Kinachoendelea kati ya Russia na Ukraine ndo kitazaa World War III (WW3)

Fanfa

JF-Expert Member
Sep 25, 2009
1,815
2,862
Tangu Putin atangaze Special Military operational yake Feb 2022 dhidi ya Ukraine, wengi waliamini kuwa huo ndo ulikuwa mwanzo wa vita kuu ya tatu (World War III) hasa Marekani na NATO walipoweka wazi kuwa wataisaidia silaha Ukraine ili iweze kujilinda dhidi ya mvamizi (Russia).

Marekani alipozishawishi nchi za EU kuisaidia Ukraine, fikra za WW3 ndo zilikolea kwa watu wengi (Pro-Russia na Pro-Ukraine).

Kinachoendelea sote tunaofuatilia vita hiyo tumekiona na tunajua, sina sababu ya kueleza.

Waliokuwa wakiamini kuwa hiyo vita ni mwanzo wa WW3 walikuwa na sababu muhimu zifuatazo;

1. Waliamini kuwa Russia ni super power na kwamba ina uwezo wa kupiga nchi zote ikiwemo marekani.

2. Waliamini vita ya Russia na Marekani itakuwa vita ngumu sana na wengine wakaenda mbali zaidi kwa kusema kuwa Marekani akiingilia ugomvi wa Russia na Ukraine ndo utakuwa mwanzo wa Marekani kupigwa na kusambaratishwa na super power aitwaye Russia.

3. Pro Russia na hata viongozi wa Russia waliamini kuwa Russia ina uwezo wa kumpiga Marekani kwa makombora yake anayoyaitwa Intercontinental Ballistic missiles, Hypersonic missiles na Nuclear missiles. Eti Kwamba Russia makombora yake ni hatari sana na ya technology ya hali ya juu sana.

4. Sababu nyingine ni kwamba waliamini kuwa Russia ana air defense systems hatari sana wakiwa wanarejea S-300 na S-400 series. Kwamba anga la Urusi linalindwa sana huwezi kupenya na kwamba marekani hana air defense systems kama za Russia.

Katika kutafakari na kufanya assessment kuhusu hali halisi ya kinachoendela katika vita ya Ukraine na Russia. Tunahitaji kujua kama kweli watu walichokuwa wanafikilia kimekuwa kweli au kimeenda kinyume chake kwa kujiuliza maswali yafuatayo.

1. Je, bado tunaamini kuwa vita ya Ukraine na Russia itazaa vita kuu ya tatu ya Dunia (World War III) ?

2. Ni kweli Russia ni supper power kama watu walivyoamini kabla ya vita kuanza ?

3. Ni kweli Russia ana uwezo wa Kuipiga Marekani na nchi zingine Duniani na pengine kuitawala Dunia.

4. Ni kweli Russia and air defense systems za hatari kuliko marekani na nchi yoyote duniani na kwamba anga lake liko salama hakuna kitu cha kupenya kwenye anga lake?

5. Ni kweli Russia ana silaha nzito za kutisha na zenye kutumia technology kubwa kuliko marekani na nchi zingine?

6. Ni kweli jeshi la Russia liko imara sana kama ambavyo tuliamini mwanzo na kwamba wana mafunzo imara ya kutumia silaha za kivita?

Tupate maoni na tafakari yenu bila matusi na ushabiki usio na hoja yenye mantiki. Tusitawaliwe na u pro-Russia au Ukraine tukajikuta tumetoka kwenye hoja.
 
..makombora yanayorushwa na Russia yatakayosababisha ajali ktk mitambo ya umeme wa nyuklia iliyoko Ukraine.

..kwa hali inavyoendelea nadhani ni suala la muda tu kutakuwa na ajali mbaya ya kihistoria Ukraine na ajali hiyo itapelekea vita kusimama / kusitishwa / kuisha.
Ikitokea hivo Russia atawezaje kutawala maeneo aliyoyachua Zaporizhzhia, Kherson, Luhansk, Donetsk na Crimea màana mikoa yote hiyo inategemea kupata umeme kutoka ZNPP. Una maana ataua Raia wake walioko maeneo hayo na kuondoka zake.

Kwa nini usifikirie kwa upande mwingine kuwa watatumia nukes kuiangamiza Russia kama kulipa kisasi. Kumbuka ZNPP marekani imewekeza na wanatumia technology ya mmarekani.
 
..sidhani kama Ukraine ana capabilities za kushambulia ndani ya Russia.

..pia wafadhili wa Ukraine hawajaonyesha nia ya kumpatia makombora yenye masafa ya kushambulia ndani ya Russia.

..So far, Russia amechakaza Ukraine nzima. Na tunaelewa ndani ya Ukraine kuna vinu ya Nyuklia.

..Je, kwa muda gani vinu hivyo vitakuwa salama?

..Je, hakuna hatari kwa vinu vya Nyuklia vya Ukraine kudondokewa na makombora ya Russia kwa bahati mbaya, au kwa kudhamiria?
 
Uko low sana kwenye huu mzozo,kwa taarifa yako Russia anapigana na ulaya nzima+Amerika ni zaidi ya nchi 40,

Ukraine ni uwanja wa mapambano tu, nothing else
Tuondoe kwanza personalities (personal attack) na jazba.

Hebu tusaidie kujibu dodoso la maswali tuliyouliza kwa kuwa umesema unauelewa vizuri sana huu mzozo na pengine hatima yake. Ukijibu kwa mtiririko wa maswali itapendeza kutoa uelewa zaidi.
 
Uko low sana kwenye huu mzozo,kwa taarifa yako Russia anapigana na ulaya nzima+Amerika ni zaidi ya nchi 40,

Ukraine ni uwanja wa mapambano tu, nothing else
Tuondoe kwanza personalities (personal attack).

Hebu tusaidie kujibu dodoso la maswali tuliyouliza kwa kuwa umesema unauelewa vizuri sana huu mzozo na pengine hatima yake. Ukijibu kwa mtiririko wa maswali itapendeza kutoa uelewa zaid
 
..sidhani kama Ukraine ana capabilities za kushambulia ndani ya Russia.

..pia wafadhili wa Ukraine hawajaonyesha nia ya kumpatia makombora yenye masafa ya kushambulia ndani ya Russia.

..So far, Russia amechakaza Ukraine nzima. Na tunaelewa ndani ya Ukraine kuna vinu ya Nyuklia.

..Je, kwa muda gani vinu hivyo vitakuwa salama?

..Je, hakuna hatari kwa vinu vya Nyuklia vya Ukraine kudondokewa na makombora ya Russia kwa bahati mbaya, au kwa kudhamiria?
Ngoja kwanza tuwekane sawa ili tujikite kwenye hoja.
Hoja iliyoko mezani siyo uwezo(capability) ya Ukaine kuipiga Russia.

Tunaomba hoja zako zijielekeze kwenye dodoso la maswali ili tuende sawa na mada iliyopo mezani.
 
..makombora yanayorushwa na Russia yatakayosababisha ajali ktk mitambo ya umeme wa nyuklia iliyoko Ukraine.

..kwa hali inavyoendelea nadhani ni suala la muda tu kutakuwa na ajali mbaya ya kihistoria Ukraine na ajali hiyo itapelekea vita kusimama / kusitishwa / kuisha.
Kwanza kinu kikubwa cha nuclear kipo chini ya warusi Kwa hiyo hawawezi kushambulia sehemu ambayo IPO Chini yake labda Ukraine washambulie hicho kinu.
 
..sidhani kama Ukraine ana capabilities za kushambulia ndani ya Russia.

..pia wafadhili wa Ukraine hawajaonyesha nia ya kumpatia makombora yenye masafa ya kushambulia ndani ya Russia.

..So far, Russia amechakaza Ukraine nzima. Na tunaelewa ndani ya Ukraine kuna vinu ya Nyuklia.

..Je, kwa muda gani vinu hivyo vitakuwa salama?

..Je, hakuna hatari kwa vinu vya Nyuklia vya Ukraine kudondokewa na makombora ya Russia kwa bahati mbaya, au kwa kudhamiria?
Rasmi leo UK imethibitisha kuipa Ukraine makombola ya Storm Shadow ambayo ni ya masafa marefu.
 
It's WW only if its Germany against the world !

Russia hawajafika level hizo, Ukraine tu inamtoa jasho. If anything its the end of Putin and Putinism in Russia.
Analysts wa masuala ya kivita, wanasema uwezo wa kivita wa Urusi ulikuwa exagerated.

Russia alipoivamia Ukraine, hakuma nchi iliyojitokeza kuisaidia Ukraine aina yoyote ya silaha kutokana na hofu ya mataifa mbalimbali juu ya uwezo mkubwa wa kivita wa Russia. Na hakuma nchi hata moja iliyoamininkuwa Ukraine ingetoa upinzani wa kivita kwa Russia.

Ni mpaka pale Ukraine ilipoweza kuizuia Russia kufanikisha mipango yake na kusababisha vifo vingi vya askari wa Urusi, ndipo mataifa mengine wakaona, kumbe inawezekana Ukraine kutoa upinzani kwa Russia. Mataifa mengi yakaanza kutoa misaada mbalimbali ya silaha za kivita kuisaidia Ukraine.

Ukweli vita hii imeianika wazi sana Urusi, na kuonekana kuwa kumbe nguvu ilizokuwa inafikiriwa Urusi inazo, haina kwa kiwango hicho.

Mataifa ya Magharibi yanazidi kuipa silaha Ukraine ili kuilazimisha Urusi kumaliza stock yake ya silaha. Sasa Urusi imelazimika kutumia mpaka silaha zilizotumika wakati wa vita ya pili ya Dunia.

Kwa upande mwingine, uchumi wa Urusi ambao ulikuwa tayari unalegalega, ambao ulifikia hatua mpaka kusaidiwa na mataifa ya Magharibi, sasa lazima utatikisika sana. Mataifa ya Ulaya yanatoa ziada kuisaidia Ukraine, Russia analazimika kutumia kile anachokihitaji sana kwa maendeleo ya wananchi wake. Vijana wasomi na wataalam wa Urusi wanakimbilia nchi za Magharibi kuogopa athari za kiuchumi na kulazimishwa kwenda mstari wa mbele kupigana vita. Haya yote, baada ya muda yatauumiza sana uchumi wa Russia.

Russia kwa sasa nguvu pekee iliyobakia nayo ni makombora ya nuklia, lakini kwa silaha nyingine na uwezo wa kupigana, haina tofauti na mataifa mengi ya Ulaya. Siyo tishio tena kwa nchi yoyote kwenye masuala ya uwezo wa kivita.
 
Weka statistics tukuamini kuwa urusi kaishiwa silaha kama huna nyamaza Tu Kwa Sababu utakuwa huna tofauti na mbwatukaji.
 
Russia dhaifu, russia Superpower wa Mchongo yet kaenda kumega eneo la Nchi Nyingine karibia 20%.
Hii nchi iliyomegewa eneo lake kwa sasa inaishi kwa Misaada ya Wanamagharibi yenyewe uwezo wake ulikwisha zamani.

If marekani anaweza peleka misaada worth billions of dollars unadhani unashindwa peleka wanajeshi maelfu kadhaa.

Ni mjinga tu anayeweza amini wale mercenaries ni watu wa kawaida na sio wanajeshi official wa marekani na washirika wake.
 
Back
Top Bottom