Kimenuka: Marekani kuishambulia Cuba?

Kimenuka: Marekani kuishambulia Cuba?

Wakusoma 12

JF-Expert Member
Joined
Jul 3, 2017
Posts
5,151
Reaction score
14,490
Rais wa Marekani Donald Trump, amedai kuwa Cuba, ambayo kwa muda mrefu imekumbwa na uhaba wa mafuta kutokana na vikwazo, ni "nchi dhaifu," alisema anaamini ataweza "kukipata" kisiwa hicho.

Akizungumza na waandishi wa habari katika White House, Trump alisema:

"Katika maisha yangu yote, nimekuwa nikisikia kuhusu ajenda ya Marekani dhidi ya Cuba. Watu walikuwa wakisema, 'Marekani itachukua hatua lini?' Ninaamini nitakuwa na heshima ya kuichukua Cuba."

Alipoulizwa alimaanisha nini kwa kusema "kuichukua Cuba," Trump alisema:

"Ndiyo, kuichukua kwa namna fulani, kuikomboa au kuimiliki. Naweza kufanya chochote ninachotaka nayo. Ni nchi dhaifu sana," na akaongeza kuwa Cuba ni "kisiwa kizuri."

Cuba imekuwa kwenye ajenda ya Trump kwa muda mrefu. Rais huyo wa Marekani mara nyingi amekuwa akisema kwamba wataishughulikia Cuba baada ya kufanikisha malengo yao Iran. Serikali ya Cuba, hata hivyo, imeonesha kutoridhishwa na kauli hizo kutoka Marekani.

Wakati huo huo, Rais wa Cuba Miguel Díaz-Canel amesema kuwa mazungumzo yameanza kati ya nchi hizo mbili ili kupunguza mvutano unaoongezeka kati ya Cuba na Marekani.
 
Cuba imekuwa nchi ya hovyo kupita mfano kwa sababu ya huo utawala wa hovyo wa kikomunisti ambao sera yake kuu ni watu kugawana umaskini.

Cuba ya leo haina kabisa tofauti na ile ya 1959 wakati dikteta Fidel Castro anatwaa madaraka ambapo waliamua kuwafuata warusi na kama inavyo fahamika warusi mkiwafuata mnabaki wachoma mahindi tu siku zote.

Matokeo yake Wacuba zaidi ya milioni tatu wakakimbilia Marekani kwenda kutafuta maisha mazuri na ndio hawa wakina Marco Rubio.

Cuba waache ujinga wakubali wachukuliwe na Marekani ili nchi yao ibadilike. Wangekuwa ni mshirika wa Marekani toka zamani leo hii wangekuwa kama South Korea, Taiwan au Singapore na kama ni ule mchezo wa karata tunaweza kusema kwa kujinasibisha na Urusi waliokota hii sio pesa.
 
Nendeni mkavamie mtajua kwanini Vita sio rafiki. Kwa Binadamu. Marekani itaangamia kabisa.%100
 
Africa isipojifunza kuungana na kujitegemea, hawa washenzi watarudi kututawala kimabavu. Inavyoonesha wamenusa hatari ya kutopikika chungu kimoja kweli labda na China. Na labda anatafutwa sasa!
Hawa washenzi wanapanga kurudi mazima tusipokuwa makini, akitokq huyo France atafuata kukusanya visiwa vyake.
Puumbaavu!!!
 
Tatizo viongozi wengi wa kiafrica wamekuwa washenzi zaidi ya wazungu
 
Cuba imekuwa nchi ya hovyo kupita mfano kwa sababu ya huo utawala wa hovyo wa kikomunisti ambao sera yake kuu ni watu kugawana umaskini.

Cuba ya leo haina kabisa tofauti na ile ya 1959 wakati dikteta Fidel Castro anatwaa madaraka ambapo waliamua kuwafuata warusi na kama inavyo fahamika warusi mkiwafuata mnabaki wachoma mahindi tu siku zote.

Matokeo yake Wacuba zaidi ya milioni tatu wakakimbilia Marekani kwenda kutafuta maisha mazuri na ndio hawa wakina Marco Rubio.

Cuba waache ujinga wakubali wachukuliwe na Marekani ili nchi yao ibadilike. Wangekuwa ni mshirika wa Marekani toka zamani leo hii wangekuwa kama South Korea, Taiwan au Singapore na kama ni ule mchezo wa karata tunaweza kusema kwa kujinasibisha na Urusi waliokota hii sio pesa.
Wewe ni mpuuzi sana
 
Huyu mpuuzi DT dunia inamlea naona anarukia rukia kila taifa kama Hitler atakuja kurukia na pasipo rukiwa na kuizamisha kabisa Marekani kama alivyofanya Hitler kwa Ujerumani
 
Back
Top Bottom