Kina nani wanaweza kumdanganya Rais wetu?

chakii

JF-Expert Member
Sep 15, 2013
20,385
24,939
Habari ya siku ya leo, Jumapili murua kabisa wakuu kwa upande wa kwangu.

Naomba niruke kwenye mjadala moja kwa moja bila kupoteza wakati.

Ni hivi.

Kina nani wanaweza kumdanganya Rais wakati linapokuja suala la maslahi ya Taifa? Hii jeuri ya mtu kumdanganya Rais wetu inaweza kutoka wapi, ni nani wanapaswa kuhakikisha Rais wetu hadanganywi?

kwani mimi naamini Rais akishadanganywa basi hata wananchi wote tumeingizwa chaka.

Tumsaidie Rais asidanganywe kwa maslahi mapana na Nchi yetu!
 
Bashite Daud kamdanganya kuwa Gwajma amemsingizia ana vyeti feki kaamua kula Limbwata lake kakubali uongo wake mpaka leo bado ni mkuu wa mkoa wa Dsm, anadanganyika sana Bashite anamdanganya sana, hata kwenye ununuzi wa ndege cash alidanganywa na akina Bashite na Dalali wa ununuzi wa ndege GSM akakurupuka na kununua ndege kwa cash ili wapate 10% yao kwa cash pia.
 
Tuache kuangalia issues kwa jicho la kisiasa kila wakati. Watanzania someni hotuba ya Prof Mruma na Mh Rais ili msipotoshwe....narudia someni zile hotuba kwa umakini sana ....waliofukuzwa sababu zimetolewa ...anayepinga uhalali wa sababu zile aende kwenye hotuba zile anukuu na kuzileta hapa na kuzipangua hoja kwa hoja ....wanaotaka kutumia takwimu kupinga ripoti ni vizuri wakatenda haki ....wachukue kila findings za tume na kuzipinga kwa hoja .....tuache kufanya siasa kwenye mambo ya msingi ....kwenye hili Watanzania watawapigia msumari wa mwisho wa unafiki wa wanasiasa wetu ....Bora Zitto aliyekiri TAFITI hupingwa kwa TAFITI ....Issues za mikataba imegusiwa kwenye ripoti ya tume lakini watu wanakomaa na spinning kupotosha umma ....shame on you ...
 
Duniani kuna watu waongo sana na mtu unapochagua marafiki inatakiwa kuwa makini sana. kuna huyu swaiba wake makufuli.

Kagame ninawasiwasi ndio atakuwa mdanganyifu mkuu na amemuwekea key rais wetu. kwasababu mara nyingi wakikutana kidogo tu ujue lazima kuna sintofahamu itajitokeza.
 
Habari ya siku ya leo, Jumapili murua kabisa wakuu kwa upande wa kwangu.

Naomba niruke kwenye mjadala moja kwa moja bila kupoteza wakati.

Ni hivi.
Kina nani wanaweza kumdanganya Rais wakati linapokuja suala la maslahi ya Taifa? Hii jeuri ya mtu kumdanganya Rais wetu inaweza kutoka wapi, ni nani wanapaswa kuhakikisha Rais wetu hadanganywi?

kwani mimi naamini Rais akishadanganywa basi hata wananchi wote tumeingizwa chaka.

Tumsaidie Rais asidanganywe kwa maslahi mapana na Nchi yetu!
Rais wetu sio malaika ni binadamu, hawezi kujua kila kitu, hivyo ana wasaidizi wa kumsaidia katika kutimiza majukumu yake.

Hivyo watu wa kwanza wanaomdanganya rais ni wale wasaidizi wake wenye jukumu la kuhakikisha rais anakuwa well informed.

Nikutolee mifano michache kuanzia awamu ya Mkapa. Watu walichonga deal wakamshauri Mkapa tununue ndege ya rais, tunahitaji radar na vifaa muhimu vya kijeshi. (Hili la vifaa vya jeshi naomba msiliulizie).

Ununuzi ulifanywa kupitia restricted tendering kupitia a single source. Wasaidizi wa rais wakamshauri tunahitaji sana hiyo radar, ndege na hizo zana!. Kumbe ulikuwa ni uongo mtupu. Watanzania wazalendo hadi wazungu wakapinga sana, na haswa bei tunayopigwa. John Cheyo hadi akamuonyesha bei ya Gulf Stream toka kwenye website yao, lakini Mkapa alitia pamba masikio na tukanunua Ndege, Radar na zana za kijeshi kwa kupigwa!.

Kilichofuata sote tunakijua, japo watu walilipwa mlungula, mimi siamini kabisa kuwa Mkapa hakujua kilichokuwa kinafanyika!.

Likaja suala la EPA, CCM ikataka fedha za uchanguzi, ndani ya Benki Kuu yetu, kumejaa minoti. Wakaunda makampuni, wajanja nao wakachomekea yao wakapiga pesa ndefu. Waziri Meghji aliletewa barua akaambiwa Mzee anajua. Akaruhusu pesa zikachotwa.

Siamini kama Mkapa hakujua wala Kikwete hakujua kuwa ameingia ikulu yetu kupitia fedha za wizi za kampuni ya Kagoda!. Jee unajua hii maana yake ni nini? . Thanks God marais wetu wana kinga ya kutokushitakiwa!

Kagoda Haina Kesi, hawafikishwi Mahakamani Ng'o!

https://www.google.com/url?sa=t&source=web&rct=j&url=/amp/s/www.jamiiforums.com/threads/kagoda-kamwe-haitafikishwa-mahakamani.169015/%3Famp%3D1314937729&ved=0ahUKEwjVrcX1jJLUAhXqI8AKHRJdC-EQFggaMAA&usg=AFQjCNFCtrJxxPf4vHiFqs6oFCboAIWdKQ&sig2=oMEIiWwqYxLqRVk33lxmmQ

Rais Kikwete pia alidanganywa na akadanganyika. Kwenye kashfa ya EPA Rais Kikwete alidanganywa hadi kuvunja katiba kwa kuiachia mijizi ya EPA kurudisha ilichokwiba. Kwenye Escrow pia alidanganywa. Pamoja na mazuri yake yote, pia aliiacha nchi yetu in a mess!. Kazi ya kwanza ya Magufuli was clearing up Kikwete's mess!.

Kama rushwa na ufisadi vilishamiri na kusadifu Mkapa's era na Kikwete's era, this means both of them were corruptible!.

Kwa utendaji huu wa Magufuli ameisha onyesha kwa maneno na matendo kuwa anachukia rushwa, unachukia ufisadi, anachukia uzembe, na anachukia sana kudanganywa. Ila pia on the other side he is very human akiambiwa ukweli na mfano mzuri ni issue ya Bashite, baada tuu ya kuibuliwa Bashite alimwendea na kurudisha confess kila kitu kuwa ni kweli. Akamlinda.

Hivyo sina uhakika kama Magufuli atakubali kudanganywa. Ila kama nilivyosema mwanzo na yeye ni binadamu na sio malaika, Hivyo anaweza akadanganywa na akadanganyika, lakini Watanzania wazalendo tusikubali rais wetu adanganywe, na akidanganywa asidanganyike, ila akidanganyika iwe ni yeye tuu kwa ubinaadamu wake, sisi Watanzania wengine tusikubali kudanganywa na kudanganywa!.

Kwenye hili la mchanga wa makinikia ya dhahabu, japo tayari ameishanganywa kuwa Tanzania ndio inchi inayoongoza kwa kuzalisha dhahabu nyingi duniani kuliko nchi
nyingine yoyote kupitia taarifa ya viwango vya dhahabu kwenye makontena 277 ya mchanga wa dhahabu wa migodi miwili tuu ya ya Acacia!.

Paskali
 
Back
Top Bottom