Kilio kikuu Migodini

Echolima

JF-Expert Member
Oct 28, 2007
3,826
2,057
Kwa wiki sasa kumekuwa na Mtafaruku katka migodi mingi kama vile GGM, NORTH-MARA, BULYANHULU, TULAWAKA na BUZWAGI hii inatokana na habari kuwa mifuko ya jamii kama vile NSSF, PPF na mingine itaacha kuwalipa wafanyakazi mafao yao pindi watakapofukuzwa au kuacha kazi wenyewe mpaka watakapo fikisha miaka 60.

Kutokana na hali halisi ya kazi zao inakuwa ngumu sana kuweza kuipata hiyo haki yao wakiwa na zaidi miaka 60 maana Mazingira ya kazi yao mara nyingi ni ya hatari sana na yana madhara ya baadaye.

Mbali na hayo waajiri wao mara nyingi sana huwa wakati mwingine wanafukuza wafanyakazi ovyo-ovyo, kama sheria hii itapita basi itasababisha maafa makubwa sana kwa wafanyakazi wengi.

Kwa sababu sasa hivi bado kuna kikao cha WABUNGE wetu tunaomba waweke nyuma malumbano yao waliangalie upya suala hili walinde maslahi ya wafanyakazi kwa ujumla, kwa sasa sheria iliopo mtu akiacha au kufukuzwa kazi alikuwa analipwa mafao yake yote bila matatizo.
 
Hivi NSSF wanasemaje juu ya Uvumi huu?
Mkurugenzi Mkuu Bw. Ramadhan Dau, yuko wapi na anasemaje juu ya hili?
NSSRA, wakiwa ni "Mamlaka ya Udhibiti Mifuko ya Hifadhi ya Jamii" nao wanasemaje juu ya hili?
Waziri wa Fedha naye anasemaje juu ya Kadhia hii iliyoanza kama rumours na sasa imekuwa Kweli?

Update, Kule NYAMONGO (Mara) wafanyakazi walioacha kazi Mgodini, baada ya jana Kwenda NSSF kufungua madai yao, wamekataliwa kupokelewa madai yao na wameambiwa eti "hadi wafikishe miaka 55." Hivi nchi hii mbona mambo ni Shaghalabaghala, iweje jambo zito kama hili likaanzishwa bila taarifa rasmi??? Hivi hata kwenye "issue" kama hii tunaleta SIASA???
 
Kwa taarifa tu ni kwamba hii sheria ilishapitishwa na kusainiwa na rais na inafanya kazi. Ukiacha au kuachishwa kazi hakuna kuchukua mafao yako hadi ufikishe umri tajwa (miaka 55 kwa hiari na 60 kwa lazima). Habari ndio hiyo na kwa sababu wafanyakazi wa Tanzania hawana mtetezi basi maana yake ni kwamba wahesabu maumivu tu!
 
Kwa taarifa tu ni kwamba hii sheria ilishapitishwa na kusainiwa na rais na inafanya kazi. Ukiacha au kuachishwa kazi hakuna kuchukua mafao yako hadi ufikishe umri tajwa (miaka 55 kwa hiari na 60 kwa lazima). Habari ndio hiyo na kwa sababu wafanyakazi wa Tanzania hawana mtetezi basi maana yake ni kwamba wahesabu maumivu tu!

Hii ni barua ya jana tarehe 20/07/2012 kutoka SSRA.
UFAFANUZI KUHUS FAO LA KUJITOA KATIKA MAREKEBISHO YA SHERIA ZA MIFUKO YA HIFADHI YA JAMII.

Ufuatao ni ufafanuzi mfupi kuhusu marekebisho ya Sheria za Mifuko hasa kuhusu fao la kujitoa.

1. Kama mtakumbuka Sheria za Mifuko ya Hifadhi ya Jamii pamoja na Sheria ya Mamlaka zimefanyiwa marekebisho na kupitishwa na Bunge tarehe 13 Aprili, 2012. Sheria hiyo tayari imeshasaininiwa na Mheshimiwa Rais na imeanza kutumika rasmi. Marekebisho haya yanawahusu wafanyakazi wote nchini mwetu bila kubagua sekta yoyote ile.

2. Kwa mujibu wa marekebisho hayo fao la kujitoa (withdrawal benefits) yamefutwa na kuanzia sasa hayatakuwepo. Mafao hayo yalikuwa yanatolewa pale mwanachama alipokuwa anaacha kazi. Sasa mwanachama wa Mfuko atapata mafao yake pale atakopfikisha umri wa kustaafu kwa hiari (miaka 55) au kwa lazima (miaka 60) au pale anapopata ulemavu wa kudumu.

3. Kwa kuzuia fao la kujitoa mwanachama anapata fursa ya kupata mikopo ya nyumba kwa kutumia dhamana ya michango yake kama ilivyoelezwa kwenye Sheria ya SSRA kipengele cha 38.

4. Marekebisho hayo kuhusu kuzuia mafao ya kujitoa yamefanyika ili kutimiza lengo na madhumuni ya hifadhi ya jamii ambayo ni kuhakikisha kuwa mwanachama anapostaafu anapata mafao bora yatakayomwezesha kumudu maisha ya uzeeni wakati ambapo nguvu ya kufanya kazi tayari imeshamwishia. Mafao ya kujitoa yanapunguza na hata kuondoa kabisa kinga ya mfanyakazi pale anapoumia kazini au anapofika uzeeni.

5. Tunawaomba muwaelimishe wafanyakazi umuhimu na madhumuni ya mafao ya hifadhi ya jamii. Hifadhi ya jamii ni nyenzo mahususi iliyowekwa kuwasaidia wafanyakazi kuendesha maisha yao wakati wanapokuwa wameishastaafu tayari. Umasikini wa kipato wakati wa uzee ni mojawapo ya changamoto ngumu kukabiliana nazo kwa mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla. Tunawasihi tena muelimishe wafanyakazi kuhusu jambo hili. Tafadhali msisite kuwasiliana na Mamlaka pale ufafanuzi zaidi utakapohitajika.

6. Kwa kuwa marekebisho hayo yamesainiwa na kuanza kutumika rasmi kama sheria, mafao ya kujitoa hayawezi kutolewa tena na wafanyakazi watakaoacha kazi kwa sababu ya marekebisho ya kipengele hicho watakuwa hawajaijitendea haki wao wenyewe na pia itakuwa ni kunyume cha Sheria. Mamlaka inaandaa kanuni za mafao ambayo lengo lake ni kuboresha maslahi ya wanachama, kanuni hizo zitajadiliwa na wadau wakiwemo vyama vya wafanyakazi na waajiri ili kupata maoni yao.

7. Tafadhali muwaelimishe wafanyakazi kwamba pamoja na kuzuia fao la kujitoa, mafao mengine ambayo ni muhimu kwa sekta ya Madini yataendelea kutolewa kama kawaida. Mafao hayo ni Kama vile kuumia kazini pamoja na fao la ulemavu.

8. Tumesikia kwamba tayari kuna hofu imejijenga kwa wanachama kuhusiana na fao la kujitoa. Ikumbukwe kwamba baadhi ya Mifuko ilikuwa inatoa fao hilo kinyume cha Sheria kwani katika Sheria zao hakuna fao la kujitoa. Tunapenda kusisitiza kwamba wanachama wawe watulivu wakisubiri miongozo.

9. Tunapenda kuwahakikishia kwamba katika hili maslahi ya wanachama yatalindwa na hakuna mwanachama atakayepunjika kutokana na utaratibu huo. Mamlaka imepanga kutembelea wafanyakazi wa sekta ya madini katika juma la kwanza la mwezi Agosti 2012 ili kutoa ufafanuzi zaidi kwa wanachama wote.

Tunatanguliza shukrani za dhati kwa ushirikiano.

Wenu.
Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Hifadhi ya Jamii.

Irene Isaka
MKURUGENZI MKUU
 
Mgodi wa Resolute Tanzania Limited, yaani Golden Pride Mining, ulioko Km 18 nje ya mji wa Nzega, mkoani Tabora unafungwa mwaka huu Desemba 2012. Kwamaana hiyo wafanyakazi wote walio-chini ya 55 - 60 itawabidi wasubiri saaanaaa ili kuja kupata mafao yao.. Anyway, Mungu awaezeshe kuwa hai hadi wakati huo ili wachukue haki yao..

 
Haiwezekani, watu wenyewe wa kufikisha miaka 55 wako wapi? magonjwa na hali halisi ya kazi na maisha kwa ujumla are not favourable for mine workers kufikisha umri huo wakiwa wanafanya kazi. Hata private companies almost zote hakuna sehemu wanapenda kufanya kazi na vibabu/vibibi vyenye umri huo.................sidhani kama hiyo sheria imepitishwa labda walikatwa vichwa!

CEOs wa hii mifuko waongee wasikike!
 
Haiwezekani, watu wenyewe wa kufikisha miaka 55 wako wapi? magonjwa na hali halisi ya kazi na maisha kwa ujumla are not favourable for mine workers kufikisha umri huo wakiwa wanafanya kazi. Hata private companies almost zote hakuna sehemu wanapenda kufanya kazi na vibabu/vibibi vyenye umri huo.................sidhani kama hiyo sheria imepitishwa labda walikatwa vichwa!

CEOs wa hii mifuko waongee wasikike!

Mkuu, kwenye mchango wangu hapo juu, ufafanuzi wa SSRA unasema sheria hii ni kwa wafanyakazi wa sekta zote. Mods wangeweza kutusaidia kubadilisha kichwa cha uzi huu ili kisomeke hivyo kwa vile wafanyakazi wa sekta zingine wanaweza wakahisi hili haliwahusu. Hiki ni kilio kwa wafanyakazi wa sekta zote na si migodini tu.
 
Sina tatizo na maamuzi yao, cha msingi serikali itimize wajibu wake kwa wananchi katika huduma.
Ajira iwe dhamana kwa mfanyakazi hapo sawa!.
 
Madai makubwa ya wafanyakazi ilikuwa ni ku-harmonize formula za kutoa mafao ya uzeeni ili zifanane mifuko yote. Ni hili ndilo lililosababisha kuundwa kwa SSRA, na kazi kubwa ilikuwa kupitia mifuko yote na kushauri/pendekeza formula ambayo ingetumiwa na mifuko yote ya hifadhi ya jamii.

SSRA baada ya kuundwa ingefanyia kazi DAI hili kubwa la wafanyakazi na kupeleka bungeni ili litungiwe sheria.

Huyu Mama Irene badala kufanyia kazi dai hilo sasa ameanza kundandia mambo mengi kabisa ambayo hayakuwa priority ya wafanyakazi kama hili la kuondoa mafao ya kujitoa.

Huu ni UPUMBAVU mkubwa wanafanya SSRA. Tunataka SSRA wa-harmonize formula ya kutoa pesheni ya uzeeni sio kuja na sarakasi hizi. Wanachama wa NSSF, PPF tunataka na sisi tupewe malipo mazuri ya uzeeni kama wenzetu wa PSPF. Mama Irene kama huwezi kufanya hili ondoka hapo unakula kodi zetu bure!
 
Back
Top Bottom