Kimya kinachouma

Nimekaa kimya kwa muda… sio kwa sababu sina cha kusema, bali nimechoka kueleza ninachopitia.

Kuna kipindi unajaribu kila njia, unaomba msaada, unajipa moyo kwamba kesho itakuwa tofauti, lakini mambo yanaendelea kukubana.

Kwa sasa nimefika sehemu sina nguvu ya kuendelea kujieleza sana. Nimekata tamaa ya kutegemea watu, lakini bado sijakata tamaa kwa Mungu.

Kama kuna kitu kinachonishikilia leo, ni imani kwamba Mwenyezi Mungu anaona yale ambayo hakuna mwanadamu anayayaona.

Sina mengi ya kusema kwa sasa… namwachia Mungu. 🤲
 
Kuna kipindi mtu ananyamaza si kwa sababu hana cha kusema, bali kwa sababu amechoka kueleza anachopitia.

Kwa sasa nimefika sehemu ambayo sina mengi ya kuomba kwa watu. Nimeamua kumtegemea Mungu, nijikusanye na nitafute njia ya kusimama tena.

Mwenye kunielewa, Mungu ambariki. 🙏🏾
 
Unatoa wapi Hela ya bando?
 
Pole sana mkuu,
Lakini nimewaza kwa sauti.. hii ni thread yako ya 2 naona unaomba the same amount, tutajuaje kama haujaanzisha tone tone campaign huku JF?? Tutajuaje kama hiyo elfu 20 umeshaipata ili watu wasiendelee kutuma!??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…