Kinachoendelea Uchaguzi Mkuu nchini Ghana

mbwewe

JF-Expert Member
Joined
Sep 10, 2014
Posts
3,267
Reaction score
3,415
Ikiwa imebaki siku moja kabla ya uchaguzi mkuu nchini kufanyika.

Tunataarifiwa mpaka sasa hakuna hta mtu mmoja aliyepoteza maisha, hakuna mgombea aliyeenguliwa na tume, hakuna vurugu zozote zilizotokea mpaka polisi walazimike kupiga mabomu ya machozi.

Wagombea wote wanapiga kampeni kwa uhuru kabisa hakuna aliyesumbuliwa na vyombo vya usalama kwa namna yoyote ile

Kwa hakika nchi zingine za Afrika tunakiwa kujifunza kutoka Ghana.
 
Nasikia katiba ya Ghana,ndiyo katiba Bora kuliko zote Afrika.
 
Ghana wapinzani ni wastaarabu hawana mihemuko kama Chadema!
Siyo kweli , Ghana wana katiba nzuri ya wananchi na tume huru ya uchaguzi. Shukuruni zimuendee marehemu Rais Jerry Rowling's.

Hapa kwetu kuna kundi halitaki tume huru wala katiba ya wananchi
 
wapinzani wa tz mjifunze kutoka hapa ghana kwa kina mh mahama vurugu hazina tija yoyote katika taifa
 
JJ Hayati Baba wa democrasia ya Ghana ukiacha Kwame Nkuruma. Alisema wakati wa Uhai wake wanataka wawe na Sheria ambazo hata Shetani akiwa Rais pale system itamtoa kabla hajafanya ushetani wake. Leo Tz katiba inaguswa guswa wote kimya.
Katiba inayotumika ni ya ccm
 
Umekuwa jumla jumla sana.

Je , ni nini kinasababisha yote haya,
Hakuna mtu aliyeenguliwa
Hakuna aliyeuawa ( kuua sio sifa)
Hakuna aliyetukana mgombea mwenzio
Hakuna aliyekashfu mwenzie
Wagombea wote wamesaini fomu ya amani
Wagombea wanaheshimiana
Wagombea wananadi sera
Wagombe wanaheshimu tume
Wananchi wana uelewa

Kuna mengi sana ya kujifunza toka Ghana kuanzia kwa viongozi wagombea wa vyama hadi wananchi.

Sio suala la kukurupuka tu na kusema hakuna aliyeuawa wala kuenguliwa ukadhani ni wajibu wa tume pekee kutimiza agenda hizo. Hili suala limaanza na wagombea, wananchi na viongozi wa serikali inayotawala.

Tujifunze
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…