Kimei miezi 4 kama miaka 5

Kimei miezi 4 kama miaka 5

SautiYaMnyonge

JF-Expert Member
Joined
May 13, 2018
Posts
439
Reaction score
742
Mbunge wetu wa vunjo mzee charles kimei amefanya kazi nyingi sana katika kipindi hiki kifupi kuliko mbatia aliyekaa miaka 5. Amejitofautisha sana kwani kila mara hurejea jimboni kufanya mikutano ya wananchi na kusikiliza kero pamoja na kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa au kushiriki shughuli za kijamii.

Amefanikiwa kuzitafutia ufadhili wa ukarabati shule tatu za msingi kupitia mashirika ya Tanzania Rising na Helpapp toka nchi ya Israel taifa teule. Ukarabati kila shule ni takribani milioni 32.5

Amefanikisha ujenzi wa vivuko 4 vya takribani milioni 6 kila kimoja kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo wa ndani ya jimbo la vunjo akiwemo olotu, rotary club mwika, madiwani wa vunjo, na wanavunjo wanaoishi nje ya jimbo hilo.

Amefanikiwa kupata miradi toka serikalini ya ujenzi wa madarasa matatu kwa kila shule, vyoo na maabara kwa zaidi ya shule nne toka fedha za EP4R...

Ujenzi wa kituo cha afya kata ya kahe ambacho kipo kwenye hatua ya kupaua...

Amefanikiwa kupata mradi wa ujenzi wa tenki la maji la zaidi ya ujazo wa lita laki moja, uwekaji mtandao mpya wa mabomba, Ujenzi wa vilula 21, nk huko makame juu kata ya kilema kaskazini

Amechangia shilingi milioni nne ujenzi wa hosteli za wasichana shule ya sekondari ghona..

Amechangia shilingi milioni mbili upauaji wa madarasa shule ya sekondari mashingia.. amechangia milioni 8.1 uwekaji tiles na umeme jengo la ofisi vicoba vunjo

Hizi fedha za kuchangia sio za mfuko wa jimbo ni za mfukoni kwake ...

Amegawa vifaa vya michezo nk


Yaani, hata mwaka bado mambo ndio haya kweli yeye ni mtendaji sio mpiga maneno...

Vunjo tuliyoitamani imeanza kuonekana...karibuni tumuunge mkono mbunge wetu dr kimei
IMG-20210329-WA0062.jpg
IMG_20201014_194154_422.jpg
IMG-20201119-WA0062.jpg
IMG_20210403_111246_861.jpg
IMG-20210328-WA0144.jpg
 
Back
Top Bottom