Kila binadamu anastahili heshima kwa sababu ya ubinadamu wake: Mengine ni matokeo ya heshima na ama dharau

Yoranda

JF-Expert Member
Jan 9, 2020
341
333
Wakuu heshima kwenu.

Niende kwenye somo tajwa hapo juu, leo mishale ya saa tisa alasiri mjini morogoro nilianzia Safar kuja jijini Dsm(jiji la Makonda).

Tukiwa tumetoka mwezi mtukufu hata matendo yetu sisi kina meko yamenywea, nilipata siti moja na mrembo mmoja, sikutaka kuongea nae chochote japo nilijua nikichomekea kamba zingenasa. Huyu dada mweupe, sura ya kiplfilipino, vidole vyeupe, kiuno kipana kiasi, sio mfupi saana, amejitanda sehemu kubwa ya masikio na sehem ndogo tu usoni inaonekana, inaelekea hakutaka mawasiliano au kuonekana saana, bila shaka hata yeye mwezi wetu mtukufu ukimnyoosha,nilijaribu kuona Kama anabastola bila mafanikio.

Alikuwa muda mrefu kwenye Simu akiongea, na kwa kuwa sikutaka kuchokoza na mazungumzo sikupenda kuyajua, aliongea kwa sauti ya wastani kukufanya jirani uskie anacholonga.

Baada ya muda kidogo nafsi fisadi, ilinipeleka kutaka kusikia nini kinaongelewa tena na binti mrembo hivi.

Umbali wa Moro chalinze, alichoka kuongea na Simu, nilijua asingependa kuzungumza, na ndivyo hali halisi ilionyesha hivyo, sisi mabaharia tunapokutana na makauzu tunakuwa wapole na wanyenyekevu. Sikumbuki kama nilimgusa kwa bahati mbaya, akaruka, la haulaa! Siti mbili za mbele na moja kushoto kwangu waligeula, kwamba mzee baharia anachombo hapo anataka kukibaka Nini?!?!!!;+^¥¢.

Wakuu nilijenga attention ya asilimia 100 nadhani IQ yangu ilivuka nje ya box. Kuwa huyu anadhani nilimtekenya? Huyu anahisi nimemuona mzur saaana kwa hiyo anajistukia? Na kwamba huyu hapa ndio mzuri sana kuliko wote? Maswali ya sekunde moja, nikamuomba radhi tu ikiwa nimemkwaza! Akanyamaza. Jirani wa siti ya Kati alishangaa kwa nn naomba radhi alikuwa live bila chenga sijafanya chochote, wakati binti ameangalia kushoto jamaa akaniukiza sheikhe mbona unaomba radhi bila sababu, nikamjibu ukikaa na malaika mjue akupende.

Baada ya nusu, nikanunua korosho nikagawa siti yetu binti mrembo akarogwa akapokea.

Mamaae! Tukazidi kuwa karibu ya aibu, wakuu dharau weka kando katika maisha yako. Binti aliomba radhi mwenyewe, nikamuuliza kwani nilikufanya nini?? Akasema Ni stori ndefu, tukiwa chalinze baharia nikanunua ice cream na ukwaju.

Binti akapokea tena. Nikamuonea huruma tu, nikabaki katika kauli ya kila binadami mpe heshima yake, nikaona anastahili heshima badala ya kwenda kumbandua kwa kosa la kufedhehesha nafs iliyojaa wema.
 
Back
Top Bottom