Kilio kwa Wasaliti - Watanzania Jiandaeni Kununua Nyama!

Boreless

Member
Aug 25, 2009
61
39
Jogoo awike, asiweke lazima kutakucha. Na zamu hii hakuna salia Mtume (S.A.W). Shoka alilinoa mwenyewe na wenzake wamemsaidia kuelekeza shingo yake kibra. Kazi ya mchinjaji ni ndogo sana. Na hili ni suala la kungoja muda tu uliowekwa uishe, shoka lipite shingoni. Haijalishi itamwagika damu kiasi gani, mnyama lazima achinjwe ili chombo kikombolewe na kiweze kusonga vema na wanyama safi. Ghalama za kuendelea kumfuga mnyama huyu muovu ni hatari kwa uzao wote, ukombozi na maendeleo ya nchi.

Kuna watu waona, hawatambui; wanasoma, hawaelewi; wanatazama hawaoni. Mfano hii tungo ya Azavel Lwaitama sijui wangapi wanaielewa?
Azavel Lwaitama
….pale unapotaka kuwaondoa madarakani tena kwa kucheza nje ya uwanja wa mchezo wa siasa unaofuata sheria zinazotungwa na wale wale ambao kwa wakati huo ndio wenye uwingi wa kura katika vikao halali za chama husika……
Niwadokeze; katika vikao vya Kamati Kuu mnyama wetu huwa ni mbishi sana na hupenda kupingana na kila hoja ya Mkuu za zizi. Ili kufikia tamati huru, Mkuu wa zizi amekuwa akilazimika kwa miaka kadhaa kuhitimisha hoja zinazopingwa na Mnyama kwa kupiga kura ya siri. Wajua matokeo huwaje? Hakuna hata mara moja ambapo mnyama amewahi kumshinda Mkuu wa Zizi! Hata hili suala la uamuzi wa hatua za awali kuelekea machinjioni liliamliwa kwa kura na mnyama akashindwa vibaya sana tena kwa aibu. Hivyo msitegemee mnyama atapona zamu hii.

Wenye meno andaeni pesa kula nyama, tena anzeni kuelekea buchani. Kama ambavyo ilitabiriwa na Ben Saanane toka kitambo, wakati wenye zizi watakapokuwa wanashangilia na kula mishkaki, wachungaji wa zizi jirani, waliokuwa wakizisifia pembe za mnyama wa mwenzao na kumnenepesha kichwa watakuwa wakisigina meno kwa maumivu. Kuna ndama wengi pia wataugua maana kuishi kwao kulitegemea maziwa yaliyozalishwa na huyu mnyama. Baada ya kuchinjwa, ndama hawa watalazimika kutafuta aina nyingine ya chakula zaidi ya maziwa na itabidi wajibidiishe kutafuta wenyewe. Hiki ndicho kilikuwa kilio kikubwa kilichosababisha moja ya beberu kutaka lijitwishe zigo lote ili mnyama abaki kwenye mlija, kazi na ujira viendelee kupatikana.

Tuachane na porojo za mnyama. Hivi mnajua kuwa umeme unapanda bei kwa asilimia 68%? Ohoho! Shauri yetu. Tumekaa kujadili hitimisho la ajira za mnyama tukasahau mambo ya msingi yanayogusa maisha ya kila Mtz na yanatuathiri kwa muda mrefu!

Sasa hivi hata usalama wa Taifa kitengo cha propaganda kimeenda likizo maana maandalizi ya siku ya kuchinja yamewafanya watz kuwa busy kiasi cha kusahau maisha mengine. Wapiga deal pia serikalini huu ndiyo muda wao wa kufanya mambo. Mkija kurudi kwenye mambo ya msingi, mtakuta kila Mtz anadaiwa TZS 500,000/=!

Dr.W.Slaa leo ukiongelea maandalizi ya kuchinja bila kuzungumzia suala la umeme sitakuelewa kabisa.
 
Too low
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom