Return Of Undertaker
JF-Expert Member
- Jun 12, 2012
- 4,572
- 26,868
Watu waliojitambulisha kuwa ni Askari polisi (bila kuonesha vitambulisho) wakiwa na silaha za moto wamewakamata madaktari wawili, Dr. Chriss Cyrilo (kushoto) na Dr. Shindo Kilawa (kulia) wakiwa maeneo ya Mbezi jijini Dar usiku huu.
Watu hao hawakutaja sababu za kuwakamata, zaidi ya kutumia nguvu kuondoka nao kwa gari aina ya Defender. Nimewasiliana na Polisi kituo cha Mbezi lakini wamekanusha kuwashikilia madaktari hao.
Tafadhali sambaza taarifa hii kwa ajili ya usalama wao, na tushirikiane kupaza sauti ili ijulikane walikopelekwa na sababu za kukamatwa kwao. #Justice4CyriloAndKilawa
Updates FROM YERRICKO NYERERE
Kelele zetu zimesaidia Makamanda wetu @dr_chriscyrilo na Dr. Shindo Kilawa wameachiwa na polisi Kimara Temboni, ajabu kesi yao wameambiwa ni uzurulaji.
Hawa ni Madaktari Professional walichelewa kurudi kwao wakiwa Muhimbili ambako kamanda mwenzetu Brock Karume amelazwa kwa ajali, walipofika Mbezi wakakamatwa kwamba ni wazurulaji hadi kufikishwa Kimara Temboni, sauti zetu zikafanya waachiwe!