Kimfaacho mtu chake wahenga hawakukosea

Daisy Llilies

JF-Expert Member
Apr 19, 2019
1,017
2,154
Miaka 20 iliyopita kuna mtu alinipa habari ya nyumba inayouzwa, hii familia ilikuwa inamuuguza mzazi wao na katika shida waliuza nyumba ya familia. Mjengo ulikua vyumba sita na uani choo cha shimo, bafu na jiko, pamoja na vyumba vitatu vya ziada.

Sikutegemea kama nitaishi mitaa ile. Nilionana nacwapangaji na kuwaelekeza ya kufanya. Nyumba ni ya zamani sana lakini aliyejenga alitumia matofali 25 kwa mfuko mmoja wa saruji. Kuta za nyumba ni imara sana.

Miaka mitano iliyopita maisha yaliyumba. Sikuwa na kipato cha uhakika. Wazo lilinijia, niliwapa notice wapangaji wote. Nilikarabati nyumba. Niliziba choo cha shimo na kuweka Indian toilet mbili pamoja na mabafu ya shower Nilibadili paa kwani mabati ya awali yakikuwa yamechoka. Chini niliweka tiles na madirisha ya aliminium.

Nyuma upande mmoja nilibadili vyumba viwili kuwa jiko na dining na sebule ya familia. Mbele nimeweka frame mbili za maduka kwa laki moja na nusu kila moja kwa mwezi. Vyumba viwili nimepangisha kwa 60,000 chumba kimoja.

Nina uhakika wa kupata laki nne kila mwezi kutokana na kodi.
 
Story kama inakuja inapotea hivi njiani, je umeiona kesho yake?
 
Back
Top Bottom