Kimachale machale ndio mpango mzima.

Kimachale machale ndio mpango mzima.

Sijajua haya mapenzi mwisho wa siku inakuaje! sijui ndivyo ilivyokuwa hata kwa wazee wetu ujanani mwao au haya ya enzi hizi yamezidi!! .....
Naambiwa zamani hali ilikuwa ni tofauti maana binti kuolewa ilikuwa ni must kabla ya kuzaa na kuweka kitambaa cheupe juu ya kitanda ilikuwa ni fahali kubwa kwa wazazi wa binti. Binti hawakuwa na tamaa ya kununua gari au kujenga nyumba bali zawadi za mabinti ilikuwa hankachifu na mafuta ya vaselini. Wazazi wa binti hawakutegemea kupata fedha kila mwezi kutoka kwa mabinti zao bali vijana wao. Kuolewa kwa binti ilikuwa ni mwisho wa kuwa katika familia ya kwao na mwanzo wa kuwa katika familia ya mume wake. Hii yote imekufa kifo cha mende, na hata ukisoma makala nyingi za akinamama hapa JF ni ubingwa wa ki-Mohamed Ally kuwa na mabwana wengi wakisingizia kuwa wanatumia DUME ingawa kiuhalisia ni kavukavu ambapo uzeeni kansa ya kizazi inawasubiri kwa kuchanganya yale maji ya uzima kutoka kwa watu mbali mbali. Kwa sasa mabinti wengi wanazaa watoto wao na kuendelea na maisha bila kuwekwa ndani. Wengi wetu miaka 22 kama Njilinji hatuwajui baba zetu na maisha yanasonga mbele.

My take: Ukiishi Roma fanya kama waroma waishivyo. Mawazo ya kuoa mpaka kifo kiwatenganishe hayapo bali mpaka hamu ya kugegedana ikiisha ndo iwatenganishe, ndo mpango mzima. Nadhani umenipatatata -Karibu Njinjo.
 
Mh! Eti mletewe wengine unadhani nani anawaharibu kama siyo nyie wenyewe? Think twice!! Labda humtoshelezi mahtaji yake ndo mana anaminjemba mingine! Think again!!Chamsingi muombe mungu akupe binti mtulivu ! Masuala ya kuishi et kimachale mguu ndani nje kama sungura porini anayeogopa mishale c kujikosesha amani huko?tulizanaaa!!
 
women are cheating now days aiseee ........never seen before
 
Tatizo wanawake malaya na wanaume malaya ndiyo maana kila mtu analalamika, wanawake waache umalaya watulie na mpenzi moja na wanaume waache umalaya watulie na mpenzi moja. Tatizo kila mtu yupo kimachale, mwanamke kimachale na mwanaume kimachale .We need change , the change it start wth you. mimi nimeamua kuwa na mpenzi moja tu ambaye ni mke wangu wa ndoa , ndoa yetu inamiaka kumi na nne, tunaaminiana, tunauhuru na simu zetu, mke wangu anaweza kutumia simu yangu mda wowote anaotaka hapa mimi pia.
 
Kimachale machale ndio style ya mahusiano siku hizi. Ukijiweka mzima mzima kama kiroba cha mpunga shauri yako, itakula kwako. Last weekend yaliyo nikuta ni majanga. Ningekuwa nimejiweka mzima mzima sasa hivi ningekuwa kula sili, kulala silali, kuoga siogi, kulia silii, maumivu tu kwenda mbele. Miezi sita iliyopita nilimpata msichana wa kumwandaa kuwa mama wa watoto wangu. Siyo mkali kihivyo, si mnajuwa tena mawife wetu tunapenda wawe wa namna gani. Kumbe tunajidanganya kweli walahi, kwa sababu wanaume wa siku hizi wengi wanaangalia yule si mwanamke, ile kitu si anayo bhaaasssiii!!

Katika kurutubisha penzi nimekuwaa nikimtoa mtoko mara kwa mara, sasa weekend iliyopita nikamtoa mtoko Fulani wa kwenda kupata dinner na kinywaji. Tukaagiza kuku wa kuwoka kwa sababu ni chakula apendacho, kisha tukaagiza vinywji. Punde tulipo maliza kula nikachukua simu yake kuangalia games kwa sababu nilisha wahi mueleza mimi ufukunyuku wa simu sina. Nikaanza kucheza game wakati yeye anaconcentrate na maongezi pamoja na kupata masanga, punde nikapata wazo la kwenda kwenye text message. Akuweza kunotice kwa sababu nilikuwa nasoma huku vidole vyangu vyote viwili vipo kwa phone as if nacheza game. Kwa bahati nzuri simu ilikuwa silent.

Nilicho kiona, nilitamani ardhi ifunguke na kunimeza haraka sana. Text message za manjemba tofauti tofauti, moja ikisema tukutane RoyalVillage hotel itakuwa powa. Mwili wangu ulitetemeka sana, haraka sana nikachukuwa beer yangu nikanywa ili nisionekane nipo tofauti. Nikarudi fasta kwenye game mode. Nikaiweka simu mezani akaichukuwa faster, kuangalia akaona nipo busy na game

Toka tuachane siku ile nimempiga kibuti cha kimya kimwa
kama lara 1 alivyo tueleza katika uzi wake.

Wana MMU kimachale machale ndio mpango mzima, mapenzi ya kuumizana yamepitwa na wakati. Ila nimejifunza, ukiwa mfumyuku sana wa kutaka kujua kila kitu walahi uwezi kuoa
Tusiwachunguze
sana bata, kwa sababu siku hizi mapenzi ni kama makunguru. Kuyafuga ayawezi kaniki.


Tumuombe sana Mungu, ikiwezekana awatoe wadada wote waliopo duniani kisha atuletee wengine labda watakuja na mfumo mwingine kabisa ambao utakuwa nafuu kwa sisi vijana.
mambo mengine tunajitakia halafu tunalalamika, hivi wewe umetoka out na mpenzi wako badala ya kuwa busy na mpenzi wako unakuwa busy na gemu, kwanini usinunue gemu zile za watoto ukawa unatoka nayo? maana mpenzi wako hana umuhimu zaidi ya gemu, kwa hiyo na yeye ana wengine wanaomuona ni wa muhimu kwao. ukiona mwanamke anakucheat ujue kuna sababu, wanawake huwa ni waaminifu sana, may be unamtoa hiyo out ya mara moja kwa wiki halafu matumizi haumpi, kwa hiyo anawakumpa matumizi ila kwa vile anakupenda anakuvulia tu. jichunguze kwanza wewe ni wapi unakosea sio kulaumu laumu tu.
 
Back
Top Bottom