Uchaguzi 2020 Kinachoendelea kwenye kampeni za CHADEMA ni kueneza chuki dhidi ya Magufuli na sio kunadi Sera na Ilani ya chama chao

Chagu wa Malunde

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
8,708
5,711
Wananchi wengi walitegemea kuwa kampeni zikianza tushudie na kusikia kuwa watatutalia vipi kero zetu.

Mfano tulitarajia kusikia kuwa pamoja na haya mambo makubwa yanayotekelezwa na Ccm na serikali yake wao wangeweza kufanya mazuri zaidi ya hiki kinachofanywa.Mfano tulitegea tusikie kuwa sekta ya afya, elimu na miundo mbinu imeimarishwa na Ccm. Je wao wapinzani watafanya nini zaidi kuperfom zaidi ya kinachofanywa na Ccm sasa hivi?

Hii inadhihirisha wazi kuwa hawa wapinzani hawapo tayari kuchukua dola kama watawala na hawana uwezo wa kutawala bali wamezunguka kueneza chuki na vinyongo walivyonavyo mioyoni mwao. Na hili linatupa mashaka huenda wakiwa na nafasi ya kutawala hawatatekeleza kama Ccm inavyofanya na hata kama wakipata nafasi watatuibia mali zetu za umma na kunedeleza ufisadi.

Nimemsikiliza mgombea wa Chadema akiwa Mwanza anaongea kwa jazba na chuki akiwaaminisha wananchi kuwa rais Magufuli ndio alitoa amri ya yeye kupigwa risasi. Na hii ni kwa sababu alikuwa akipinga jitahada za JPM kulinda rasilimali za watanzania. Na ameyasema haya baad ya kumsikia rais na ambaye ni mkuu wa nchi kuwa anampenda na asipoteze muda kufanya kampeni,bali atulie na atapewa kikazi kidogo cha kufanya. Mimi binafsi najua JPM ni mtu wa utani na huenda alikuwa anamtania tu huyu mgombea wa Chadema.

Lakini mgombea wa Chadema wa urais ameongea maneno makali sana akionyesha dhahiri kuwa ana chuki na JPM na amethibitisha kwa wananchi kuwa JPM alitoa amri ya yeye kupigwa risasi. Hii sio picha nzuri na wala sio sula linalofaa. Mgombea wa Chadema kama anauhakika kuwa JPM alitoa amri ili ashambuliwe anatakiwa afuate taratibu za kisheria na kwa sababu yeye ni mwanasheria anafahamu fika Mahakama kuu inayo mamlaka ya kulazimisha vyombo husika vikalishughulikia suala lake.Lakini pale wananchi wanapojazana ili wasikie utawasaidia vipi kutatua kero zao alafu unabaki kueneza chuki hii haisadii chama chake wala yeye mwenyewe.

Badala yake watu watachoka hizi hadithi zake za kupigwa risasi na October ikifika wataambulia mbunge mmoja tu.
 
Si amejenga fly over, ameleta ajira million 6, ameboresha maslahi ya watumishi, ameleta umeme kila kona, amejenga hospital za kutosha sasa ni Mtanzania gani ataweza kueneza chuki dhidi ya mtu huyu ambaye watumishi wa umma, wakulima na wafanyabiashara wanampenda sana?
 
Me nafikiri washauri wake hawako vizuri au hautaki urais?? Kapewa hiyo nafasi ili amrushie maneno mwenzie???

Kwa stail hii no kazi sana nafikiri Chadema ijikite zaidi kwenye kueneza Sera na sio kushambulia na mikoa hii ndo muhimu sanaaaa jamaa likienda huko linamwaga sumu wanasahau yote ya nyuma
 
Si amejenga fly over, ameleta ajira million 6, ameboresha maslahi ya watumishi, ameleta umeme kila kona, amejenga hospital za kutosha sasa ni Mtanzania gani ataweza kueneza chuki dhidi ya mtu huyu ambaye watumishi wa umma, wakulima na wafanyabiashara wanampenda sana ?
October mnaweza kutoka na mbunge mmoja tu.
 
Hakika mkuu.
tapatalk_1577354951190.jpg
 
Mwaka wake wa kwanza tu magufuli alikua ameshaiharibu nchi na kuchukiwa na watz wote......🤔🤔
Ajibu maswali ya Rais Tundu Lissu hatutaki blabla.....😒😒

Kwani Hajaanza kula mahindi 🤣🤣
 
Back
Top Bottom