kimwili CCM kiroho CHADEMA

kimwili CCM kiroho CHADEMA

Tujisahihishe Tz

Platinum Member
Joined
Nov 17, 2011
Posts
3,061
Reaction score
1,367
Nilimsikia Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, akisema (Chadema) hakina hazina ya viongozi kama iliyonayo Chama Cha Mapinduzi (CCM). Alitamba kwamba CCM inaweza kusimamisha wagombea urais 20 wenye sifa zinazofanana, lakini Chadema inamtegemea Dk. Wilbrod Slaa pekee.

Kwa maelezo yake, mtu kama Mbowe, hana sifa za kuwa rais kwa sababu ni mchezesha disko la usiku! Madai haya ya Mzee Sitta si ya leo. Ameanza kuyazungumza siku nyingi. Yametuchosha kuyasikia. Wakati mwingine si jambo la busara sana kwa mtoto kuingia
kwenye malumbano na mtu aliyemzidi umri, lakini inapotokea mzee akapuuza hatari iliyo mbele yake; hatari ambayo mtoto anaijua, huyo mtoto asipomweleza ukweli huyo mzee, atakuwa amefanya kosa hubwa.

Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, katika maandiko yake kupitia Kitabu cha Tujisahihishe aliyoyatoa Mei, 1962 (miaka 50
sasa) alisema, "Ukweli una tabia moja nzuri sana, haujali mkubwa wala mdogo, haujali adui wala rafiki. Kwake watu wote ni sawa.
Pia ukweli unayo tabia ya kujilipiza kisasi kama ukipuuzwa.

Ukiniona nataka kupiga teke jiwe kwa kuwa unafikiri kuwa ni dogo au mpira, natumaini utanionya. Lakini nikilipuuza onyo lako kwa sababu eti wewe ni mdogo au kwa sababu sikupendi, nikalipiga teke, basi litanivunja dole japo ningekuwa nani. Ukweli haupendi
kupuuzwapuuzwa."

Mwisho wa kunukuu. Nukuu hii nimeitumia ili Mzee Sitta na wahafidhina wengine ndani ya CCM wasidhani kuwa nawakosea adabu kuwakosoa. Pili, Baba wa Taifa, kwa kutambua kuwa kuna watu wanaoacha kujadili hoja ya msingi na kurukia mambo yasiyoendana kabisa na ukweli wa mambo, kupitia kitabu hicho hicho cha Tujisahihishe, alisema,

"Wakati mwingine mtu tunayempinga huwa ana makosa kweli, lakini hoja tunazotoa ni za kibinafsi na hazihusiani kabisa na hoja zake. Nikisema mbili na tatu ni sita, nakosa. Lakini ni bora kunionyesha kwamba pengine nafikiri tunazidisha kumbe tunajumlisha. Ni kweli mbili mara tatu ni sita, lakini mbili na tatu ni tano, siyo sita. Lakini ukijaribu kuwashawishi wenzetu wakatae mawazo yangu na kukubali yako kwa kusema kuwa meno yangu ni machafu, au natoa kamasi daima, utakuwa unatumia hoja ambazo hazina maana.

Huu ni mfano wa upuuzi, lakini mara nyingi hoja tunazotumia kuwashawishi watu wakatae mawazo ya wale tusiowapenda, au kukubali mawazo yetu huwa hazihusiani kabisa na mambo tunayoyajadili." Mwisho wa kunukuu. Hapa utaona kuwa hoja kwamba
Mbowe ni mcheza au mwendesha disko, hazikusiani kabisa na suala la kumpata Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Dunia imeshuhudia mataifa mengi duniani yakiongozwa na watu waliopitia mazingira na kazi mbalimbali (wakiwamo tunaowaita waasi).
Kuna mataifa yameongozwa na wana muziki. Yapo yaliyoongozwa na wacheza mieleka. Sidhani kama kuna mtu kazaliwa, kaa bila kufanya shughuli yoyote, mwisho wa siku akaipata kazi aliyopangiwa akingali tumboni, yaani kazi ya urais.

Hata Mzee Sitta mwenyewe si ajabu alikuwa mchunga mbuzi kabla ya kuijua siasa! Je, tuseme sasa kuwa hafai kuwa rais kwa
sababu amepata kuwa mchunga mbuzi? Kichwa cha makala yangu, "Kimwili ni CCM, rohoni ni Chadema", kinajieleza vizuri. Sitta
alijidanganya kwa nadharia zake za kwamba Chadema anayoiona sasa ndiyo Chadema baada ya kuingia madarakani.

Mara zote nadharia hizi zimethibitika kinyume kabisa. Kwa mfano, wazee waliokuwapo wakati wa harakati za TANU kudai Uhuru wa Tanganyika wanasema Mwalimu Nyerere na wapambanaji wengine walipuuzwa na kubezwa mno. Wabezaji hawakuwa Wazungu, Waarabu, machotara na Wahindi pekee, bali hata Waafrika weusi. Hawa ni wale walioamini kuwa hakuna Mwafrika anayeweza
kuwang'oa wakoloni. Mwafrika alionekana kuwa dhaifu katika kila idara. Kigezo cha elimu kilitumika kama moja ya nyenzo za kuhalalisha fikra hizo potofu.

Wapo waliohoji, "Wanataka Uhuru, wakiupata nchi itaongozwa na nani ilhali hakuna wasomi?" Maneno hayo hayakuwakatisha
tamaa wapambanaji mahiri wakiwamo kina mama kama Bibi Titi Mohamed ambao hawakuwa na elimu kubwa. Baada ya Uhuru wakapatikana watu wenye sifa ya kuwa viongozi, hata kama kwa idadi walikuwa wachache. Wakawamo watu kama kina Dereck Bryceson, Amir Jamal, Alnuur Kassum na kadhalika.

Hawa wakaungana na wenzao weusi kuliongoza taifa jipya la Tanganyika. Hii maana yake nini? Maana yake ni kwamba wakati wa harakati za mapambano ya kudai Uhuru si Wazungu, Wahindi au machotara wote waliotaka kuonekana wakiwa mstari
 
Mimi nafikiri Sitta hakuelimika vizuri, labda akiusoma uzi huu nakuchanganya na tamko lililotolewa na Dr. Slaa ataelimika. ILA USISAHAU KUMDAI TUITION FEE HUYU 6.
 
samwel sitta, spika wa viwango aliyewahi kutokea katika historia ya tanzania
 
KAMA CCM INAHAZINA KUBWA YA VIONGOZI IMEKUAJE TENA INARUDIA TENA WATU WALIOSTAAFU( Kinana) na WENGINE WALIOSHINDWA HATA CHAGUZI ZA WILAYANI/MIKOANI (mangula) Iko wapi hiyo hazina ya viongozi??? mpaka manarudiarudia viporo na watu wenyesifa za kushindwa???
 
Ina maana Samwel 6 kiroho CHADEMA lakini kimwili ccm?

Samwel 6 hata akija CHADEMA leo, atafit wapi?

CHADEMA haitaki watu wanaotafuta tuu makuu! Huyu si alikuwa na ndoto za urais

CHADEMA haina haja ya watu watakaokuja kwa sharti la kupewa kugombea Urais ujao!

CHADEMA kinataka watu wa kuja kutumika kukijenga chama, siyo kufikia kwenye Urais.

Nadhani viko vyama vingine vina hitaji hilo ila bahati mbaya ni kwamba uwezekano wa kuupata urais ni mdogo ndiyo maana hawawezi kuhamia huko hata kama wataahidiwa kugombea Urais kupitia vyama hivyo

Kwa hiyo wabaki huko huko na haya maneno yao mengine dhidi ya CHADEMA ni maneno ya sungura tu ya 'sizitaki mbichi hizi', kumbe......
 
Mimi nafikiri Sitta hakuelimika vizuri, labda akiusoma uzi huu nakuchanganya na tamko lililotolewa na Dr. Slaa ataelimika. ILA USISAHAU KUMDAI TUITION FEE HUYU 6.[/QUOTE

Lipi jipya alilolisema hapo? naona kama aliyeandika ni MBOWE mwenyewe vile, analalamika baada ya kuambiwa ukweli na SITTA. Mwenyewe analijua hilo kuwa hana sifa za kuiongoza nchi, kama hajasoma vizuri katiba ya nchi anaweza kujidanganya kuchukua fomu. Elimu ya kidato cha nne na sifa ya kuwa karani wa benki kuu, tena kwa mgongo wa MTEI? tutakuwa tunajidhalilisha ndani na nje ya nchi.
 
Ina maana Samwel 6 kiroho CHADEMA lakini kimwili ccm?

Samwel 6 hata akija CHADEMA leo, atafit wapi?

CHADEMA haitaki watu wanaotafuta tuu makuu! Huyu si alikuwa na ndoto za urais

CHADEMA haina haja ya watu watakaokuja kwa sharti la kupewa kugombea Urais ujao!

CHADEMA kinataka watu wa kuja kutumika kukijenga chama, siyo kufikia kwenye Urais.

Nadhani viko vyama vingine vina hitaji hilo ila bahati mbaya ni kwamba uwezekano wa kuupata urais ni mdogo ndiyo maana hawawezi kuhamia huko hata kama wataahidiwa kugombea Urais kupitia vyama hivyo

Kwa hiyo wabaki huko huko na haya maneno yao mengine dhidi ya CHADEMA ni maneno ya sungura tu ya 'sizitaki mbichi hizi', kumbe......

Wajanja wanatakiwa kuelewa vizuri ulichokisema hapa mkuu, Hivi kweli kwa akili zako, NASSARI, LEMA, SUGU, ABWAO, OWENYA na KIWELU wako CHADEMA kwa sababu wanafiti na kwamba wanamzidi SITTA? ZITTO sijui kama amesoma huu mchango wako, CDM wanaka watu wa kujenga chama kama yeye na baadaye, wale MBOWE, SLAA na MTEI, ha ha haaa, kazi kwao wale wanaotumika CDM kama daraja nadhani ujumbe huu utakuwa umewafikia.
 
samwel sitta, spika wa viwango aliyewahi kutokea katika historia ya tanzania

Tena aliyekuwa akililiwa na CDM ahamie kwao kwa uchonganishi kuwa ametoswa na chama chake kurudia kwenye u-spika , leo wanamponda baada ya kuwaambia ukweli.
 
KAMA CCM INAHAZINA KUBWA YA VIONGOZI IMEKUAJE TENA INARUDIA TENA WATU WALIOSTAAFU( Kinana) na WENGINE WALIOSHINDWA HATA CHAGUZI ZA WILAYANI/MIKOANI (mangula) Iko wapi hiyo hazina ya viongozi??? mpaka manarudiarudia viporo na watu wenyesifa za kushindwa???

Unataka kutuambiaje, 2015 Sasa ni ZITTO na siyo SLAA kwa vile CDM hawarudii?
 
Kwa maelezo yake, mtu kama Mbowe, hana sifa za kuwa rais kwa sababu ni mchezesha disko la usiku!

Hata Mzee Sitta mwenyewe si ajabu alikuwa mchunga mbuzi kabla ya kuijua siasa! Je, tuseme sasa kuwa hafai kuwa rais kwa
sababu amepata kuwa mchunga mbuzi? Kichwa cha makala yangu, "Kimwili ni CCM, rohoni ni Chadema", kinajieleza vizuri. Sitta
alijidanganya kwa nadharia zake za kwamba Chadema anayoiona sasa ndiyo Chadema baada ya kuingia madarakani.

Hawa wakaungana na wenzao weusi kuliongoza taifa jipya la Tanganyika. Hii maana yake nini? Maana yake ni kwamba wakati wa harakati za mapambano ya kudai Uhuru si Wazungu, Wahindi au machotara wote waliotaka kuonekana wakiwa mstari

Sasa wewe unataka kulinganisha mchunga mbuzi na mpiga disco anaepata kipato kupitia pombe na makahaba?
Halafu unatupostia hotuba ndefu hivi unafikiri tuko ktk majukwaa ya kutangaza orodha ya mafisadi?
 
Pamoja na uchambuzi murua toka kwa ndugu yangu Yericko nyerere mi ninaamini ktk maisha ya wanaccm hawajawahi kukutana na upinzani kama wa chadema,wameshindwa kulaghai top leaders wa chama,wamejikuta wanavuliwa nguo kila uchwao na hadi kuanza kupick presidential materials ktk chama,wanajaribu kumchokoza mh.mbowe kwa kuwa wanamfaham zaidi hasa ktk pilika zake za kimaisha,lakini wanasahau pamoja na kuwa na dr.slaa as presidential material lakini wapo wengine,anyways mzee sitta ni mtu wa kumsamehe bure kwakuwa stress za mwaka 2010 kwenye kugombea u-spika zilimchanganya sana mpaka akaishia kuhongwa uwaziri,yeye kwasasa anaishi kwa fadhila ktk chama chake vinginevyo kama yeye mpenda haki basi angalikataa uwaziri.labda siyo vizuri kuwasema wazee lakini ajue ukweli unabaki kuwa ukweli hata kama umezungumzwa na mdogo.ila aache uchumia tumbo kama kweli yeye ni mzalendo kwa nchi hii.
 
Last edited by a moderator:
Unataka kutuambiaje, 2015 Sasa ni ZITTO na siyo SLAA kwa vile CDM hawarudii?

Ni nyinyi ccm mlisema chadema inauongozi mwembamba, nyinyi wenye uongozi mpana mbona mnarudiarudia matapishi ya waliostaafu na kushindwa chaguzi ndogo kama (Mangula na Kinana)? CDM ni wachache lakini sauti zao ni kubwa na zinatingisha nchi kuliko hao mafisadi wengi wa Chama cha majambazi.
 
Nilimsikia Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, akisema (Chadema) hakina hazina ya viongozi kama iliyonayo Chama Cha Mapinduzi (CCM). Alitamba kwamba CCM inaweza kusimamisha wagombea urais 20 wenye sifa zinazofanana, lakini Chadema inamtegemea Dk. Wilbrod Slaa pekee.

Kwa ufisadi, unafiki, umalaya na kupenda tambo zisizo na msingi kama tulivyoshuhudia Dodoma juzi. Wengine wanachotambua ni kujipendekeze pendekeza tu kwa wakuu ili kupata uongozi (mfano Kimbisa na hoja ya kubadilishwa jina chuo kikuu cha Dodoma ili kiitwe Mrisho Jakaya Kikwete). Wote wana mawazo mgando tu, hakuna jipya. Si wazee si vijana.
 
Back
Top Bottom