Kilio pesa za korosho kisikilizwe

kidati

Member
Feb 2, 2013
86
20
Kwa muda wa miezi mitatu sasa wananchi wa kusini wamekua wakililia pesa zao za korosho bila majibu kwa kuwa hata baadhi ya waliopata wamepaya baadhi ya minada.

Swali kubwa wanalojiuliza wakulima hawa ni kuwa kwa nini malipo haya yanachelewa wakati korosho imeshauzwa na tena waliahidiwa kuwa hakuna mfumo wa stakabadhi ghalani ?

Jambo pekee wanaloomba wananchi hawa ni kuharakishwa kwa pesa zao ili zisaidie maandalizi ya kuwapeleka watoto shuleni pia kumudu gharama za ujenzi ambao kimsingi walalahoi wengi wameonekana kutaka kufanya hivyo ukizingatia simenti ya dangote imeshaanza kusambaa huku madukani.

Tafadhali wadau na wahusika Kama mnatusikia mfanye hima kuwalipa wakulima hawa maskini kwa wakati
AHSANTENI
 
Serikali ya CCM ni ya kilaghai sana. Kuna rafiki yangu ameniambia kwamba ameuza korosho zake pale Likokona AMCOS (wilayani Nanyumbu) toka mwanzoni mwa mwezi Oktoba, hadi leo imepita miezi mitatu pesa anazisikia redioni tu.
 
Kwani walete mbuzi waliokuwa wananyweshwa soda hawajanenepa tu. .??...vipi bodaboda walizonunua Je.. ziko juu ya mawe. .??
 
Back
Top Bottom