Kwa haraka haraka ni kwamba serikali imefilisika. Serikali ikifilisika inamaana haiwezi kulipa wafanyakazi, kuhudumia shughuli zote za serikali.
Ndo ugiriki wamefikia hali hiyo, wamekopa hadi wamefikia hatua ya kutokopesheka kabisa, na bado hawana hela hata ya kulipa hayo madeni.
Inabidi umoja wa ulaya wawape mkono kwasababu wapo ndani ya umoja huo. Hizo deadlines unazoona wamewekeana ni kwamba wamepiga mahesabu baada ya kupita huo muda serikali haina pesa kabisa. Wafanyakazi hawatakuwa na mshahara, shughuli zote za serikali zitasimama zote.