Kima cha chini cha 300,000 ni kwaajili ya chakula cha mtu mmoja tu. Huu ni ukatili uliobarikiwa na viongozi

Bonde la Baraka

JF-Expert Member
Sep 22, 2016
4,580
7,938
Kichwa chajieleza.

Kuna baadhi ya watumishi Serikalini hulipwa kwa kima cha chini, yaani 300,000 Sh. Fedha hii ukikata makato ya NHIF, PAYEE na mfuko wa hifadhi ya jamii mhusika anabakiwa kama 260,000 Shs. Ukiigawa kwa siku za mwezi unapata kama 8000-8500 per day.

Hii ni fedha ya chakula tu kwa mtu mmoja ndo maana inafanana na ile wanayopewa wanafunzi wa Chuo kikuu kwaajili ya chakula.

Huyu mtu hana mke/Mme?
Huyu mtu hatumii usafiri kwenda kazini?
Huyu mtu halali(halipii pango)?
Huyu mtu hanunui/havai nguo?
Huyu ndiye anayeambiwa achape kazi. Nazi gani?

Usije hapa ukasema kuna overtime allowances. Overtime hulipwa kisheria na inalipwa kwa kuwa umeutumia muda wa mtu.

Bodi inayopanga mishahara pamoja na viongozi wa nchi ndio chanzo cha unyanyasaji huu.

Kwenye makampuni binafsi ndo usiseme, full kutesana.
Kuna taaasisi hasa Mashirika ya umma wanajitahidi kwa kuwapatia watumishi wao mahitaji muhimu.

Kuna watumishi wa umma ukimwona mtaani unaweza ukamdhani ni kuli wa bandarini au mchoma tofali, amechoka kwa ugumu wa maisha.

Note: Usiache kazi hata kama mazingira ni magumu kama hujui unaenda kufanya mini huko uendako.
 
Kichwa chajieleza.
Kuna baadhi ya watumishi Serikalini hulipwa kwa kima cha chini, yaani 300,000 Sh. Fedha hii ukikata makato ya NHIF, PAYEE na mfuko wa hifadhi ya jamii mhusika anabakiwa kama 260,000 Shs. Ukiigawa kwa siku za mwezi unapata kama 8000-85000 per day.
Hii ni fedha ya chakula tu kwa mtu mmoja ndo maana inafanana na ile wanayopewa wanafunzi wa Chuo kikuu kwaajili ya chakula.
Huyu mtu hana mke/Mme?
Huyu mtu hatumii usafiri kwenda kazini?
Huyu mtu halali(halipii pango)?
Huyu mtu hanunui/havai nguo?
Huyu ndiye anayeambiwa achape kazi. Nazi gani?
Usije hapa ukasema kuna overtime allowances. Overtime hulipwa kisheria na inalipwa kwa kuwa umeutumia muda wa mtu.
Bodi inayopanga mishahara pamoja na viongozi wa nchi ndio chanzo cha unyanyasaji huu.
Kwenye makampuni binafsi ndo usiseme, full kutesana.
Kuna taaasisi hasa Mashirika ya umma wanajitahidi kwa kuwapatia watumishi wao mahitaji muhimu.
Kuna watumishi wa umma ukimwona mtaani unaweza ukamdhani ni kuli wa bandarini au mchoma tofali, amechoka kwa ugumu wa maisha.
Note: Usiache kazi hata kama mazingira ni magumu kama hujui unaenda kufanya mini huko uendako.
Kwani kigezo cha malipo ya mshahara yanatokana na ukubwa wa mahitaji ya mtu au tija kwenye kazi?
Nauliza tuu.
 
Kuna mishahara watu tunalipwa basi tu Siku ziende tusikae nyumbani bure
 
Kwani kigezo cha malipo ya mshahara yanatokana na ukubwa wa mahitaji ya mtu au tija kwenye kazi?
Nauliza tuu.
Kwani neno tija kwenye utumishi wa umma unalitafsiri vipi?.
Hata wenye shahada bado wanalipwa fedha kiduchu sana kwa taasisi nyingi. Je, hizi taasisi hazina tija?
Au wasomi waliopo taasisi hizi zinazolipa wafanyakazi kwa schedule ya serikali kuu hawana tija?.
 
Hivyo basi usizaliane hovyo bila ya mpango kama huwezi hata kununua chakula!
Ndugu vipi wewe? Una matatizo ya akili nini?
Nimetoa general feature wewe unakuja kuniambia nisizaliane hovyo. Do you know me?
Nimekuambia Mimi ndiye mwathirika? Hata kama ningekuwa mimi ndiye muhusika jibu lako liko kisheria au kikanuni?.
 
Kwani kigezo cha malipo ya mshahara yanatokana na ukubwa wa mahitaji ya mtu au tija kwenye kazi? Nauliza tuu.

Mkuu, kinachosikitisha ni kwamba serikali haichukui hatua yeyote dhidi ya waajiri ambao wanawalipa watu mishahara chini ya kiwango cha serikali cha kima cha chini.

Labda serikali itoe ufafanuzi na kutuambia inaposema mshahara wa kima cha chini ni Tshs 300,000. KImsingi, sio kwa ajili ya taasisi za serikali tu, ni mshahara unaotakiwa kulipwa kama kima cha chini pamoja na waajiri katika sekta binafsi

Kima cha chini maana yake ukiajiri mtu usimplipe chini ya Tshs 300,000 kwa mwezi - hata kama ni housegirl nyumbani, kwa muliozioea kuwalipa Tshs 15,000 hawa wadada.
 
Kaka mimi niliuza swali tu lakini hukunijibu.
 
Kwani kigezo cha malipo ya mshahara yanatokana na ukubwa wa mahitaji ya mtu au tija kwenye kazi?
Nauliza tuu.
Mshahara unatakiwa ukutoshe kulipa kodi ,usafiri,chakula na mavazi kutokan na kiwango chako. Kamba wewe ni wa ngazi ya chini ukutoshe kula hata you ugali na maharage kwa lunch na dinner na pia kukaa nguo zako za mafundi bila kusahau breakfast ya uji wa mapande. Iishe kulipa chimba japo cha nyumba ya udongo
 
Kama ni hivyo basi nawe unapaswa kumlipa mfanyakazi wako wa ndani kwa kutumia kigezo hicho hicho
 
Back
Top Bottom