Kimenuka CCM Arusha sasa vipande vipande

Kimenuka CCM Arusha sasa vipande vipande

PISTO LERO

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2011
Posts
2,819
Reaction score
1,455
Muda mfupi baada ya Ikulu kuwasafisha makada waliotuhumiwa kwa kashfa za Tokomeza ujangili na Escrwo wana ccm arusha nao walipuka.

Wanahoji kwanini lowasa hasafishwi kama hao wengine?

Wahiji kwanini lowasa amefungwa mikono na mdomo kisha anaambiwa apigane?

Wanachama hao wa ccm arusha wanahoji kwanini ikulu iwasafishe Maswi,mhongo na wengine lakini haijawahi kudhibitisha wala kukataa tuhuma zilizoelekezwa kwa lowasa?

Wataka na lowasa asafishwe lasivyo pata chimbika.
 
Atasafishwa tu kwani kwa CCM kusafishana ni jadi leo kesi ya Mramba na wenziwe akina mgonja ina miaka kumi haijaisha ila Farijara anaongezewa miaka tu kila wakati anapopaswa kutolewa
 
Nadhani suala la CCM kuwasafisha watuhumiwa wa Escrow liko wazi sana kwa mtu yeyote mwenye kutafakari; kwamba CCM wanachotaka kufanya ni kuwashawishi wananchi wasiione CCM kama chama cha ufisadi hasa tunapoelekea kwenye suala la uchaguzi. Hata hivyo, hii inaweza kuwaumiza CCM wenyewe, kwamba badala ya wananchi kuona watuhumiwa wa Escrow hawakuwa na makosa, wataona CCM ni chama cha mafisadi wanaoteteana na kulindana hata wakifanya kosa gani. Sidhani kama CCM walitafakari kwa makini athari za kutaka kuwasafisha watu wa Escrow, wakati Bunge lilishatoa tamko. Infact, ushauri wangu kwa CCM ni kwamba wangetumia hiyo nafasi kusema CCM iko tayari kumwondoa fisadi yeyote ndani ya chama kama walivyofanya kwa watuhumiwa wa Escrow.
 
Atasafishwa tu kwani kwa CCM kusafishana ni jadi leo kesi ya Mramba na wenziwe akina mgonja ina miaka kumi haijaisha ila Farijara anaongezewa miaka tu kila wakati anapopaswa kutolewa
Usitumie kichwa kufugia tu nywele
 
kila siku sisi kina gogo la shamba tunasema hila za ccm ndio zinazokizamisha chama chao,sasa leo kwa kutumia hila ya kuwasafisha ni wazi wananchi wataona ccm hawawezi na hawana uwezo wa kuwachukulia hatua wanaokwenda kinyume na maadili katika chama chao, hilo ni pigo kubwa sana kwa ccm na niongezeko miongoni mwa mambo yatakayowatoa magogoni
 
Muda mfupi baada ya Ikulu kuwasafisha makada waliotuhumiwa kwa kashfa za Tokomeza ujangili na Escrwo wana ccm arusha nao walipuka.

Wanahoji kwanini lowasa hasafishwi kama hao wengine?

Wahiji kwanini lowasa amefungwa mikono na mdomo kisha anaambiwa apigane?

Wanachama hao wa ccm arusha wanahoji kwanini ikulu iwasafishe Maswi,mhongo na wengine lakini haijawahi kudhibitisha wala kukataa tuhuma zilizoelekezwa kwa lowasa?

Wataka na lowasa asafishwe lasivyo pata chimbika.

huo uwongo waliosafisha tokomeza/escrow ni tume richmond iliundiwa tume ikkuta na lowasa kutuhumiwa
 
Wapendwa katika Bwana wala msilalamike kuhusu CCM kusafishana, usafi wao ni kweny maandishi ila mioyoni wa Watanzania wanaoteseka na uovu huu, hakuna aliye msafi na kwa kushupaa shingo huku kwa CCM ndio kutasababisha mlipuko wa hasira za wananchi, siku hazigandi na tarehe zinayoyoma kwa kasi kuelekea october, mafuriko ndani ya CCM hayazuiliki hata waweke kingo za namna gani, tayari CCM i hoi kwa mgawanyiko wa wao kwa wao, kilichobaki ni kwa mpinzani wake kumalizia palipobaki na CCM kubaki historia.........Mungu atubariki katika hili, tukeshe tukiomba kwani saa ya ukombozi ni sasa.
 
Takataka moja kuisafisha takataka nyingine iko kazi, msanii kubeza sanaa iko kazi, WAMBIENI HAO WANACCM ARUSHA FISADI HUENDA HASAFISHIKI HATA KISANAA SANAA TU, kama inawauma wajiunge CHADEMA haraka, na waache wizi.
 
Walichofanya ni kuwaongezea Ukawa hoja za kupeleka kwa wananchi zikiwa na mifano hai
 
Bunge lenye wabunge wengi wa ccm na kamati ya maliasili inayoongozwa na mbunge wa ccm iliwaona mawaziri wanahisika kwenye madhila yaliyowapata wananchi wakati wa operation tokomeza. Bunge hilohilo likawaona Muongo na Maswi wanahisika na Escrow. Leo hii serikali inayoongozwa na ccm inawaona wote hawana matatizo na wamesafishwa. Serekali inawaona wabunge na Wananchi kuwa wajinga kabisa haswa baada ya kutumia hela nyingi za walipa kodi kutafuta ukweli wa operation tokomeza na Escrow. Serikali iliwahadaa washirika wa maendeleo kuwa wamechukua hatua juu ya wahusika wa escrow. Na hili ndo Joka la makengeza alikuwa ameshauri kuwa Rais aachiwe achukue hatua baada ya kufanya uchunguzi. Tusubiri October
 
erroo...muna nyima lowassa kuwa raisi wa nshii hii...

washaa hiyo rafiki
 
Back
Top Bottom