Kimondo ni kitu gani?

K 4 LIFE

JF-Expert Member
Jul 21, 2015
2,567
416
Wakuu tunafahamu kitu kinaitwa kimondo hiki kimondo uonekana mara chache sana kikitoa mwanga wakati wa usiku na kikimbia angani kuelekea chini na ghafla upotelea angani.

Je hiki kimondo nini? kinatokea wapi na uwa kinaelekea wapi?kwa nini kimondo upotea angani kabla ya kufika chini? au kinauhusiano na mambo ya uchawi?
 
Kimondo au kwa lugha ya wenzetu wanakiita shooting star. Ni mawe makubwa ambayo mara chache hupita kwenye uso wa dunia kwa kasi sana na kuacha miale ya mwanga kama moto kwa mvutano unatokea baina ya nguvu ya dunia na chenyewe.
 
Kimondo sio Jiwe wala chuma niliwahi kukiona pale mbozi mbeya. Ila sio jiwe wala chuma.
 
Kimondo ni mfano wa jiwe lenye moto nakumbuka ilishawahi kuanguka sehemu nishasahau ila linataka kufanana na jiwe hupita kwenye uso wa dunia

Na kazi ya kuu nikulinda mipaka hususan huachiwa kwa ajili ya kushambuliwa majini na shetani wasivuke mipaka maana hata malaika anamipaka yake akipitiliza anaunguzwa vilevile.
 
Kimondo au kwa lugha ya wenzetu wanakiita shooting star. Ni mawe makubwa ambayo mara chache hupita kwenye uso wa dunia kwa kasi sana na kuacha miale ya mwanga kama moto kwa mvutano unatokea baina ya nguvu ya dunia na chenyewe.
Mkuu umeukaribia ukweli,
Sasa ni hivi hili jiwe linasafiri kwa kasi sana na wakati linasafiri likishalikaribia jua linaunguzwa na kuyeyuka na ndio maana unaona linakuwa na kama na mkia, hapo ujue lililuwa kwenye speed na likajipitisha very close to the sun.
Kama kuna mtu anahitaji ufafanuzi zaidi asema.
 
Kimondo ni mfano wa jiwe lenye moto nakumbuka ilishawahi kuanguka sehemu nishasahau ila linataka kufanana na jiwe hupita kwenye uso wa dunia

Na kazi ya kuu nikulinda mipaka hususan huachiwa kwa ajili ya kushambuliwa majini na shetani wasivuke mipaka maana hata malaika anamipaka yake akipitiliza anaunguzwa vilevile.

kama kina linda mipaka sasa chenyewe kiko upande gani wa shetani,majini,yesu,mazimwi au?
 
Kimondo ni mfano wa jiwe lenye moto nakumbuka ilishawahi kuanguka sehemu nishasahau ila linataka kufanana na jiwe hupita kwenye uso wa dunia

Na kazi ya kuu nikulinda mipaka hususan huachiwa kwa ajili ya kushambuliwa majini na shetani wasivuke mipaka maana hata malaika anamipaka yake akipitiliza anaunguzwa vilevile.

au kinalinda mipaka ya nchi?
 
Acha kudanganya watu.
 
Mkuu umeukaribia ukweli,
Sasa ni hivi hili jiwe linasafiri kwa kasi sana na wakati linasafiri likishalikaribia jua linaunguzwa na kuyeyuka na ndio maana unaona linakuwa na kama na mkia, hapo ujue lililuwa kwenye speed na likajipitisha very close to the sun.
Kama kuna mtu anahitaji ufafanuzi zaidi asema.

Linasafiri kutoka wapi mpaka lipite karibu na jua?.
Kwa hiyo kama halitapita karibu na jua halitaunguzwa na kuyeyuka?.
Natanguliza shukrani.
 
Kuna majini wanapenda kusikiliza mazungumzo (siri) yanayozungumzwa mbinguni na malaika, hawatakiwi kuyasikia, kwa hiyo jini yeyote anaekaribia tu eneo hilo hurushiwa hicho kinachoitwa kimondo (moto).
 
Linasafiri kutoka wapi mpaka lipite karibu na jua?.
Kwa hiyo kama halitapita karibu na jua halitaunguzwa na kuyeyuka?.
Natanguliza shukrani.

Kaka nisome kwa makini sana nitajaribu kuelezea kwa kutumia kiswahili japo nitachanganya na maneno ya kingereza kwani hata kama hivi vimondo vina majina ya kiswahili yatatuchanganya.....

Kwenye SPACE kuna nyota nyingi sana na zile sayari zinazojulikana, nyota zipo kubwa na ndogo na kuna nyota kubwa kuliko hata ukubwa wa hii dunia. Baadhi yake zimeundwa kwa mawe, namaanisha sakafu ya hizi nyota ni mawe na baadhi yake hizi nyota na sayari zina volcanic activity ambazo zipo active au zilishawahi kuwa active.
Kuna kitu kinaitwa METEOROID hili ni jiwe dogo linalosafiri kwenye Space, space ni nje ya dunia huko kwenye nyota na sayari zinapoelea,
Kuna mawe mengine yanaitwa asteroids, ni kitu kile kila kama meteoroid ila asteroid ni kubwa kidogo zaidi ya meteoroid, kuna jamii nyingine inaitwa comets.."icy dirty ball" hii comets ina mchanganyiko wa mawe,water ice na mchanganyiko wa baadhi ya gesi kama methane cabondioxide,monoxide.
Kaka sasa hii comet wakati inasafiri ikipita pembeni ya jua zile gesi zinayeyusha na ukali wa joto la jua na linatengeneza kitu kama tail. Unaweza ukaona nyota imepita kwa speed na mkia mrefu ...
Turudi kwenye Meteoroid, yenyewe nayo inasafiri kwa speed kali sana inaweza ikazidi 72,000km/h. Sasa kuna kitu hapa kinaitwa aerodynamic heating-is heating of an object produced by its high-speed passage through air, yani speed yake kali tu inakisababisha kipate moto kiungue na wewe unaona kama moto umepita angani fasta.
. Kaka nadhani umenipata kidogo .
Nisiendelee sana sitaki nikuchanganye.
Hayo mengine ni kudanganyana tu ila hii ndio concept.
 
Back
Top Bottom