nngu007
JF-Expert Member
- Aug 2, 2010
- 15,860
- 5,803
na Chalila Kibuda
SERIKALI inatarajia kujenga reli za Kimara, Goba na Mbagala kwa mwaka wa fedha 2014/2015 ili kuwasaidia wananchi wa maeneo hayo kuondokana na adha ya usafiri.
Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe alieleza hayo jana alipotembelea kukagua uharibifu wa reli uliotokana na mvua zinazoendelea kunyesha jijini Dar es Salaam.
Mwakyembe alisema wananchi wa Dar es Salaam wamekuwa na changamoto ya usafiri wa kufika mjini inayosababishwa na msongamano wa magari na kuathiri shughuli za biashara na huduma za kijamii.
Dk. Mwakyembe alisema usafiri wa treni umerahisisha usafiri ambapo kujengwa reli katika maeneo mengine itakuwa ni neema, kwani wananchi wataondokana na adha hiyo.
Alisema baada ya kuharibika kwa njia ya reli ya Ubungo, huduma ya usafiri itarejea katika hali ya kawaida baada ya kumalizika kwa ukarabati.