Kimenuka udom

Kimenuka udom

CELLO

Member
Joined
Sep 6, 2013
Posts
11
Reaction score
3
Ndugu wana jamvi kuna taarifa zilizonifikia kutoka vyazo mbali mbali vya habari kutoka chuo kikuu cha Dodoma(UDOM) Kitivo cha lugha na sayansi za jamii kuwa kuna mgogoro unaofukuta ndani ya serikali ya wanafunzi(UDOSO) katika kitivo hicho,unaoweza kusababisha kuanguka kwa serikali hiyo.Vyanzo vya habari vinasema mgogoro huo ulianza mara baada ya bunge kugundua kuwepo kwa ubadhirifu mkubwa ndani ya serikali uliowahusisha raisi wa serikali hiyo aliejulikana kwa jina moja Janus,waziri mkuu aliejulikana kwa jina la Willium Joseph pamoja na waziri wa fedha aliyejulikana kwa jina moja la Perezi.Hata hivyo viongozi hao waliamuriwa na kamati ya bunge iliyoundwa kuchunguza ubadhirifu huo warudishe fedha hizo kiasi cha shilingi milioni moja walizokuwa wamekwapua.

Hata hivyo vyanzo vya habari vinaendelea kudokeza kuwa mgogoro huo haukuishia hapo kwani uliendelea chini kwa chini kwa baadhi ya wabunge na mawaziri wawili kutoka wizara nyeti kushinikiza kuwa viongozi waliohusika wawajibike kikatiba ili kulinda hadhi ya serikali hiyo na chuo kwa ujumla.Hata hivyo viongozi hao hawakuwajibika na kuanza kupanga mipango michafu dhidi ya viongozi hao walioamua kupigania maslahi ya wanafunzi wenzao.

Habari zinasema kuwa mipango ya kuwaondoa mawaziri hao ulianza hasa kwa waziri anaejulikana kwa jina moja Kawiche ambae yeye amekuwa akipingana waziwazi na viongozi hao kuhusu ubadhirifu unaofanywa na viongozi hao.Waziri huyo ambae alikubaliana wazi na maamuzi ya bunge ya kuundwa kwa kamati ya uchunguzi kuhusu suala hilo la ubadhirifu wa viongozi hao lilizidisha msuguano na viongozi hao.Hata hivyo waziri huyo alionekana kusimamia msimamo wake wa kutaka wahusika wawajibike na hivyo kuzidisha msuguano dhidi ya wabadhirifu hao.

Habari zinasema kuwa mipango ya kuhakikisha anaondolewa katika serikali hiyo ilianza ili kufanikisha ubadhirifu walioukusudia kwani Kawiche alionekana kama ndio kikwazo kwao.Vyanzo vya habari vinaeleza kuwa mipango hiyo ilikuwa ikifanywa kwa usiri mkubwa ingawa waziri huyo alikuwa akiifahamu fika kutokana na intelegensia yake binafsi.Watu walio kuwa wakipanga mipango hiyo ni pamoja na raisi,waziri mkuu,waziri wa fedha,naibu waziri wa wizara ya waziri huyo aliyatambulika kwa jina moja la Lusasi na wabunge wawili ambao huwa wanaitetea sana serikali hiyo bungeni hata kwa hoja zisizo na maslahi kwa wanafunzi au zilizobeba maslahi binafsi ya viongozi hao ambao hata hivyo walishindwa kufamika mara moja.

Habari zinazidi kusema mikakati ya utekelezaji ilianza kwa kuhakikisha waziri mkuu hampi ushirikiano waziri huyo katika utendaji ili kumdhoofisha kiutendaji,hata hivyo mbinu hiyo haikufanikiwa.Wakaamua kwa makusudi kumkosanisha na spika wa bunge ili aonekane mkorofi na aondolewe lakini mbinu hiyo bado haikufua dafu.Ndipo sasa viongozi hao walipoamua kumtumia naibu waziri kuvuruga utendaji wa wizara ijapokuwa mbinu hiyo haikufanikiwa sana kama walivyofikiri.

Taarifa zinazidi kusema kuwa waziri huyo anayesifiwa na wanafunzi pamoja na viongozi mbalimbali katika serikali hiyo kwa utendaji uliotukuka wa kazi alizidi kusimamia misimamo yake hiyo ya kupinga ubadhirifu unaofanywa hasa na raisi huyo.Ndipo walipomtuma naibu waziri wa wizara ya waziri huyo amwombe waziri huyo ampe kiasi fulani cha fedha za wizara ili apeleke kwenye miradi binafsi ya naibu huyo, hata hivyo waziri Kawiche alipinga katakata ombi la naibu waziri huyo na kumwambia hawezi kutoa fedha za wizara kwa shughuli binafsi ndipo naibu huyo akaingia kwenye mgogoro na waziri kawiche.Kusudio la naibu huyo ilikuwa ni Kawiche akubali kumpa fedha hizo ili serikali imuhusishe na ubadhirifu hivyo raisi kupata sababu ya kumwondoa kwa ahadi kuwa kawiche akiondolewa yeye atakuwa waziri wa wizara hiyo, hata hivyo mbinu hiyo ilishindikana.

Vyanzo vya habari vinaendelea kusema kuwa baada ya kuona Kawiche hakamatiki katika mbinu yoyote, raisi kwa kutumia mamlaka yake kikatiba aliamua kumtengenezea kawiche sababu zisizo za kweli na zisizo za msingi na tarehe 6/1/2014 kumuandikia barua ya kumvua uongozi.Kutokana na hali hiyo baadhi ya wabunge,mawaziri na wanafunzi wakiongozwa na makamu wa raisi aliejulikana kwa jina la Benedict Kyando walipinga hatua hiyo ya raisi kwa kuwa walijua ni ya kionevu kwa maslahi ya viongozi hao kuendelea kufanya ubadhirifu ndani ya serikali hiyo.

Hata hivyo kuna tetesi kuwa waziri huyo ameondolewa pia kwa mashinikizo ya CCM udom kutokana na waziri huyo kuhusishwa na harakati za chadema nje ya chuo ambazo ni mwiba mkali kwa chama tawala CCM.

Hata hivyo baada ya waziri kawiche kufuatwa na kuulizwa kuhusu sakata hilo alikataa kuzungumzia lolote na kusema waulizwe wahusika wa serikali wanaotakiwa kutoa taarifa.

NOTE; Kama wasomi ambao hata hawajamaliza masomo wanakuwa wabadhirifu wa mali za uma kiasi hichi ni vipi tukiwakabidhi nchi? ama kweli UDOM ni chuo cha CCM kama wasemavyo wengi.
source;viongozi wa serikali hiyo.
 
Hebu fafanua bunge lipi liloundwa kuchunguza tuhuma za ukwapuaji wa shilingi milioni moja?
Bunge hilo litatumia gharama kiasi gani kumaliza uchunguzi wa tuhuma za ukwapuaji wa shilingi milioni moja?
 
Hebu fafanua bunge lipi liloundwa kuchunguza tuhuma za ukwapuaji wa shilingi milioni moja?
Bunge hilo litatumia gharama kiasi gani kumaliza uchunguzi wa tuhuma za ukwapuaji wa shilingi milioni moja?

hahahahahah
 
Hebu soma bila kukurupuka mkuu sijasema bunge ndio limechunguza nimesema kamati iliyoundwa na bunge.
 
UDOM ni Janga la Taifa...hata wanafunzi wake ni janga la Taifa.
 
Habari za ki shule shule hizo, ngoja niwaachie wanafunzi
 
serikali za vyuo huwa ni mamluki tu, hawana lolote
 
Dah! pole sana Kawiche sisi wanafunzi tunakukubali sana hasa unavyopambana kuhakikisha mikopo yetu inakuja kwa wakati lakini nakutabiria kuja kuwa kiongozi wa kuigwa Africa endelea kupinga ufisadi hata kama upo nje ya hiyo serikali uchwara.
 
serikali za vyuo huwa ni mamluki tu, hawana lolote

Kawaulize Tunisia ndio wanajua kama wanafunzi ni wa kupuuzwa kwa kigezo cha uanafunzi au la kwa taarifa yako wanafunzi ni jeshi la pili la nchi yoyote baada ya majeshi rasmi ya nchi na ni jeshi lenye nguvu zaidi ya majeshi ya dola. Sasa kwa mtu mwenye akili hawezi kizipa kisogo habari zinazohusu wanafunzi kwa sababu tu ni wanafunzi
 
Back
Top Bottom