Kilio chetu tuliokuwa wanachu wa St. Joseph

JOHN RAYMOND

Member
Jul 18, 2015
31
19
. KILIO CHETU

*Ujumbe huu uufikie umma.*

Mnamo tar 19/02/2016 Serikali kupitia Tume ya vyuo vikuu (TCU) ili vifungia vyuo vikuu vishiriki vya Mt Joseph tawi la Songea na Arusha wanafunzi hao walihamishiwa katika vyuo vikuu tofauti ikiwemo Chuo kikuu cha Dodoma.

Ni baada ya kuchukua hatua stahiki kufuatilia matatizo yetu yanayotukumba katika ngazi mbalimbali za kiuongozi ili kutatua changamoto zetu lakini mpaka sasa hatuelewi ni nani atakaye tusaidia tunapenda kuujulisha umma kuwa serikali imetutelekeza tunataka umma ulitambue hilo. Sisi ni waalimu wa masomo ya sayansi na hisabati, tusiopungua 203. Ni idadi ambayo ni kubwa Sana na yenye athari katika jamii.

''Tunaukumbusha umma kuwa ni baadhi ya wanafunzi tuliohamishiwa katika Chuo kikuu cha Dodoma (UDOM) hasa tuliokuwa mwaka wa Tatu(3) tukarudishwa mwaka mmoja wa masomo''

Leo hii hatutambuliki Kama tumerudia mwaka..! Na imepelekea hadi sasa tunafanya mafunzo kwa vitendo(field) bila kupewa hela wakati ni haki yetu kupata maana bado ipo ndani ya bajeti yetu ya masomo. " Je serikali ulikuwa mpango wako kutuhamisha kwa nia ya kututesa na kutupotezea ndoto yetu ya kimasomo?
"
Hatuamini macho yetu kwa hili linaloendelea.
wenzetu tuliokuwa tunatumia mtaala ule ule serikali inawatambua na wamefanikiwa kumaliza wakati sisi tumekataliwa na kufutiwa matokeo yetu yote na kulazimika kurudia au kusoma miaka miwili ndani ya mmoja tena kwa muda mfupi tena bila pesa zozote ikiwemo ya field tuliyonayo sasa huku wazazi wetu ambao ni wakulima tena wadogo wakiubeba mzigo huu mkubwa, hatujui hatma yetu nini sisi tulioitwa watoto wa kambo.

Wazaz wanalazimika kuuza mashamba ili watoto wao wajimudu katka vituo vyao vya masomo ya mafunzo.

Pia imepelekea tukawa na maswali mengi maana hadi sasa hatujui nini hatma yetu kwa sisi wanufaika wa mkopo Kama mkopo wetu upo kwa mwaka wa masomo ujao. Kwani hii inadhihilisha kuwa endapo serikali haitawajibika kwa hili jambo kuna hatari ya kutoendelea na masomo kwa mwaka ujao hii ni kutokana na kukosa hela ya kujikimu pamoja na malipo mengine ambayo ni pamoja na ada (fee).

Tumefuatilia Sana Bodi ya mkopo (loan board), Tume ya vyuo vikuu (TCU) na wizara ya Elimu (wizarani) lakini majibu tunayopewa ni kwamba hawatambui kuwa tumerudishwa mwaka hivyo wafuatilie. Mpaka leo hii tumeonekana ni wahanga ambao hatuna pakupatiwa ufafanuzi na ufumbuzi wa tatizo letu,

kwani umma utambue kuwa tangu mwezi wa tisa (9) tarehe12, 2016 tupo vituoni bila hata hela ya kuendeshea haya mafunzo kwa vitendo tunazidi kupaza sauti zetu ili Serikali ilitambue hilo

Tupo katika mazingira magumu tena sana! ombi letu lisikike hata katika vyombo vya habari ili liweze patiwa ufumbuzi haraka na mapema ili kunusuru maendeleo yetu kitaaluma.

TUNAIPENDA SANA TANZANIA YETU
 
Back
Top Bottom