Wana Jf
Naomba nitoe wito kwa kina dada ambao bado mama zao bado wako hai au mama wazazi wanao walea au ndugu wa karibu kama walezi ili wajifunze naswala mengi ya muhimu ya ndani, imekuwa aibu sana nje kwa wengine wasichana akikutana na mwenza kwenye maeneo kama:
1. Mapishi: Kina dada tusisubiri kuelekezwa na kufundishwa kupika tukiwa wakubwa au tunapotaka kuolewa sio vizuri hata, muda wowote na wakati wowote unaweza ukajikuta unaanza maisha flani mfano kuishi hostel ukizingatia wazazi hawana pesa ya kukupa kula hotelini kila siku, kwa hostel zinazoruhusu wanafunzi kujipikia jitahidini muda mwingi muwe mnakula chakula mlichopika na mjifunze kwa wengine, unaweza ukaenda kuishi kwa ndugu wa karibu kutokana na dharura au shugjuli flani, unaweza ukaenda kuishi kwa mwanaume au mume ambaye atakuwa na ww muda wote na siku zote, tusisubiri kwenda kujifunza huko ni aibu kwa wazazi wako kuwa hujafunzwa, haipendezi. Nliwahi kuishi na mdada kwa wiki moja ndio alikuwa amemaliza chuo kikuu sasa anatafuta kazi basi kupika ugali wa mahindi haikuwa rahisi kwake, akipika ugali unakuwa haujaiva au una mabonge na mlaini kama uji, kupika mboga kama dagaa ni kibarua kigumu sana niseme kwamba eneo hili ukikosea au usipojitahidi kujifunza ni aibu sana ukiwa kwako usimtake mwanaume amtafute msichana wa kazi ndani ya muda mchache baada ya kuolewa pambana kwanza mwenyewe na nyumba yako hadi mume atakuhurumia, usifanye kumchukua msichana wa kazi akawa mpishi zaidi yako hadi mume akubali mapishi ya msichana wa kazi zaidi ya yakwako maana mapishi yako yanaboa tuliangalie sana swala la mapishi, tukiwa majumbani tunapolelewa tuache kwanza habari ya ku chat na simu muda wote tutilie maanani swala hili la upishi na tuwe na juhudi za kupenda kukaa karibu na mama zetu wanapokuwa wanapika tuzoee na tuwe wazoefu.
2. Usafi: Anapo lala msichana, chini ya uvungu wa kutanda anapolala, choo anachokitumia lazima kiwe kisafi muda wote, vyombo anavyo vitumia muda viwe visafi, wapo wanao olewa na kuwafanya waume zao kutopenda tabia ya uchafu zaidi sana wanaume wapenzi wa usafi, hata mdada aendako kwa ndugu ajitahidi kuwa msafi, muonekano wa nje unapoonekana barabarani ukiwa umependeza uendane na unapolala na unapoishi, lazima tutenge muda wa usafi na muda wa kufanya mambo mengine, yote haya yatatusaidia kuepukana na maradhi na magonjwa mbali mbali tusiyoyategemea na hivyo hata kumfanya ndugu, mume, bwana au rafiki kuomgeza mapenzi kwako, usafi haufundishwi siku ya sendoff au kitchen party bali mtu hujifunza na kuupenda mwenyewe.
Niseme kwamba yapo mengi ya kujifunza na kuomba kufundisha haswa huduma yako inapohitajika na wengine lazima uonyeshe kwa umri wako kuwa unaweza sio huwezi na kusababisha aibu. Naomba dada zetu kweli tengeni muda wa ku chati, kwenda kudhurura, kufanya kazi za ajira au vibaruwa na muda wa mapishi na usafi waachieni wanaume wakahangaike kula mahotelini, ninyi wekeni jitihada nyingi sana katika kupika na kuandaa mazingira ya unapoishi ili msifike muda wote mjue kuwa raha kwenu ni kusifiwa na si kuonyesha chukizo na aibu maana hamchelewi kulia.