Kina dada ni nani aliwakataza kuwasalimia wanaume pindi mkikaa nao siti moja safarini?

the_forum

JF-Expert Member
Apr 28, 2017
774
1,003
Katika uzoefu wangu wa kusafiri hasa katika routes za DOM, DAR, ARUSHA, KILIMANJARO, MBEYA.

Lakini pia hata routes ndefu ndefu za ndani ya mji! Mfano;

SIMU2000 -MNAZI MOJA
MBEZI - BUGURUNI
SIMU2000- MBAGALA, G. MBOTO

Ikitokea mwanaume umekaa na mdada seat moja? Ni mara chache mdada kutoa salam au kuanzisha maongezi hata safari ikiwa ni ndefu sana.

Sasa kina dada napenda kujua kama mkikaa siti moja na mwanaume either wa umri wako au mkubwa kwako (makamo), nini hasa inakua fikra ya kwanza kichwani kwako! Na kwanini wengi mnasubiri hadi msalimiwe ndo mjibu salam na sio nyie kuanza kusalimia?

USHUHUDA:-
Miaka michache nyuma, nilikua natoka Dar naenda mkoa fulani, nilikaa na mdada kwa kua aliamua kupiga kimya na mimi sikua na mood siku hiyo nikapiga kimya hadi tunafika Morogoro hata salam hatujapeana! Wakati tunaondoka sasa Morogoro baada ta kupata chakula, yule dada aliingia na box la juice ya Azam kwenye bus, bahati mbaya bus linavoondoka box likaniangukia na juice ikanimwagikia mapajani! Alitaka anifute na kitambaa chake nikakataa nikajifuta mwenyewe.

Ila safari nzima kuanzia hapo yule dada akawa kama MC, yani kumbe ni muongeaji vibaya mno! Mimi nipo cool yeye anaongea sana. Kujitambulisha sana kuniambia dhumuni la safari yake, a bit of her family issues.

Kina dada naomba kujua kwanini mna hii tabia, au ni kiburi au maringo au dharau?
 
Hata mie nna hio tabia ndo maana nimejibu kulingana na mazingira husika. Nikimkuta mbabu namsalimia nimemaliza, kazi inahamia kwenye simu au kuangalia nje mpaka mwisho wa safari.

Nikimkuta mkaka nauchuna
Ok sasa wew mfano safr ya mkoa...ukikaa na mkaka siti moja hua unamuwazia nn kichwani mwako! Au hata ikitokea kaamua kukuchangamkia pia hua unamuwazia nini!?
 
Kwa madada wengi nadhani ni namna ya kuanzisha maongezi...


Unajua kwa sisi mwanaume unapoanzisha maongezi na mwanamke alafu akakukaushia tunachukulia easy, simple...

Siyo kwa mwanamke.. Ndiyo maana wanakaa kimya mpaka wewe ndiyo umuanze...


Cc: mahondaw
I like the idea! Inaweza kua kweli kabisa...tatzo mdada ukimuanza na ukaonesha kumchangamkia basi anahisi unamtaka...hii unaivhukuliaje mkuu
 
Huwa nawaza huyu sio type yangu ni ya mwanangu ajae maana wakaka huwa mnapenda dogo dogo mtu una miaka 50 unaoa kabint miaka 20
Umetisha mkuu! Ila Kama ameclick kichwani mkuu hua unaonesha njia? Unatoa ushirikiano wa story!?
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Back
Top Bottom