Punainen
JF-Expert Member
- Jul 19, 2013
- 1,303
- 1,056
Wakati Yeriko anamsemea Lowassa haya maneno yasiyofaa kuna mliokuwa mnamtetea Lowassa! Lowassa alipohamia CHADEMA mmemgeuka mnampinga wakati Yeriko amegeuka anamuunga mkono....mna tofauti gani nyie?! Mzee wa push-up alipokuwa anawaahidi kuwa ataunda mahakama ya mafisadi kwa sababu wameiumiza nchi hii mlikuwa mnarukaruka kwa shangwe! Sasa hivi kwa nini yeye wala ninyi hamuiongelei hiyo mahakama? Sasa hivi hamsemi lolote kuhusu nyoka wa makengeza, ni mwenyekiti wa bunge lenu tukufu...lakini akihamia upinzani itakuwa balaa. Lowassa hadi 2015 alikuwa mwenyekiti wa kamati ya bunge ya mambo ya nje, hebu tuonyesheni mlimpinga wapi? Sisi wengine tunachotaka ni kuwa na serikali yenye kuwajibika kwa raia, yenye kusimamia sheria kwa haki. Yeyote anayestahili kushitakiwa ashitakiwe na apewe stahili yake bila kujali ni Lowassa au ni nani, bila kujali ni ccm, upinzani au hana chama. Msituambukize ule ugonjwa wa dom kuwa akitukana wa upinzani anaadhibiwa, ila akitukana wa ccm hakuna tatizo!