Kimachale machale ndio mpango mzima.

Kimachale machale ndio mpango mzima.

kwamtoro

JF-Expert Member
Joined
Nov 15, 2010
Posts
4,922
Reaction score
3,245
Kimachale machale ndio style ya mahusiano siku hizi. Ukijiweka mzima mzima kama kiroba cha mpunga shauri yako, itakula kwako. Last weekend yaliyo nikuta ni majanga. Ningekuwa nimejiweka mzima mzima sasa hivi ningekuwa kula sili, kulala silali, kuoga siogi, kulia silii, maumivu tu kwenda mbele. Miezi sita iliyopita nilimpata msichana wa kumwandaa kuwa mama wa watoto wangu. Siyo mkali kihivyo, si mnajuwa tena mawife wetu tunapenda wawe wa namna gani. Kumbe tunajidanganya kweli walahi, kwa sababu wanaume wa siku hizi wengi wanaangalia yule si mwanamke, ile kitu si anayo bhaaasssiii!!

Katika kurutubisha penzi nimekuwaa nikimtoa mtoko mara kwa mara, sasa weekend iliyopita nikamtoa mtoko Fulani wa kwenda kupata dinner na kinywaji. Tukaagiza kuku wa kuwoka kwa sababu ni chakula apendacho, kisha tukaagiza vinywji. Punde tulipo maliza kula nikachukua simu yake kuangalia games kwa sababu nilisha wahi mueleza mimi ufukunyuku wa simu sina. Nikaanza kucheza game wakati yeye anaconcentrate na maongezi pamoja na kupata masanga, punde nikapata wazo la kwenda kwenye text message. Akuweza kunotice kwa sababu nilikuwa nasoma huku vidole vyangu vyote viwili vipo kwa phone as if nacheza game. Kwa bahati nzuri simu ilikuwa silent.

Nilicho kiona, nilitamani ardhi ifunguke na kunimeza haraka sana. Text message za manjemba tofauti tofauti, moja ikisema tukutane RoyalVillage hotel itakuwa powa. Mwili wangu ulitetemeka sana, haraka sana nikachukuwa beer yangu nikanywa ili nisionekane nipo tofauti. Nikarudi fasta kwenye game mode. Nikaiweka simu mezani akaichukuwa faster, kuangalia akaona nipo busy na game

Toka tuachane siku ile nimempiga kibuti cha kimya kimwa
kama lara 1 alivyo tueleza katika uzi wake.

Wana MMU kimachale machale ndio mpango mzima, mapenzi ya kuumizana yamepitwa na wakati. Ila nimejifunza, ukiwa mfumyuku sana wa kutaka kujua kila kitu walahi uwezi kuoa
Tusiwachunguze
sana bata, kwa sababu siku hizi mapenzi ni kama makunguru. Kuyafuga ayawezi kaniki.


Tumuombe sana Mungu, ikiwezekana awatoe wadada wote waliopo duniani kisha atuletee wengine labda watakuja na mfumo mwingine kabisa ambao utakuwa nafuu kwa sisi vijana.
 
mapenzi yana stage

sasa kama hamuishi pamoja na hata posa hujapeleka

why unaanza ku act kama mume?

Sija muuliza kitu chochote up to now. Kwa sababu natambua is just a girlfreind. sina mamlaka ya kumuuliza sababu siyo wife wangu.

 
Mh simu yako haina games?? Ndo ukome "usichokijua kamwe hakiwezi kukudhuru"
 
mapenzi yana stage

sasa kama hamuishi pamoja na hata posa hujapeleka

why unaanza ku act kama mume?

hakajakua bado hako, ni kavulana

kwanza eti yupo na demu wake then anacheza game ? inaingia akirini

huyu atakua anajiaandaa na mtihani wa Form two mwezi ujao
 
We acha tu..dunia imebadilika mkuu..labda umchonge wako..!
 
Sijajua haya mapenzi mwisho wa siku inakuaje!
sijui ndivyo ilivyokuwa hata kwa wazee wetu ujanani mwao au haya ya enzi hizi yamezidi!! kwamtoro kaka kwa muda wa miezi sita kama wewe nimekaa na binti kwa heshima na upendo, nikimwaminisha kua sitaki kumchezea, nipo siriaz nae na focus zangu ni awe Mrs.Tasia.
wakuu mabadiliko yakaanza, nisipofanya kie mawsiliano yeye hata wiki yaweza isha. kukomaa nikapewa jibu kua its over.
kiukweli nilishangaa hadi nikacheka, anyway, maisha yanasonga.
 
Last edited by a moderator:
hakajakua bado hako, ni kavulana

kwanza eti yupo na demu wake then anacheza game ? inaingia akirini

huyu atakua anajiaandaa na mtihani wa Form two mwezi ujao


upo wewe mrembo?
tutafutane basi kikubwa lol
 
kwakweli silaha kubwa ambayo ninajitahidi kua nayo kwa dunia ya sasa ni kujifunza ku-relax
na kutatu matatizo yangu bila pressure, kujaribu kuwaza kwa namna chanya,
dunia imekua na stress nyingi sanaaaaaaa, maisa ni magumu, sio ofisdi, sio biashara, sio ukulima, kila kitu changamoto zimekua kubwa sana.
sasa mapenzi ndio yalikua faraa ya hizi changamoto ila kwa sasa mapenzi yamekua namba moja kati ya sources za stress
kwa hyo hapa ni ku-relax. nakula zangu maisha taratibu.
 
Kuna watu kwa makusudi wana nia ya kuharibu uzi huu, kama mtaona auwahusu piteni kimya kimya. Wa kwanza ayanda
Please, please
 
Last edited by a moderator:
Hahaha mie nimependa hiyo paragraph ya mwisho. Kweli tunahitaji some new shit, izi sijui 40th end azichukue kwakweli.
 
Kimachale machale ndio style ya mahusiano siku hizi. Ukijiweka mzima mzima kama kiroba cha mpunga shauri yako, itakula kwako. Last weekend yaliyo nikuta ni majanga. Ningekuwa nimejiweka mzima mzima sasa hivi ningekuwa kula sili, kulala silali, kuoga siogi, kulia silii, maumivu tu kwenda mbele. Miezi sita iliyopita nilimpata msichana wa kumwandaa kuwa mama wa watoto wangu. Siyo mkali kihivyo, si mnajuwa tena mawife wetu tunapenda wawe wa namna gani. Kumbe tunajidanganya kweli walahi, kwa sababu wanaume wa siku hizi wengi wanaangalia yule si mwanamke, ile kitu si anayo bhaaasssiii!!

Katika kurutubisha penzi nimekuwaa nikimtoa mtoko mara kwa mara, sasa weekend iliyopita nikamtoa mtoko Fulani wa kwenda kupata dinner na kinywaji. Tukaagiza kuku wa kuwoka kwa sababu ni chakula apendacho, kisha tukaagiza vinywji. Punde tulipo maliza kula nikachukua simu yake kuangalia games kwa sababu nilisha wahi mueleza mimi ufukunyuku wa simu sina. Nikaanza kucheza game wakati yeye anaconcentrate na maongezi pamoja na kupata masanga, punde nikapata wazo la kwenda kwenye text message. Akuweza kunotice kwa sababu nilikuwa nasoma huku vidole vyangu vyote viwili vipo kwa phone as if nacheza game. Kwa bahati nzuri simu ilikuwa silent.

Nilicho kiona, nilitamani ardhi ifunguke na kunimeza haraka sana. Text message za manjemba tofauti tofauti, moja ikisema tukutane RoyalVillage hotel itakuwa powa. Mwili wangu ulitetemeka sana, haraka sana nikachukuwa beer yangu nikanywa ili nisionekane nipo tofauti. Nikarudi fasta kwenye game mode. Nikaiweka simu mezani akaichukuwa faster, kuangalia akaona nipo busy na game

Toka tuachane siku ile nimempiga kibuti cha kimya kimwa
kama lara 1 alivyo tueleza katika uzi wake.

Wana MMU kimachale machale ndio mpango mzima, mapenzi ya kuumizana yamepitwa na wakati. Ila nimejifunza, ukiwa mfumyuku sana wa kutaka kujua kila kitu walahi uwezi kuoa
Tusiwachunguze
sana bata, kwa sababu siku hizi mapenzi ni kama makunguru. Kuyafuga ayawezi kaniki.


Tumuombe sana Mungu, ikiwezekana awatoe wadada wote waliopo duniani kisha atuletee wengine labda watakuja na mfumo mwingine kabisa ambao utakuwa nafuu kwa sisi vijana.

pole mkuu!
 
Uki search simu ya demu wako ni kama unategua mabomu tena Nyuklia ujiandae kua na ant-missile(yalinikutaga hayo sikuwahi hata siku moja kupekua siku niliyopekua ndo hiyohiyo tuliyoachana)

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Kimachale machale ndio style ya mahusiano siku hizi. Ukijiweka mzima mzima kama kiroba cha mpunga shauri yako, itakula kwako.........

Tumuombe sana Mungu, ikiwezekana awatoe wadada wote waliopo duniani kisha atuletee wengine labda watakuja na mfumo mwingine kabisa ambao utakuwa nafuu kwa sisi vijana.

Yaani mkuu vijana wenye mawazo ya kimachalemachale mletewe wadada wapya, kweli mkuu. Kama ni hiyo ni suluhu kwa nini msiondolewe wote wakaja wakaka na wadada wapya?
 
Back
Top Bottom