Kimenuka au kimenukia?

Kimenuka au kimenukia?

Herbalist Dr MziziMkavu

Platinum Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
43,114
Reaction score
34,956
attachment.php


Kwa tukio hili, vijana wa mjini wanasema; kimenuka! Hivi karibuni wanawake watano ambao majina yao hayakuweza kufahamika mara moja walinaswa usiku mnene wakifanya mapenzi na wanaume wawili kwenye chumba kimoja kilichopo Mwananyamala jijini Dar.

attachment.php

Watu hao walinaswa katika…


Kwa tukio hili, vijana wa mjini wanasema; kimenuka! Hivi karibuni wanawake watano ambao majina yao hayakuweza kufahamika mara moja walinaswa usiku mnene wakifanya mapenzi na wanaume wawili kwenye chumba kimoja kilichopo Mwananyamala jijini Dar.

Watu hao walinaswa katika oparesheni kabambe iliyoongozwa na Kamanda Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Kinondoni, OCD Wilbroad Mtafungwa pamoja na Ofisa wa Oparesheni, Inspekta Jacob Swai.
Katika zoezi hilo, polisi walivamia kambi kuu inayotajwa kusheheni wanawake wanaojiuza iliyopo Mwananyamala A ambapo ‘wauza sukari’ hao hutumia vyumba vyao kufanya ufuska huo.

Polisi hao walipofika kwenye chumba kimoja kilichopo eneo hilo, walikumbana na upinzani mkubwa wa watu waliokuwa ndani na baada ya kufanikiwa kuufungua mlango, waliwakuta wanawake watano na wanaume wawili wakiwa kimahaba.

Mbali na hao, polisi walifanikiwa kuwanasa wanawake wengine kwenye vyumba vyao na baadhi mtaani wakijiuza ambapo walipewa kibano cha hali ya juu.

Imeelezwa kuwa, wanawake hao wamekuwa na tabia ya kujiuza na wakati mwingine hukubali kufanya mapenzi na wanaume zaidi ya mmoja, hali ambayo ni hatari sana.

Mkazi mmoja wa eneo hilo, Husein Juma alisema: “Kwanza tunampongeza Kamanda Mtafungwa kwa operesheni hii, wanawake hawa wamekuwa ni tatizo kwani wamekuwa wakijiuza waziwazi na kutupa ovyo kondomu.

Naye Inspekta Swai alisema wamekuwa wakipokea malalamiko kutoka kwa wananchi wa eneo hilo wakaona ni vyema kuyafanyia kazi ambapo waliwakamata zaidi ya watu 35, wanawake kwa wanaume wanaohusika. Global Publishers
 

Attachments

  • k?MENUKA JAMAN?.jpg
    k?MENUKA JAMAN?.jpg
    70.1 KB · Views: 2,511
  • walinaswa.jpg
    walinaswa.jpg
    60.8 KB · Views: 322
  • aibu tupu.jpg
    aibu tupu.jpg
    45.7 KB · Views: 896
lakini pia naona askari wa kiume amkamata dada wa watu kimahaba, sheria jamani...............
 
Do! hii noma! yaani live bila chenga lakini mbona mateja hawakamatwi alafu mimi sijaona kama wamevunja sheria yeyote kwani maswala ya mapenzi si makubaliano ya anayetenda na anayetendewa, mbona wahakamatwi wauza gongo na wapo na posili wanajua
 
Back
Top Bottom