Nadhani suala la CCM kuwasafisha watuhumiwa wa Escrow liko wazi sana kwa mtu yeyote mwenye kutafakari; kwamba CCM wanachotaka kufanya ni kuwashawishi wananchi wasiione CCM kama chama cha ufisadi hasa tunapoelekea kwenye suala la uchaguzi. Hata hivyo, hii inaweza kuwaumiza CCM wenyewe, kwamba badala ya wananchi kuona watuhumiwa wa Escrow hawakuwa na makosa, wataona CCM ni chama cha mafisadi wanaoteteana na kulindana hata wakifanya kosa gani. Sidhani kama CCM walitafakari kwa makini athari za kutaka kuwasafisha watu wa Escrow, wakati Bunge lilishatoa tamko. Infact, ushauri wangu kwa CCM ni kwamba wangetumia hiyo nafasi kusema CCM iko tayari kumwondoa fisadi yeyote ndani ya chama kama walivyofanya kwa watuhumiwa wa Escrow.
Umesema vema, lakini ndani ya ccm nani anaweza kuwa na tafakuri ya hivi?
Hata wale ambao wana mawazo mazuri hawawezi kwa sababu ni wachumia tumbo.
Nobody in ccm will think beyond his nose.