Mmawia
JF-Expert Member
- Aug 20, 2013
- 123,233
- 98,194
Bunge lenye wabunge wengi wa ccm na kamati ya maliasili inayoongozwa na mbunge wa ccm iliwaona mawaziri wanahisika kwenye madhila yaliyowapata wananchi wakati wa operation tokomeza. Bunge hilohilo likawaona Muongo na Maswi wanahisika na Escrow. Leo hii serikali inayoongozwa na ccm inawaona wote hawana matatizo na wamesafishwa. Serekali inawaona wabunge na Wananchi kuwa wajinga kabisa haswa baada ya kutumia hela nyingi za walipa kodi kutafuta ukweli wa operation tokomeza na Escrow. Serikali iliwahadaa washirika wa maendeleo kuwa wamechukua hatua juu ya wahusika wa escrow. Na hili ndo Joka la makengeza alikuwa ameshauri kuwa Rais aachiwe achukue hatua baada ya kufanya uchunguzi. Tusubiri October
Nikichekesho sana,