bakundande jr
JF-Expert Member
- Oct 22, 2021
- 507
- 670
Kwa kuanza nianze kuwasalimi wadau wote wa jamii forum. Amani iwe juu yenu/Assalam aleykum kwenu nyote mabibi na mabwana.
Kwa muda mrefu na mara nyingi katika familia zetu kina mama hukaa muda mwingi na watoto wao kuliko kina baba ambavyo hukaa nao, hii inatokana na utekelezaji wa majukumu mbalimbaili ya kijamii na kiuchumi.
Hali hii hupelekea watoto kujenga urafiki sana hasa na kina mama, hufikia hatua mtoto akiwa na shida yoyote huanza kumueleza mama kabla ya baba na wakati mwingine huogopa kabisa kumweleza baba yake shida alionayo na kupelekea kina mama kuwa kama daraja la mawasiliano baina ya baba na mtoto.
Sisemi ni jambo baya ila mara nyingi kina mama wengi hutumia nafasi hiyo kujikweza kwa watoto na kuficha uwajibikaji wa waume zao wakati wa kutatua shida za watoto. Mfano unakuta mtoto kaomba pesa kwa ajiki ya manunuzi ya vifaa vya shule ama matumizi mengine bila kuficha mama humwambia mumewe kuwa kijana wetu anashida hizi.
Cha ajabu baba akitoa pesa ni kina mama wachache ambao huweza kusema hii pesa baba yako katoa kwa ajili yako. Kitu pekee ambacho kina mama wengi huwaambia watoto kuhusu baba zao ni "SUBIRI BABA YAKO ARUDI" hii ndio huwa kauli inayotolewa na kina mama pale tu mtoto anapokosea.
Jambo hili hupelekea watoto kuona baba zao kama mahakama. Na kupelekea watoto wengi kutokuwa na mapenzi hasa kwa baba zao.
Kwenu kina mama sio kosa kumwambia mwanao mame na mazuri ya baba yake ili kudumisha upendo baina ya baba na mtoto.