Kima cha chini mishahara ya walimu kinakidhi-Mdau | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kima cha chini mishahara ya walimu kinakidhi-Mdau

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by Mahesabu, May 9, 2011.

 1. Mahesabu

  Mahesabu JF-Expert Member

  #1
  May 9, 2011
  Joined: Jan 27, 2008
  Messages: 5,043
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  Na Abdul Mitumba

  8th May 2011
  Walimu wa Shule za Msingi na Sekondari katika wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma, wamekiri kuwa kima cha chini cha mshahara anacholipwa mwalimu anayeanza kazi kwa mara ya kwanza ni kikubwa kuliko cha mtumishi yoyote wa serikali ukimuondoa wa sekta ya afya.
  Ukweli huo ulijitokeza mjini hapa, wakati walimu walipotoa ushahidi mbele ya Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Tamisemi) Elimu, Kassim Majaliwa, kufuatia kuzuka mjadala ulioambatana na malalamiko kuwa walimu ndiyo watumishi wanaolipwa mishahada duni zaidi kuliko mtumishi yoyote serikalini.
  Aliyesababisha siri ya walimu kulipwa zaidi ni mwalimu Thomas Majumba, ambaye alimtaka Naibu Waziri aeleze kwa nini serikali inawaonea walimu kwa kuwalipa mishahara duni huku wana taaluma wengine wenye viwango sawa vya kitaaluma kutoka sekta nyingine wakilipwa fedha nyingi.
  Kufuatia malalamiko hayo, Naibu Waziri Majaliwa alisema siyo kweli kuwa walimu wanapunjwa mishahara na kwamba kwa sasa ndiyo watumishi wanaolipwa vizuri pamoja na wale wa sekta ya afya.
  "Mimi sitaki niseme kwamba mshahara mnaolipwa unatosha la hasha, lakini ninachosema na ndiyo ukweli wenyewe kwamba mshahara wenu ni mkubwa kulinganisha na sekta nyingine mkiondoa sekta ya afya pekee," alisema na kuzua minong'ono ndani ya ukumbi huo.
  Kisha akamtaka mwalimu anayeanzakazi mwaka huu kutoa ushahidi kwa kutaja kiwango chake cha mshahara.
  Ndipo akasimama mwalimu mwenye taaluma ya shahada ya kwanza, ambapo alisema ameanza na mshahara wa Sh.490, 000 kwa mwezi wakati mwenye stashahada analipwa Sh. 280, 000 hatua ambayo iliwazima kabisa midomo walimu hao.
  Baadaye akamsimamisha afisa utumishi wa wilaya ya Tunduru ambapo alisema mtumishi mwingine asiye mwalimu au wa sekta ya afya anaanza na kiwango cha mshahara cha Sh.180, 000 kwa mwezi, hivyo kuonyesha walimu wapo juu zaidi.
  Akizungumzia hilo, Majaliwa alisema siyo kweli kwamba serikali haiwajali walimu na kwamba kila kukicha inafanya kila namna ya kuboresha maslahi yao kwa kuwaweka katika viwango tofauti vya mishahara.
  Majaliwa yupo mkoani Ruvuma kuzungumza na walimu, wakuu wa idara mbalimbali, wanafunzi wa shule za msingi na sekondari na wazazi ili kuwahimiza umuhimu wa elimu kwa watoto na taifa kwa ujumla.  CHANZO: NIPASHE JUMAPILI

  ngazi ya cheti je analipwaje ?
   
Loading...