Kilio hiki bwana Lowassa utakilipia kabla ya 2015

Kilio hiki bwana Lowassa utakilipia kabla ya 2015

Nitake radhi. Mie sio tapeli. Na sijawahi kukopi kazi ya mtu kisha niitangaze kuwa yangu. Na kubwa zaidi nimeridhika na elimu ndogo niliyonayo badala ya kuzusha "nimesoma Urusi" (labda anasema Urusi ili msimwongeleshe Kiingereza)
Tunataka pravda...! Hatutaki longolongo.
 
Ila Chahali kwa kiasi kikubwa umepoteza imani ya kuaminiwa.
Nitabaki kusomaa maandiko yako kwa umakini mkubwa.

Mbona mliongea hivyohivyo wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu wa mwaka 2015, kwamba nimepoteza kuaminiwa kwa vile sikuisapoti Chadema? Here I am. Well and alive. Nilianza uandishi mwaka 1998 - takriban miaka 20 sasa - na kamwe sikuwahi kufanya vitu kwa minajili ya kumpendeza mtu. Sijawahi kuandika kitu ili niaminike.

Na kama kuna tukio ambalo lingenifanya niumizwe na "kutoaminika" ni lililonitokea February 2013, nikaLazimika kuweka hadharani kilichonisibu, nikaishia kuambiwa "nahadaa watu ili nipate makazi UK." Nyie Waswahili hamna maana. Na mtu yeyote atakayejihangaisha kufanya kitu ili aaminike au apendwe anapoteza muda wake.

Hivi hao wahuni wa kisiasa mnaowapeleka Dodoma kila miaka mitano wanaaminika? Mbunge wako anaaminika? Ni wangapi miongoni mwenu msioaminika kwa wenza wenu? Na wangapi mnajiamini wenyewe, let alone kuwaamini wenzetu? Mie si mwanasiasa kwamba "mniamini kisha mnipe kura zenu." Hapana. Atakayeamua kusoma ninachoandika, poa.Ataayepuuza ni poa pia. Life goes on.

Kitu pekee nyie waswahili mnaamini ni UBUYU. Kama Rais wenu alimudu kutamka hadharani kuwa anamwamini mtu aliyefanya uhalifu kwa kuvamia kituo cha redia, na mtu huyhuyo amefoji jina na cheti cha elimu, kuna haja kweli ya KUAMINIWA katika tanzania yetu?

By the way, ukipata wasaa nenda HAPA kisha tafakari tena: huyu ni kweli huyu mtu haaminiki?
 
Umefilisika kiwango hiki mkuu? Jamaa ndio wamegoma kabisa kukulipa 12m yako kabisa au Bashiru amekubali kukulipa?
wewe Lowassa alikukatia kiasi gani maana unajisahaulisha kuwa haukuwa unamtukana lakini leo wewe ndo mlamba miguu wake.
 
Umefilisika kiwango hiki mkuu? Jamaa ndio wamegoma kabisa kukulipa 12m yako kabisa au Bashiru amekubali kukulipa?
Mkuu naona unachungulia na kusepa, mithili ya ka-mwizi kanakovizia kupora kuku wa kisasa nyumbani kwa balozi wa mtaa.
Hoja zote za uzi wako mwenyewe umezikimbia. Chezea siasa weye!😀😀
 
wewe Lowassa alikukatia kiasi gani maana unajisahaulisha kuwa haukuwa unamtukana lakini leo wewe ndo mlamba miguu wake.
Yericko amekuwa mdogo kama piritoni. Halafu mbona hajawahi kuwaeleza nini kilitokea kipindi kile "alipopotezwa"? Siku Chadema watapojua ukweli would be too late.
 
Yericko nina ishu yako na KATAMBI. Nakustahi
Kwa Yericko siwezi shangaa, maana ilishahitimishwa kwamba anaendeshwa na njaa. Nashauri Mkuu uifumue tu issue yake na Patrobas, maana hata kwenye kambi ya upinzani walishamtema kiaina huyu.
 
Yericko amekuwa mdogo kama piritoni. Halafu mbona hajawahi kuwaeleza nini kilitokea kipindi kile "alipopotezwa"? Siku Chadema watapojua ukweli would be too late.
Hahahaaaaa... Watu kama nyie ndo mnaturudisha nyuma tz is full of conspiracy
 
Back
Top Bottom