kufanya blunder kama hiyo , je spika mwenyewe?
Mziki mzima umeandaliwa ili kuwaondoa wote wanaompinga mama yenu serikalini huko ndani kwa ndani wanakopingana wao kwa wao wakikaa kama cabinets, ndio mama yenu sasa anaitumia hiyo kuunda baraza lake jipya, wakina katelephone wote hawaelewi uendeshani wa serikali wa mama yenu, na imefikia hatua hawawezi kwenda pamoja tena.
WANANCHI BILA KATIBA
Bila katiba wananchi tunadharauliwa na kutupwa huku na huku kwa drama za kisiasa za wanasiasa, uongo mwingi na sisi tunashangilia na kushabikia uongo mtupu, ukweli unabaki nyuma ya pazia.
Ili kuondoa aibu hii ya kudanganywa danganywa kama watoto , wananchi tuwe watu wazima sasa, tuamue kupata katiba iliyoboreshwa kwa kuondolewa mapungufu yote yanayoleta upuuzi kama huu. Katiba mpya ndio utu uzima wa taifa hili, huu ni utoto.
NB: Hii video nimeikuta baada ya mimi kupost
NIMEWEKA VIDEO HAPA , WACHAMBUZI WA SIASA ZA TANZANIA WAKUBWA WAKIONGEA KAMA HIKI NILICHOSEMA MM HAPA, NAONA MODES NAO WAMEANZA KUINGILIA BUNGE HUMU.